Jumanne, 3 Mei 2016

WASOMI WAKOSOA ASILIMIA 2% YA KODI ALIYOPUNGUZA RAIS MAGUFULI

Siku moja baada ya Rais Magufuli kushusha Kodi ya Mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn – PAYE ) kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9. Wataalamu wa uchumi nchini wamelipokea katika mtazamo tofauti
Mtaalamu wa Uchumi ambaye ni Msimamizi Fedha wa Kampuni ya Clouds Media Issa Masoud katika mahojiano yake na
mtembezi.com ameanza kwa kusema
“Sipingani na wengi waliosema kwamba punguzo la kodi ya mshahara kutoka 11% mpaka 9% (2%) ni kidogo sana ukilinganisha na gharama za maisha. Kwa misingi ya kwamba bado Watanzania wengi wanaofanyakazi wanawajibika kugharamia haya..
1. Afya
2. Makazi (kupanga na gharama za vifaa vya ujenzi)
3. Usafiri
4. Elimu- ingawa elimu inatolewa bure lakini bado ubora wake upo chini ukilinganisha na shule binafsi matokeo yake watu wengi watoto wao wanasoma shule binafsi tofauti na zamani.
4. Habari -mifumo yote ya kupata habari sasa hivi ni ya kulipia.
5. Huduma nyingine za jamii n.k
Kwa hiyo serikali ingejikita sana kwenye kurahisisha hayo mambo hapo juu ili kumsaidia huyu mwananchi wa chini.
Ingawa kwa upande mwengine, bado nchi nyingi duniani zinategemea kodi ya mishahara kama moja ya chanzo cha kueleweka cha mapato ya serikali, hata zile zenye mishahara mikubwa kama Ufaransa, Australia, Austria, German nk. wao kodi zao za mishahara zinafika mpaka 49.8%, kwa maana ya kwamba nusu nzima ya mshahara wako unarudi kama kodi.
Kwa hiyo kwa Tanzania punguzo la 2% kwenye idadi ya wafanyakazi zaidi ya milioni 15,000,000 kwa mujibu wa sensa ya 2012 (Serikalini na Binafsi) kwa kiasi cha Tsh. 3,800 ni jumla ya Tsh. 57 bilioni kwa mwezi serikali imejipunguzia kutoka kwenye mapato yake kwa mwezi, kwa hiyo kwa mwaka ni sawa na punguzo la pato la serikali kwa takribani zaidi ya shilingi bilioni 600 za Kitanzania.
Mapendekezo yangu ni kwamba serikali iangalie zaidi kwenye gharama za maisha sababu punguzo hilo ni kubwa sana serikalini ila ni dogo sana kwa mtu binafsi. Wananchi wasaidiwe kupunguza gharama ya vitu tajwa hapo juu. Ikiwemo ujenzi wa nyumba bora na nafuu kwa kuwapangisha au kuwauzia wafanyakazi.
Na serikali izidi kubuni vyanzo vingine vya mapato tofauti na kodi ya mshahara na kuhakikisha vilivyopo vinalipa kodi ipasavyo”
Kwa upande wake Mtaalamu na Mshauri wa Uchumi Malembo Lucas Elias kutoka Taasisi ya Umoja wa Maendeleo ya Afrika (ADA) licha ya kuunga mkono lakini amebainisha kuwa serikali inapashwa kuzingatia zaidi kasi ya maisha kwa kulinganisha kasi ya uzalishaji ili punguzo hilo liweze kuwa na tija kwa watumishi katika suala la chakula, malazi na mavazi.

PROF MUHONGO: TATIZO LA UMEME KUISHA MWAKA HUU MWEZI SEPTEMBA

SERIKALI inatarajia kuzindua mradi mkubwa wa kuboresha miundombinu ya kusafirisha umeme Septemba mwaka huu, utakaomaliza tatizo la umeme kukatika.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kwa sasa miundombinu ya kusafirishia umeme ni midogo na katika kuboresha hilo, kuna mradi mkubwa utazinduliwa Septemba mwaka huu wa kusafirisha umeme.
Alisema mradi huo ni wa kusafirisha umeme kutoka kilovoti 220 hadi 400 kutoka Dar es Salaam-Tanga hadi Arusha na Iringa-Dodoma-Shinyanga, hivyo tatizo la kukatika umeme litatatuliwa.
Waziri huyo alitoa maelezo hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM) aliyetaka kufahamu lini umeme utakoma kukatika wilayani Korogwe.
Akielezea hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alisema Serikali inafanya marekebisho ya transfoma na chanzo cha umeme cha Hale mkoani Tanga ili kumaliza tatizo la kukatika umeme mara kwa mara wilayani Korogwe na mkoani Tanga kiujumla.

