Ijumaa, 17 Machi 2017
Home »
» Ndoto za Mbwana Samatta Kucheza na Mau United Zawekwa Pending
Ndoto za Mbwana Samatta Kucheza na Mau United Zawekwa Pending
Ndoto za mshambuliaji wa timu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mtanzania Mbwana Samatta za kukanyaga katika dimba la Old Trafford la Manchester United zimesubirishwa baada ya matokeo ya droo ya robo fainali kombe la Europa kwenda kinyume na matamanio yake.
Hamu ya Nahodha huyo wa Taifa Stars ilikuwa ni kuona timu yake ya Genk inapangwa kukutana na Man United katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, ili atimize ndoto yake mojawapo ya kucheza katika uwanja wa huo maarufu na uliotoa mastaa wengi duniani.
Samatta baada ya mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ambao timu yake iliibuka na ushindi wa 5-2 na kutoa nafasi kubwa ya kufuzu robo fainali, alinukuliwa akisema "Moja kati ya ndoto zangu ni kukanyaga katika dimba la Old Trafford, kwahiyo naomba kila siku timu yetu ikivuka, ipangwe na Manchester United"
Hata hivyo, katika droo iliyochezeshwa leo, KRC Genk imepangwa kuanzia nchini Hispania dhidi ya Celta Vigo, na mchezo wa marudiano utapigwa nchini Ubelgiji.
Ili timu hiyo ikutane na Man United msimu huu, inapaswa kwanza kuitoa Celta Vigo, huku ikiomba Man UNited pia ifuzu nusu fainali, halafu droo iwakutanishe.
Kutokana na ukweli kwamba timu ya Man United ndiyo yenye mashabiki wengi zaidi duniani, ingeweza kuwa ni fursa adhimu kwa Samatta kujitangaza zaidi, kwa kuwa watu wengi hawapitwi kutazama mchezo wowote unaoihusu timu hiyo iliyo chii ya kocha Jose Mourinho.
Related Posts:
Nuh Mziwanda Afunguka Kuhusu Kurudiana na ShiloleMsanii Nuh Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Alikiba amefunguka na kusema kuwa hata kama ikitokea mpenzi wake huyo wa zamani akitaka kurudiana na yeye ni kitu kisichowezekana kwa sa… Read More
PICHA: Jionee kaburi atakalozikwa Papa WembaPicha hii inasemekana ndilo kaburi atakapozikwa mwanamziki Maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo maarufu kwa jina la Papa Wemba. Huu ni zaidi ya ufahari, lakini mimi naona hauna maana.. … Read More
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida Asimamishwa Kazi Baada ya Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu Watumishi HEWAMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida, Simion Mumbee amesimamishwa kazi baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu watumishi hewa. Katika taarifa hiyo, Mumbee anadai watumishi hewa 19 waliogundulika kwenye halmash… Read More
Mheshimiwa Rais Wanaodhani Wako Juu ya Sheria ni Wengi Sana...Soma Kisa HichiMIAKA michache iliyopita, wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ambayo imeshapita, kuna jambo moja lilinishangaza sana. Jambo hili lilimhusu Waziri wa Serikali hiyo na mlinzi wa benki. Kilichotokea ni kwamba Mheshimiwa Waziri al… Read More
CHADEMA na Katibu Mkuu mfu..Ukimya Wake ni Hatari kwa Mustakabari wa ChamaKiukweli huyu katibu mkuu hajui hata pa kuanzia Chama kinaonesha dalili za kuifuata TLP na UDP sioni harakati zake ki ukweli CHADEMA ilikosea sana Dr. Mashinji ni unpopular figure hata akitembea kwa miguu Karikoo hakuna wa ku… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni