Ikiwa imepita siku moja toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama
mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na
uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi.
Klabu ya Young Africans imemshitaki Emmanuel Okwi kwenye Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka
Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia
mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili
na Yanga.
Kiungo
wa kimataifa wa Spain Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern
Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada
ya uhamisho wa paundi millioni 5.
Alonso ambaye alijunga na Real Madrid
akitokea Liverpool ametambulishwa rasmi leo hii kwenye mkutano waandishi
wa habari na kutoa sababu ambayo imemfanya mpaka akaamua kuondoka
Santiago Bernabeu.
Kiungo huyo ambaye juzi alitangaza
kujiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Hispania amesema kwamba
kilichomfanya kuhama Madrid sio upinzani wa namba kama inavyodhaniwa na
wengi.
“Klabu haikutaka niondoke, ulikuwa uamuzi wangu mwenyewe kuondoka.
Baada ya kushinda La Decima, nilihisi nahitaji changamoto mpya. Nilihisi
muda wa kuondoka umefika,” Alonso aliwaambia waandishi wa habari.
“Sikuamua kuondoka kwa sababu ya ujio wa Toni Kroos. Madrid wamefanya
usajili mzuri sana na tungecheza wote kwa muda mwingi. Hivyo sikuondoka
kwa sababu yake, nilihitaji tu changamoto mpya.
“Bayern ndio lilikuwa chaguo sahih kwangu mimi.” – Alonso
Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na
nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali
kuondoka katika timu hiyo.
Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kwa ada ya
uhamisho ambayo ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza – £50m
akitokea Liverpool – leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo
sasa anajiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkataba wa mkopo wa
miaka miwili.
Torres anajiunga na AC Milan kwenda kurithi nafasi ya Mario Balotelli ambaye amejiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa £16m.
Torres ameichezea Chelsea mechi 172 na kufanikiwa kuifungia magoli 45 tangu alipotia mguu Stamford Bridge.
Mchezaji huyo anategemewa kutua Milan leo tayari kufanyiwa vipiko vya afya.
Siku
hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo
flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha
malalamiko yao na mfano mzuri ni hivi karibuni kwa Wanafunzi wa kike
kwenye shule ya sekondari ya Wasichana Tabora Tanzania kubaki nusu uchi
kwa nia ya kupigia kelele matatizo ya shule ikiwemo maji.
Nchi
jirani ya Kenya matukio kama haya yamekua mengi pia lakini hawa ndio
wamechukua headlines kwa kuwa Wanamuziki wa kwanza kuandamana kwa aina
hii.
Ripota
wa TZA Kenya Julius Kepkoich amesema Wasanii hawa waliandamana nje ya
ofisi za Nation Media Nairobi wakiwa nusu uchi kulalamikia nyimbo zao
kutochezwa na vyombo vya habari.
Wakiwa
na mabango yao Wasanii hawa kutoka maeneo ya Vitongojini walisema
wanaumizwa na kitendo cha nyimbo zao kutochezwa, wamekua wakitoa nyimbo
mpya kila wakati lakini hazichezwi kwenye Radio wala TV badala yake
zinazochezwa ni za wasanii walewale kila siku.