Ni moja kati ya wasanii waliofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Tanzania kwa mwaka 2014 toka Kilimanjaro.Ramjey ndo jina lake katika sanaa akiwa amemshirikisha Rita ngoma yake inakwenda kwa jina la Sijajua kosa langu ambayo imefanywa na producer Malwo kutoka studio ya Sunlight.Ni msanii ambae amejaaliwa sauti nzuri na anaitendea haki kwa ngoma kali aliyoiachia hivi karibuni.Ili kuiskiliza ngoma ya huyu mkali toka Kilimanjaro mkoa ambao haubahatishi katika muziki DOWNLOAD hapa chini ili uweze kusikiliza.
Jumanne, 2 Desemba 2014
Hii ni kuhusu matokeo ya zoezi la upimaji wa kilevi kwa madereva wa mabasi Ubungo
Lile zoezi ambalo lilianzishwa na Jeshi
la Polisi Tanzania kukagua madereva wanaoendesha mabasi ya abiria kwenda
mikoani kama wanatumia kilevi leo limefanyika kwa ghafla katika Kituo
cha Mabasi cha Ubungo.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1
imesema zoezi hilo limetoa majibu kwamba madereva wamekuwa na uelewa
juu ya athari za matumizi ya kilevi wakiwa wanaanza safari.
Unaweza kuisikiliza hapa taarifa hiyo niliyokurekodia wakati habari hiyo ikirushwa hewani.
BARNES:GERRAD BADO MZURI KWA LIVERPOOL
Winga wa zamani wa Klabu ya
Liverpool John Barnes anaamini kiungo na nahodha wa timu hiyo Steven
Gerrard, bado ni mzuri vya kutosha kuendelea kuitumikia liverpool
"Katika hatua hii ya kazi yake, bado ni bora kabisa na uzuri wa kutosha kwa ajili ya Liverpool bado," Barnes alisema.Barnes alitumia misimu 10 katika uwanja wa Anfield kabla ya kuondoka na kujiunga na Newcastle United katika umri ambao anao Gerrard hivi sasa.
Pamoja na ufanano wa umri ambao Barnes aliihama liverpool winga huyo anaimani Gerrard ana nafasi yakuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka atakapostaafu soka.
"Bila shaka tunajua ubora wa Gerrard ulivyokua nyuma, na tunajua nini huwatokea wachezaji wengi wanapofika mwisho wa kazi zao,bado ni mchezaji muhimu sana kwa klabu ya Liverpool”.
tayari liverpool kupitia meneja wake Brendan Rodgers imetangaza kumpa ofa ya mkataba mpya. Steven Gerrard utakao muwezesha kumalizia kipaji chake kwa majogoo wa jiji la London.
Aliyewakosoa Sasha na Malia ajiuzulu
Mfanyakazi katika chama cha
Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu
wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia
kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.
Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.
Mwanamke huyo akiomba msamaha, alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha mwenendo wangu, '' alisema Lauten.
MKE WA KIONGOZI IS AKAMATWA
Vikosi vya usalama nchini Lebanon
vimemkamata mkewe kiongozi wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la IS Abu
Bakr al-Baghdadi karibu na mpaka na Syria na mwanawe mvulana.
Jeshi
linasema kuwa Mkewe Baghdadi alikamatwa pamoja na mwanawe ingawa majina
yao hayajatolewa. Walikamatwa na wakuu wa ujasusi baada ya kuingia
Lebabon siku kumi zilizopita.Jarida la al-Safir liliripoti kuwa mkewe Baghdadi anahojiwa katika ofisi za waizara ya usalama nchini Lebanon.
Mnamo mwezi Juni, Baghdadi alitajwa kama kiongozi wa kundi hilo katika maeneo ya Syria na Iraq ambayo yanadhibitiwa na IS.
Mwezi jana kundi hilo lilikannusha madai kuwa kiongozi huyo aliuawa au kujeruhiwa, katika shambulizi la angani lililofanywa na majeshi ya Marekani, mjini Mosul.
Kundi lenyewe lilitoa kanda ambapo lilisema utawala wao unapanuka na kutoa wito kwa wapiganaji wa jihad kujitolea mhanga.
Jarida lililoripoti kukamatwa kwa mkewe Baghdadi, limesema kuwa maafisa wa usalama walikuwa wameiweka operesheni yao kama siri kubwa kiasi kwamba hakuna aliyekuwa na taarifa kuhusu operesheni yenyewe.
Mwandishi wa BBC Jim Muir, ambaye yuko, anasema kuwa kukamatwa kwa mkewe Baghdadi na mwanawe kutawaweka katika hali tatanishi ambayo inaendelea kuibuka Lebanon.
Kundi la IS pamoja na kundi lengine la jihad al-Nusra linawazuilia wanajeshi 20 wa Lebabon kama mateka.
Al Shabaab waua 36 Mandera,Kenya
Kundi la wanamgambo nchini Somalia
Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye
machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Katika
taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao
wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya
Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.
Inaarifiwa kuwa wafanyakazi hao walipigwa risasi wakiwa katika mahema ya. Walioshuhudia shambulizi walisema kwamba wapiganaji hao waliwatenga waisilamu na wakristo huku wakiwachinja baadhi, na kuwapiga risasi wlaiosalia.
Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi eneo hilo, amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa Kenya.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine wanne wamejeruhiwa.
Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo.
Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya kigaidi.