Jumapili, 12 Februari 2017

UTAFITI: Wanawake Weupe Wanaringa Kuliko Weusi


UTAFITI: Wanawake Weupe Wanaringa Kuliko Weusi

Kutokana na utafiti niliofanya mimi mwenyewe sasa ni dhahiri wanawake weupe wanaringa sana kuliko wale weusi...
Utafiti huu ulijumuisha kuwatokea moja kwa moja, asilimia kubwa kati yao hata ilipotokea kuwaita wengi walionesha dharau sana kuliko wale weusi. 
Sasa kama na wewe ulishawai kutokewa na hali hii unga tela ili nione kama utafiti wangu uko sahihi kias gani

Huwa Napata Shida sana Nikikutana na Wanawake Wenye Hii Tabia



Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Ghosh,ur still a kid,mi nadate guys who are 45 years above...Wanajua kupenda,they are so caring,yaani nyie vijana mnasumbua sana''.Sio tunasumbua,anajua kabisa miaka 29 bado ndo unasaka hela,ndo umeanza maisha huna cha kumhonga,ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi!

Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47..Uongo mtupu!Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45??Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga,amefanya kazi ana hela,unajifanya unampenda kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni,hamna hata aibu..Mnapenda sana vitu ready made,tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha hapo alipo,we unakuja unadandia tu,,,Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani,msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti hes caring uone inavyouma,utatamani umpige patasi ya kisogo...Gold diggers,waone kwanza,msione gesi mtwara mshaanza kuandamana!45years guy waiting for u student of 23 years,ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au??

Hivi ni Kwanini Wanawake Wengi Hujivunia Sana Makalio Yao?


Angalia hata picha wanazopiga wanawake utaona jinsi wanavyojibinua ili wanaonekane wana makalio makubwa.
Hata wakati wa kutembea pia wengine hutembea tofauti ili kuhakikisha kuwa makalio yake yanatikisika na ndio maana hata wengine hudiriki hata kutumia dawa za mchina ili kukuza makalio yao na hata baadhi yao wakati mwingine hujigamba kuwa eti wanamshukuru Mungu kwa kuwapa hips kubwa na wakati mwingine husikika wakisema eti mwanamke inye. 
Hivi nyie wanawake hususani wasichana ni kwanini mnapenda sana kujivunia na kuringia makalio yenu? Ina maana katika miili yenu kitu mnachokiona ni cha thamani ni makalio pekee? Badilikeni bwana maana kujivunia makalio badala ya akili ni ujinga wa kiwango cha lami

Mke Wangu Anunuliwa Nguo za Ndani na Mwanaume

Baada yakudakua mawasiliano ya mke wangu na kukuta Jamaa akimwambia zawadi yako ipo tayari hivyo watafutane ampatie..

Baada ya siku mbili tatu nakaona kimfuko kipo na chupi nne na brazia mbili, sikuuliza ila nikahisi hii ndio ile zawadi. Nikaamua kudakua mawasiliano yake tena.

Nikakutana tena na mawasiliano wakiulizana vip ameipenda zawadi na je zimemtosha.

Kiumweli ni zaidi ya wiki tatu sasa sijamuuliza au kuonyesha tofauti yoyote kwake, ila bado najiuliza ni sahihi kwa mwanamke tena mke wa mtu kupewa zawadi ya chupi au brazia na mwanaume tofauti na Mume/Mpenzi wake..!

Lakini pia je huyu mwanamke anaweza kuendelea kua na vigezo vya kuendelea kua mke.

Lamwisho ni mwanamke / Mwanaume anapokua anaamua kumnunulia mwenzake nguo za ndani anakua anamaanisha nini?

Natumai mawazo yenu yatanisaidia Asante.!

Ubuyu wa Moto Moto..Masogange Afunguka A to Z Juu ya Kupangiwa Mjengo na Makonda…


