Alhamisi, 20 Novemba 2014

Louis van Gaal kayatoa ya moyoni…. anataka nani ashinde Ballon d’Or 2014? Ronaldo na Messi ?

Screen Shot 2014-11-20 at 3.53.45 AM 
Wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2014 walishatangazwa ambapo list hiyo pia inawahusisha mastaa wa soka kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, huku list hiyo ikiwa pia na wachezaji wa Ujerumani iliyoshinda kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Baada ya ushindi wa Ronaldo na Messi kuchukua headlines sana kocha wa Manchester United Louis van Gaal (63) ameamua kuyatoa ya moyoni na kusema mwaka huu Ronaldo na Messi hawatakiwi kuchukua hiyo tuzo bali ni halali ikachukuliwa na mchezaji wa Ujerumani.
Wajerumani wanaowania tuzo hiyo ni Mario Gotze, Toni Kroos, Philipp Lahm, Thomas Muller, Manuel Neuer na Bastian Schweinsteiger.
Screen Shot 2014-11-20 at 4.04.25 AM 
Anasema ‘Naamini Ujerumani inafaa kuchukua hii tuzo, mara nyingi imekua tu ni wachezaji maarufu/wanaofahamika ndio wanashinda hii tuzo, kitu kikubwa kushinda ni kombe la dunia ndio maana naamini itachukuliwa na mchezaji wa Ujerumani sababu kiukweli wanastahili
Screen Shot 2014-11-20 at 3.50.45 AM 
Umeonaje mawazo ya Van Gaal? ungependa nani ashinde Ballon d’Or ya 2014 mtu wangu? naomba niachie maoni yako kwenye comment hapa chini.

Baada ya kuandikwa amemuomba Diamond collabo, Jose Chameleone ametoa haya majibu

Screen Shot 2014-11-20 at 4.14.24 AM 
Ni stori nyingi tunakutana nazo kwenye vyombo vya habari kila tunapoamka na mara nyingi tunaamka nazo kwenye mitandao ya kijamii moja wapo ikiwa hii ya mwimbaji wa Uganda Jose Chameleone kudaiwa kumuomba Diamond wafanye collabo.
Kwenye interview na Mambo Mseto ya Radio Citizen November 19 2014 Chameleone amekanusha hizo taarifa kwa kusema ‘kitu ambacho nitakwambia kabla ya kusema chochote, mimi naheshimu wasanii wote mashariki na duniani na nataka niwakumbushe kitu kingine, nimekaa kwenye muziki kwa miaka kumi na nne… mimi sio msanii mchanga’
Diamond 2 
‘Ilikua ni uongo sijui umetokea wapi eti mimi nimemuomba collabo, Yes…. tunaweza kufanya collabo lakini mimi sijamuomba collabo, wamesema mimi nimezungumza na Diamond kwenye whatsapp… yes tumezungumza lakini ilikua ni kirafiki wala hatujaongea maneno ya kimuziki’ – Jose
‘Mimi ni msanii mkubwa, sio msanii mchanga… naheshimu kila msanii kuanzia mchanga mpaka mkubwa na vilevile mimi pia ni msanii mkubwa na siwezi kuomba collabo kama hivyo, nimeshangazwa sana’

Kauli ya Raisi wa Simba kuhusu usajili wa Mnigeria Emeh Izechukwu

IMG_8912.JPG
Siku chache baada ya dirisha la usajili kufunguliwa kumekuwepo na tetesi za usajili kumhusu mshambuliaji wa kinigeria Emeh Izuchukwu kurudi Msimbazi.
Lakini Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema kwamba hawana nafasi ya kusajili ya mshambuliaji wa kigeni na kwamba Emmanuel Okwi, Amisi Tambwe na Paul Kiongera wanawatosha.
Kauli hiyo ya Aveva inakuja wakati tayari vyombo vya habari vimekuwa vikiwahusisha washambuliaji Mnigeria, Emeh Izuchukwu na Mganda Danny
Sserunkuma kusajiliwa na Simba.
Aveva amesema kwamba Izuchukwu ambaye ni mchezaji wao wa zamani, ameomba mwenyewe kurejea kuchezea klabu hiyo, lakini anasikitika hawana nafasi ya mchezaji
wa kigeni.
“Hao wachezaji wengine hao, ni magazeti tu yamekuwa yakiandika, lakini ukweli ni kwamba hatujazungumza nao,”amesema Aveva

Kwa wale watumiaji wa mboga za majani Dar, hii imetokea jana kwenye habari

dothao-12190000
Huenda wewe ni mmoja kati ya walaji wa mbogamboga za majani lakini hujui mboga hizi zinalimwa katika mazingira gani… sasa baraza la mazingira Tanzania NEMC limebaini kuwa wakulima wa mboga za majani Dar wamekuwa wakitumia majitaka kumwagilia hizi mboga.
Afisa wa NEMC amezungumza na ITV na kusema; “… Kama Serikali hatuwezi kuruhusu kitu kama hicho.. hatutaruhusu tena kumwagilia kinyesi kwenye mchicha, haturuhusu hicho kitu, hakuna serikali hiyo ambayo itaruhusu vitu hivi…
Kama unataka kuisikiliza taarifa hiyo bonyeza play hapa.