ITALIA WAJA NA UTAALAMU WA KUPANDIKIZA KICHWA KWA MTU

Mtaalam wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero kutoka nchini Italia, anakusudia kufanya jaribio la kwanza la kupandikiza kichwa cha binadamu kwenye mwili wa binadamu mwingine, ifikapo mwakani.
Wataalam wengi wa upasuaji wanafikiria wazo hilo ni la kiuwendawazimu, lakini sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema bado anapanga kujaribu pandikizo la kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head Transplant)
Dk. Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya zoezi hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam wa software Valery Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake ya mwili.
Dk. Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango wake wa kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (donor) bado upo, na ataanza mpango huo mwishoni mwa mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya kutibu waliopooza mwili.
“Ningesema tuna takwimu nyingi zinaendelea, ni muhimu kwa watu kuacha kufikiria jambo hili sio rahisi, hii inawezekana kabisa na tunaendelea kulifanyia kazi”, alisikika Dk, Canavero akimwambia mwanasayansi mchanga.
Timu iliyo nyuma ya kazi hiyo ilipost video ikimuonesha nyani ambaye alifanyiwa upandikizwaji huo, na kufanikiwa kutembea baada ya uti wa mgongo kutenganishwa na kuunganishwa tena’
Chanzo:mtembezi

VYAKULA VINAVYO ONGEZA HISIA KATIKA MAPENZI

Kama kawaida mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi.
Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa Capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya Endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mgusu wa hisia za raha.
MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.
Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi, kwani matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (Cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.
Pia wanandoa wanapozidi kunenepa ndipo na hali ya kufurahia au kutaka au hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua.
NAFAKA
Nafaka zina nyuzinyuzi (Fibre) na sukari ngumu (Complex Sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili, hivyo nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu.
Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.
TANGAWIZI
Tangawizi ni kiungo ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume, Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa na kuwa kama unga.
ASALI
Asali ina madini yanayoitwa Boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya Estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa.
KARANGA
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya (Vascular System).
Pia mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri, karanga zina madini muhimu kama vile Magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.
CHOCOLATE
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni.