ISHU hot iliyotrendi wiki hii ni kuhusu kigogo mmoja kudaiwa kumpangishia Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ mjengo wa maana uliopo Makongo Juu jijini Dar ambapo Ijumaa limechimba ili kujua ukweli wa mambo.
Madai hayo yaliibuka juzikati baada ya watu kibao wakiwemo mastaa kuhoji kwa nini modo huyo hakutajwa kwenye listi ya mastaa wa unga wakati aliwahi kunaswa akisafirisha ‘mzigo’ nchini Afrika Kusini na sasa anaishi maisha bomba.
“Unajua kati ya mastaa wanaoishi kwenye nyumba za kifahari Masogange yumo, watu wanasema anauza madawa lakini ninachojua mimi ni kwamba kapangishiwa bonge la jumba kule Makongo juu, ukifika pale utadhani anaishi bosi f’lani.
“Kapangishiwa na kigogo mmoja na huyo ndiye anampa jeuri mjini, sasa jaribuni kufuatilia mtaujua ukweli ila mimi msinitaje, msije mkanitafutia matatizo,” alidai mtoa ubuyu huyo.
Kufuatia madai hayo, Ijumaa lilifanya jitihada za kufahamu ilipo nyumba hiyo ambapo, kwa kuwatumia watu wanaomjua vizuri lilifanikiwa kufika Makongo Juu na kushuhudia nyumba hiyo ya kihafari.
Katika ‘kunyapianyapia’ ili kujua kama staa huyo alikuwemo ndani, paparazi wetu aligonga geti muda mrefu lakini halikuweza kufunguliwa wala kuonekana mtu yeyote.
Ijumaa laamua kumpigia simu
Waandishi wetu wakiwa wamekaa nje ya nyumba hiyo huku wakiangaza huku na kule, waliamua kumpigia simu Masogange na bahati nzuri alipokea na alipoambiwa wako nje kwake, alijibu kuwa hakuwepo hapo nyumbani.
“Sipo, niko mbali kidogo,” alisema mdada huyo mwenye figa matata.
Alipotakiwa kufungukia madai kuwa, nyumba hiyo anayoishi amepangiwa na kigogo mmoja maarufu na ndiye anayempa ujanja wa kuishi mjini, Masogange alisema kuwa ni kweli amepangiwa nyumba hiyo lakini siyo na kigogo kama inavyodaiwa.
“Watu wanasema eti nimepangiwa nyumba na kigogo, ukweli naujua mwenyewe. Nina mpenzi wangu na ndiye aliyenipangishia nyumba hii na hili suala lipo wazi kabisa kwani watu wangu wa karibu wanamjua,” alisema Masogange.
Aidha, katika muendelezo wa madai ya Masogange kupangiwa mjengo na kigogo, juzikati ilivuja clipu iliyodaiwa ni ya staa Wema Sepetu akihoji sababu za Masogange kutotajwa kwenye listi ya mastaa wa unga.
Hata hivyo, juzi kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda  na waandishi wa habari, mmoja wa mapaparazi alimuuliza sababu za Masogange kutotajwa kwenye listi hiyo kama alivyodaiwa kuhoji Wema ambapo mheshimiwa huyo aliyedhamiria kupambana vilivyo na biashara ya madawa ya kulevya katika Jiji la Dar alijibu:
“Kwanza ni kosa kisheria mtu anapokuwa anashikiliwa na jeshi la polisi kushika simu, sasa kama una jambo unataka kulisema na uko polisi, kwa nini usiliseme badala yake u.”

Paul Makonda Afunguka Kuitwa na Bunge Kwa Ajili ya Kuhojiwa


Paul Makonda Afunguka Kuitwa na Bunge Kwa Ajili ya Kuhojiwa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kwa kuwa hajapokea barua ya kuitwa.
Akizungumza  jana jijini Dar es Salaam, Makonda alisema hatoweza kwenda mbele ya kamati hiyo bila barua rasmi iliyomtaka kufanya hivyo.
Bunge lililokuwa likiendelea na vikao vyake Dodoma kabla ya kuahirishwa juzi, lilipitisha uamuzi wa kuwataka Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alaxander Mnyeti, kufika mbele ya kamati hiyo na kuhojiwa kutokana na kauli walizozitoa, zinazodaiwa kuudharau mhimili huo wa dola.
Lakini Makonda alisema jana “hilo suala la mimi kuitwa kwenye kamati nalisikia na kulisoma kwenye magazeti."
"Sina uhakika ni lini wamefikia uamuzi huu wa kuniita na hata kama wamefikia uamuzi huo, sijaletewa barua rasmi.”
Baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo wa kuitaka Ofisi ya Bunge iwaandikie barua viongozi hao, juzi baadhi ya wabunge walihoji kauli ya Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, kwamba azimio la chombo hicho cha kutunga sheria kumtaka Makonda kufika mbele ya kamati kujieleza kuhusu tuhuma za kuudharau mhimili huo, halikufuata utaratibu.
Hatua hiyo iliamsha hasira kwa baadhi ya Wabunge na kuomba mwongozo kuhoji kwa nini Katibu wa Bunge ametoa kauli ambayo inakinzana na makubaliano ya Bunge.
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara na mwezake wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (wote Chadema) walihoji kuhusu kauli ya Dk. Kashililah.
Waitara alisema, “Asubuhi ya leo ( juzi) nimetumiwa ‘clip’ ya sauti ya Katibu wa Bunge akikosoa uamuzi wetu hapa na pia gazeti la Habari Leo, Ukurasa wa 25, kuna habari imeandikwa.
Katika taarifa hii, Katibu wa Bunge anasema maazimio ya Bunge yalikosewa na hayakufuata utaratibu,” alisema na kuongeza kuwa: “ Kwa maana nyingine, hatatekeleza kile tulichokubaliana.”
Mchungaji Msigwa wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alieleza kuwa hajafurahishwa na kauli ya Katibu wa Bunge.
Alisema Katibu wa Bunge amekosea kwenda katika vyombo vya habari na kudai chombo hicho cha kutunga sheria kimekosea kwa kuwa anafanya kazi ya Bunge na kwamba hajaajiri wabunge na anapaswa kufuata maagizo yao.
Hoja ya kutaka kina Makonda washughulikiwe iliwasilishwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) katikati ya wiki na ilijadiliwa na kuungwa mkono na wabunge wote, wakiwamo mawaziri kwa kusema ‘ndiyo’.

