Alhamisi, 3 Julai 2014

NEW AUDIO MO MUSIC BASI NENDA

NEW AUDIO DIAMOND-KITORONDO

NEW AUDIO ALLY NIPISHE-MSHAMBA

Huyu hapa Mchezaji mwingine wa Yanga aliyehamia Azam Fc.

Taarifa ambayo imekua kama ya ghafla ni kuhusu Aliyekuwa mchezaji kiungo wa Yanga Athumani Iddi ‘Chuji’ kijiunga na timu ya Azam Fc na asubuhi ya leo ameonekana akiwa mzoezini Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
Azam ni timu yenye mafanikio makubwa sana katika ulimwengu wa soka kwa kipindi kifupi tangu ilipoanzishwa timu hiyo. Na mleta habari wako Tony Power.

Kilichosemwa na Dudubaya kwa madai ya Kufukuzwa,kupitia You heard ya July 03.

Taarifa ya kuripotiwa polisi kwa Dudubaya imetoka muda mchache baada ya mwanamke wake kupokea vitisho kadhaa,Soudy Brown ameongea na Dudubaya baada ya madai haya kutoka,ingawa kwa ujumla ya mazungumzo Dudubaya amekana yote yaliyosemwa na mwanamke huyo.
 

KAMPUNI YA TTCL YATWAA TUZO YA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
Muonekano wa Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo. Namtayarishaji wako Nickson Luvega.

MFARANSA AJA TANZANIA KUONYESHA UMAHIRI WA KUCHEZA MPIRA WA MTAANI

Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn’s John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha staili mbali mbali za kucheza mpira mbele ya waandishi wa habari. Namtayarishaji wako Nickson Luvega.

MAMBO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

Muonekano wa lango kuu la kuingia ndani ya banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana kwa kupewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Utajiuliza kwani LG wapo ndani ya Banda la MeTL Group kwenye maonyesho ya Sabasaba kwa sababu MeTL Group wamekuwa Mawakala waliothibitishwa Tanzania nzima (Authorized Dealers) kuuza vifaa vya LG nchini. 
Kampuni ya MeTL Group inahusika pia na masuala ya Vitenge, Khanga, Mashuka na n.k Njoo upendeze mwanamke na vitenge bora na imara kutoka MeTL Group…..Sikukuu ya Eid ilee na maandalizi yawe mapema kabisa…!,(A.I).Na mleta habari wako Nickson Luvega kutoka Dar es Salaam.

AJARI YA GARI MAENEO YA POSTA IRINGA

Ni ajali ambayo imehusisha gari mbili aina ya Suzuki Carry na Toyota inayomilikiwa na Asas, hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.

MBUNGE APIGWA RISASI MOGADISHU

Kundi la al-shabab limesema limempiga risasi na kumuua mbunge mmoja maarufu mjini Mogadishu.
Ahmed Mohamud Hayd aliuawa na watu waliokua ndani ya gari, wakati akitoka hoteli aliyofikia  katika eneo linalolindwa vikali, wamesema watu walioshuhudia. Mlinzi wake pia ameuawa na msaidizi mmoja kujeruhiwa. Mtoa habari wa youngluvega.blogspot.com Paul Luvega amesema mauaji ya bwana Hayd- ambae ni kamanda wa zamani wa kijeshi na pia ni waziri- yameshtusha wengi duniani kote.