Siri Kuu Kuhusu Escrow zafichuka

SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka.
Nyaraka mikononi mwa gazeti hili zinaonesha zaidi ya asilimia 90 ya wale waliopewa fedha na Rugemalira, ni wale waliomsaidia “kufanikisha ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 324 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) na kujinasua katika mikono ya sheria.”
“Rugemalira alishika kila mmoja. Kuanzia Ikulu ya Jakaya Kikwete, TAKUKURU, mahakama, BoT, hazina, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, viongozi wa madhehebu ya kidini na hata baadhi ya mawaziri wa zamani wenye ushawishi serikalini,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi kutoka Ikulu.
Amesema, “…fedha katika akaunti ya Escrow zilihusisha mtandao mpana ulioratibiwa na Rugemalira na Harbinder Sigh Seth (Singasinga).”
Majaji wa mahakama kuu, Aloycious Mujulizi na Eudeus Ruhangisa, ni miongoni mwa waliokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rugemalira; na walikuwa washauri wake wakuu wa kisheria.
Mawasiliano kati ya Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa yalifanyika kupitia kwa Rugemalira mwenywe na katika eneo jingine kupitia kwa mkewe, Benedicta.
Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa walitajwa bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwa miongoni mwa vigogo waliopewa mgawo wa fedha hizo na Rugemalira.
Bunge liliagiza majaji hao wachunguzwe na wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.
Hadi sasa, hakuna taarifa zozote kuwa majaji walichunguzwa na kuchukuliwa hatua.
Rugemalira alikuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni ya kigeni ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing Limited.
Jaji Mujulizi na Ruhangisa walilipwa na Rugemalira kila mmoja Sh. 404 milioni.
Mabilioni ya shilingi yaliyohifadhiwa katika akaunti ya Escrow yalikwapuliwa na Harbinder Sigh Seth, aliyejiita mmiliki wa IPTL kwa msaada mkubwa wa Rugemalira na kile kilichoitwa, “amri ya mahakama.”
Seth alidai kumiliki IPTL kupitia kampuni yake ya Pan African Power Tanzania Limited (PAP).
MwanaHALISI linaweza kuthibitisha kuwa kati ya tarehe 13 na 26 Novemba 2014, kilikuwa kipindi ambacho Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ilimhoji Rugemalira juu ya ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow.
Aidha, ni katika kipindi hichohicho, Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Jaji Mujulizi na Ruhangisa.
Wengine waliokuwa na mawasiliano na Rugemalira katika kipindi hicho, ni waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo; aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Bernard Membe na aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi.
Aliyepata kuwa waziri wa utawala bora, Mathias Chakawe; aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah; aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG), Frederick Werema na aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara, Dk. Abdallah Kigoda, walikuwa pia na mawasiliano na Rugelalira.
Wengine ni naibu gavana wa BoT, Dk. Enos Bukuku; aliyekuwa Mnikulu Mkuu wa Ikulu, Shaban Gurumo; aliyekuwa Kamishna mkuu mamlaka ya mapato (TRA), Rished Bade na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati wa ujio wa IPTL nchini (1994), Andrew Chenge.
Orodha ya waliokuwa katika mawasiliano na Rugemalira inahusisha pia mawaziri wa zamani, Paul Kimiti na Wilson Masilingi; aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali – Daily News na Habari Leo – Gabriel Nderumaki; aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini, Wiliam Ngeleja na mkurugenzi wa kampuni ya G and S Consultancy Limited, Dk. Gideon Shoo.
Wengine ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Constantine Massawe; Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilain; Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa na aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
Prof. Tibaijuka alikiri kupokea kiasi cha Sh. 1.6 bilioni kutoka kwa Rugemalira. Hata hivyo, alisema kuwa fedha ambazo alipokea zilikuwa ni mchango wa shule yake ya Barbro Johanssen ya jijini Dar es Salaam na Kajumulo Girls High School iliyoko Bukoba.
Kwa mujibu wa taarifa, Dk. Hoseah alimruhusu Rugemalira kutafuta msaada popote pale, ikiwa ni pamoja na nje ya nchi na kwamba ofisi yake “ingetoa maofisa kumsaidia.”
“Kama una jambo la msingi kufanya nje ya nchi, una baraka zangu zote. Watakapohitajika maofisa wa TAKUKURU kwa ufafanuzi, wako tayari kukusaidia pale uliko,” anaeleza Dk. Hoseah na Rugemalira andishi lake la 16 Novemba 2014.
Dk. Hoseah anamaliza kwa kumueleza Rugemalira, “…nakutakia kila la kheri.”
Rugemalira alikuwa anaomba TAKUKURU kuingilia kati kile kinachoitwa, “mgogoro wa hisa kati ya IPTL na Benki ya Standard Chartered (SCB) ya Uingereza.”
Hata hivyo, Rugemalira anaonywa na Masilingi, ambaye wakati huo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, kuwa mwangalifu na mtulivu wakati suala hilo linaendelea.
Alisema, “mimi nikiwa mwanasheria, ninakushauri wewe na kampuni yako kushirikiana kwa ukamilifu na TAKUKURU. Suala la IPTL ni gumu. Limekuwa na mchanganyiko mkubwa. Akili nyingine haziwezi kulielewa.”
Masilingi anasema, “…nimebaini kwamba TAKUKURU ndio wanaolichukulia suala hilo kwa usiri mkubwa katika hatua za uchunguzi na wenyewe wanaweza kukusaidia kupata hukumu iliyo ya haki.”
Benki ya Standard Chartered ilikuwa inadai na mpaka sasa bado inadai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow, ni mali yake.
Inadai kuwa kampuni ya MECHMAR ya Malasia ilishindwa kurejesha mkopo iliochukua benki na kwamba hilo ni jambo linalosababisha mitambo ya IPTL iliyopo Tegeta Salasala, jijini Dar es Salaam, kuwa mali yake.
Akihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, wiki tatu baada ya Bunge kuagiza waliohusika katika wizi wa fedha za Escrow wachukuliwe hatua, aliyekuwa Rais wa Jamhuri, Jakaya Mrisho Kikwete alikiri kuwapo udanganyifu katika kufikia utoaji wa fedha hizo.
Alikiri baadhi ya nyaraka kughushiwa. Akakiri kuwa kampuni ya PAP imekwepa kodi ya serikali na kudai kuwa serikali yake bado inaendelea kuitafuta kampuni ya MECHMAR iliyodaiwa kuuza asimia 70 ya hisa zake ndani ya IPTL.
Rais alikiri kuwa aliyepewa fedha na serikali – PAP – hakuwa na sifa; serikali yake haikufanya uchunguzi yakinifu kuhusu historia, uhalali, sifa na uwezo wa kampuni ya PAP katika uwekezaji wa umeme, ununuzi wa mitambo na mtaji.
Naye mwanasheria wa Rugemalira, Camilo Schutte, katika barua aliyomwandikia Rugemalira, anasema “…baada ya kusoma ushauri wa Masilingi juu ya msaada wa TAKUKURU, itakuwa busara kuomba TAKUKURU kusubiri hukumu kati ya Standard Chartered na IPTL.”
Anasema kampuni ya Rugemalira (VIP) “…inapaswa kuomba TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya sera ya benki ya Standard Chartered kuhusu ununuzi wa madeni ambayo mchakato wake unaweza kuwa na rushwa.”
Camilo Schutte anamueleza Rugemalira katika barua yake hiyo na ambayo imenakiriwa kwa majaji, mawaziri, kiongozi wa TAKUKURU, maofisa wa Ikulu na watu wengine kuwa, “…tatizo la benki ya Standard Chartered, kama zilivyo taasisi nyingine, ni kufanya biashara ili kujipatia faida kubwa.”
Akiandika kwa Dk. Gideon Shoo, mwanasheria wa Rugemalira (Camilo Schutte) anaelekeza kufanyika mambo matatu kwa haraka.
Kwanza kutafuta, kwa “gharama yoyote ile,” watu wote wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ambao wanapigia kelele ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Miongoni mwa waliotajwa, ni Zitto Kabwe, mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini; David Kafulila, ambaye alikuwa mbunge wa Kigoma Kusini; Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose; Wilson Masilingi na balozi wa Finland nchini.
Pili, Camilo Schutte anasema, ni sharti mtandao wao ujiridhishe ikiwa watu wanaolizungumzia jambo hilo wanalifahamu kwa undani au wanalijua nusunusu au hawalijui kabisa.
Kwa maoni ya mwanasheria wa Rugemalira, wabunge waliokuwa wameshupalia jambo hilo walikuwa hawana taarifa zozote muhimu kuhusu suala hilo.
Tatu, mwanasheria alimtaka Dk. Shoo kuangalia athari za taarifa zilizosambazwa juu ya ukwapuaji wa fedha hizo, kwa kampuni ya IPTL na Rugemalira binafsi.
“Baada ya kukamilisha haya, naomba unijulishe haraka ili tuweze kupanga mikakati ya kukabiliana na kila tatizo nililolitaja hapo juu,” anaeleza Camilo Schutte.
Kupatikana kwa mawasiliano haya kumekuja mwaka mmoja na nusu baada ya mabilioni ya shilingi kukwapuliwa BoT; na Bunge kuelekeza serikali kufanya uchunguzi.
Aidha, kupatikana kwa taarifa kuwa Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya karibu na “kindungu” na mkuu wa TAKUKURU, kumekuja wakati ambapo taasisi hiyo imeshindwa kuanika orodha ya watu walionufaika na mgawo wa fedha hizo kutoka benki ya Stanbic.
Bunge liliagiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wote wa Escrow, ikiwa ni pamoja na kufilisi mtambo wa IPTL na kuitangaza benki ya Stanbic kuwa taasisi ya kutakatisha fedha.
Bunge liliagiza pia kuchunguza na kuwajibisha majaji waliotajwa kunufaika na mgawo wa fedha kupitia benki ya Mkombozi na kumfukuza nchini, anayejiita mmiliki wa IPTL, Harbinder Sigh Seth.
Akizungumzia kutajwa kwa Dk. Hoseah na baadhi ya majaji katika mawasiliano na Rugemalira, mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema jambo hilo linaongeza shaka juu ya uadilifu wa viongozi wa CCM na serikali yake.
Ameliambia gazeti hili katika mahojiano kwa njia ya simu, “…hili liserikali lote limeoza. Kuanzia Ikulu, mfumo wa mahakama hadi viongozi wa madhehebu ya kidini; kote kumejaa rushwa.”
Lissua ameongeza, “Tulisema ndani ya Bunge, kwamba majaji wamehongwa na hivyo tukataka wachunguzwe, lakini serikali ya CCM imegoma kwa kuwa walioiba waliwajua na walishirikiana nao.”
Mwanasiasa huyo wa upinzani anasema, “utapeli huu ulifanywa na serikali ya Rais Kikwete, BoT, Benki ya Stanbic na PAP.”
Amesema, “…sasa kama kweli wanataka kusafisha nchi, basi waanzie hapo. Siyo kukimbizana na vidagaa. Waanze na maofisa wao wa Ikulu waliokuwa wameigeuza ofisi ya umma kuwa ofisi binafsi.”
Chanzo: Mwanahalisi