Majaliwa Afunguka Issue ya Madawa ya Kulevya Inayoratibiwa na Makonda..


JUMLA ya Watanzania 578 wamekamatwa na kufungwa katika magereza ya nchi mbalimbali kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Akiahirisha mkutano wa sita wa Bunge la 11 mjini Dodoma juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitaja nchi ambazo Watanzania hao wamefungwa kuwa ni pamoja na China (200), Brazil (12), Iran (63), Ethiopia (7) na Afrika ya Kusini (296).
Majaliwa pia alisema vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya inapaswa kuungwa mkono.
Alisema madawa ya kulevya huingia zaidi kutumia kwa njia za bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na mipakani kwa njia ya magari binafsi na mabasi yatokayo Kenya, Uganda na Zambia.
“Lengo la serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri - wauzaji na wasambazaji," alisema Majaliwa.

40 ya Nillan: Wolper Achafua Hali ya Hewa, Atoa Povu Hadharani Mbele ya Wageni

WAKATI sherehe ya kutimiza 40 kwa mtoto wa Diamond na Zari, Nillan ikiendelea, staa wa Bongo Movies, Jackline Wolper Massawe amekerwa na wanaomsema vibaya Zari na kuamhua kuwafungukia hadharani akitoa povu lake mbele ya wageni waalikwa.

Baada ya Kutoka Selo Kwa Dhamana Hii Ndio Post ya Kwanza Aliyoandika Wema Sepetu Instagram


Inawezekana kama wewe ni shabiki wa Wema Sepetu ulikua na hamu sana ya kujua post yake ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii itahusu nini baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama kufuatia sakata la dawa za kulevya lililomfanya alale Polisi.

Post ya kwanza ya Mwigizaji huyu haijahusu chochote kuhusu kesi yake ama alichokipitia wiki iliyoisha bali imemuhusu dada yake ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa kama inavyoonekana hapa chini.



Wema Sepetu atarudi tena Mahakamani mwishoni mwa mwezi huu baada ya kupata dhamana Alhamisi ya wiki iliyopita kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam.

Tundu Lissu Abaini Mbinu Chafu kwa Chama Fulani Kuweka Mgombea Urais TLS..!!!


