Diego Costa akianguka katikakati ya wachezaji wa stoke city
Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose
Mourinho amesema kuwa ilikuwa hatari kumchezesha mshambuliaji Diego
Costa baada ya kujeruhiwa wakati wa ushindi wa Chelsea wa 2-1 dhidi ya
kilabu ya Stoke City siku ya jumamosi.
Costa alichukua mahala pake
Oscar wakati wa mapumziko huku mabao yakiwa 1-1, lakini alicheza kwa
dakika 10 pekee kabla ya kulazimika kutoka nje baada ya kupata jeraha
jengine.
''Kama matokeo yangalikuwa 2-0 asingecheza.Lakini ilibidi
tumchezesha .Kitengo changu cha matibabu kiliamua kumchezesha'',
alisema Mourinho.
Amsema kuwa mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa wiki mbili .
Hii
inamaanisha kwamba Costa ataikosa mechi dhidi ya QPR tarehe 12 mwezi
Aprili na ile dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Stamford
Bridge tarehe 18 mwezi Aprili.