Mwanasheria Mkuu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama hicho, Tundu Lissu amezungumzia hatua yake ya kujitosa kuwania urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Mosi, Lissu amesema amepata msukumo kutokana na kauli ya rais John Magufuli kuwa kuna kampeni zimeanza za kumuondoa rais wa sasa wa TLS na zinaendeshwa na chama fulani ambacho kimeweka mgombea wake.
Pili, akasema Lissu ni kauli kuwa mawakili wanaotetea wauza dawa za kulevya nao wakamatwe wawekwe ndani.
“Sikuwa na mpango wa kugombea lakini the moment (wakati) aliposema, nikasema sasa nitagombea urais wa TLS,” amesema mbunge huyo.
Rais alitoa matamko hayo katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Sheria iliyofanyika mapema mwezi huu kwenye uwanja wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Lissu amesema TLS imepoteza mwelekeo na nafasi yake katika jamii kwenye masuala ya kisheria, hasa kushindwa kukemea vitendo vya uvunjifu na ukiukaji wa Katiba na sheria unaofanywa na viongozi.
“Chama cha wanasheria kinatakiwa kiwe cha kwanza kupiga kelele sheria za hovyo zinapotungwa, kinatakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukiukaji wa Katiba na sheria vinavyofanywa na watu wenye mamlaka lakini Law society ya kwetu imekaa kimya,” amesema.
Kuhusu msimamo wake wa kisiasa na chama hicho endapo atapata nafasi hiyo, Lissu amesema masuala ya kisheria hayana uhusiano na vyama vya kisiasa na kwamba chama hicho kipo kwa ajili ya kulinda na kusimamia utawala wa sheria.
Pia, amesema kama chama chake kitakuwa na msimamo sawa na misingi ya chama hicho katika kutetea utawala wa kisheria, si tatizo na kwamba, ikiwa kitakuwa na msimamo tofauti katika mambo ya msingi, hakina budi kukosolewa.
“Sigombei ili kuipeleka Chadema ndani ya TLS. Masuala haya yanatuhusu sisi wote kujua mambo yanapoharibika, kuona sheria zinapokiukwa na kuona sheria mbovu zinapotungwa,” alisema.
Ofisa Maboresho ya Sheria wa TLS, Mackphason Buberwa amesema mchakato wa kupata wagombea umeshakamilika na waliopitishwa na kamati ni watano.
“Taratibu zimekamilika, kilichobaki ni wagombea kuandaa kampeni zao kabla ya Machi 18 siku ambayo uchaguzi utafanyika mjini Arusha,” amesema Buberwa.
Wagombea wengine ni Francis Stola, Lawrance Masha, Victoria Mandali na Godwin Mwapongo. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Machi 18 jijini Arusha ambako zaidi ya mawakili 6,000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Jaji Chande Apewa Kazi Umoja wa Mataifa..!!

Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande ameteuliwa kuongoza jopo la wataalamu watakaochunguza mazingira yaliyosababisha ajali ya ndege iliyomuua aliyekuwa katibu mkuu wa umoja huo, Dag Hammarskjold.
Uteuzi huo wa jaji mkuu mstaafu umefanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres.
Hammarskjold alipoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea Zambia mwaka 1961 wakati akitokea Congo ambayo ndiyo kwanza ilikuwa imepata uhuru.
Hammarskjold alikuwa nchini humo kwa ajili ya ujumbe wa amani.
Naibu msemaji wa UN, Farhan Haq amesema Chande ataongoza jopo hilo ambalo litakuwa na kazi kupitia taarifa zilizoandaliwa na wachunguzi waliopewa jukumu na katibu mkuu mstaafu, Ban Ki-moon.
Uchunguzi huo unafuatia azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa na Baraza Kuu ambalo lilipendekezwa kufanyika uchunguzi wa kina kubaini mazingira ya ajali hiyo.
Awali, kulikuwa na ripoti kuwa Uingereza na Marekani zilikuwa zimegoma kutoa baadhi ya taarifa muhimu kuhusu tukio hilo, huku Afrika Kusini ikilalamikiwa kwa kushindwa kutoa majibu kwa baadhi ya hoja.
Ripoti iliyotolewa na wataalamu huru waliochunguza ajali hiyo inaeleza kuwa Hammarskjold aliuawa baada ya kunusurika kwenye ajali hiyo. Kumekuwa na taarifa kuwa ndege hiyo ilishambuliwa.
Jopo hilo linaloongozwa na Chande linatarajia  kuanza kazi mara moja na kwamba litakuwa na jukumu la kupitia nyaraka zote, ikiwamo ripoti ya kurasa 99 iliyoandaliwa na wataalamu wa awali waliochunguza mazingira ya ajali hiyo.

Vita Dhidi ya Madawa ya Kulevya..Wanawake Wawili Wadakwa na Kilo 114 za Bangi..!!


Wanawake wawili ni miongoni mwa watu zaidi ya 15 waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya mkoani Mwanza
Watu hao wamekamatwa wakijihusisha nadawa hizo ndani ya wiki moja kuanzia Febuari 6.
Habari zinasema wanawake hao wamekamatwa wilayani Magu wakiwa na kilo 114.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema watuhumiwa 11 wamekamatwa wilayani Nyamagana na Ilemela na kilo 57 za dawa za kulevya aina ya miraa na kete mbili zinazodaiwa kuwa ni heroin.
“Mtuhumiwa mwingine ambaye ni mfanyabiashara wa vipuri vya magari, alikamatwa eneo la Butimba akiwa na kete 240 ya dawa za kulevya zinazodaiwa kuwa ni  heroin na ndunga mbili,” amesema.
Msangi amesema mtuhumiwa huyo alitaka kuzitumbukiza  chooni dawa hizo ili kupoteza ushahidi, lakini polisi waliwahi kukata bomba.