Punguzo Kodi ya Mishahara Kwa Wafanya Kazi Laibua Mapya

Uamuzi wa Rais John Magufuli kupunguza asilimia mbili ya Kodi ya Mshahara (PAYE) umeibua mjadala baada ya kubainika kuwa utampa nafuu ndogo mfanyakazi, huku wachambuzi wakihamia kwenye kodi nyingine ya mapato kwa kuzingatia viwango vya mishahara.
Baadhi ya wadau wanapendekeza kodi hiyo, inayoitwa excess charge, ipunguzwe kumpa unafuu mfanyakazi, huku wengine wakishauri kuweka nguvu kwenye uchumi wa viwanda na kilimo na baadhi wakishauri juhudi zifanyike kudhibiti mfumuko wa bei ili mshahara utosheleze mahitaji ya mfanyakazi.
Baadhi ya wadau wanapendekeza kodi hiyo, inayoitwa excess charge, ipunguzwe kumpa unafuu mfanyakazi, huku wengine wakishauri kuweka nguvu kwenye uchumi wa viwanda na kilimo na baadhi wakishauri juhudi zifanyike kudhibiti mfumuko wa bei, ili mshahara utosheleze mahitaji ya mfanyakazi.
Juzi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Rais alitangaza kupunguza kodi ya PAYE kutoka asilimia 11 hadi tisa, lakini kwa mujibu wa wahasibu uamuzi huo ni punguzo la Sh1,100 kwa wafanyakazi wa mshahara wa kima cha chini na Sh3,800 kwa mshahara unaoanzia Sh360,000 na kwenda juu.
Akifafanua kuhusu PAYE, mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Richard Kayombo alisema kiwango cha mapato kisichozidi Sh170,000 hakina kodi, lakini mapato ya kati ya Sh170,000 hadi 360,000 yalikuwa yanakatwa asilimia 11 na hivyo sasa yatakatwa asilimia tisa.
Alisema mapato yanayoanzia Sh360,000 hadi 540,000 hukatwa PAYE pamoja na asilimia 20 ya excess charges, wakati mshahara unaozidi Sh540,000 hukatwa PAYE pamoja na asilimia 25 ya makato ya excess charges.
Suala hilo pia lilizungumzwa na mchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa, Godlisen Malisa katika waraka alioutuma kwenye mtandao kuchambua punguzo hilo la Rais Magufuli.
Malisa alionyesha kushangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kusifu punguzo hilo, wakiwamo wabunge wa upinzani.
“Kama Rais angepunguza excess charges, angalau zikafika 10% kutoka 30% ziliko sasa, ingekua na maana kubwa sana kuliko kupunguza PAYE,” anasema Malisa katika waraka huo.
“Kwa kifupi ni kuwa punguzo hilo litawanufaisha zaidi wenye mishahara chini ya 720,000/= lakini kwa wanaolipwa zaidi ya hapo hakuna benefit (manufaa) yoyote. Hata hao wanaolipwa chini 720,000/= bado watanufaika kidogo sana.”
Alidai kwamba kama kuna mbunge yeyote anayeshangilia punguzo ni wazi kuwa hajui hesabu, hivyo anatakiwa kukumbushwa ili aelewe kuwa kupunguza PAYE wakati makato yanayozingatia viwango vya mishahara yako palepale, ni kiini macho.
“Yaani Rais JPM alichofanya ni kutulazimisha tukatae ongezeko la mshahara,” anasema.
Alisema ni kweli wapinzani waliomba PAYE ipunguzwe tangu mwaka 2011 kwamba isomeke kwa tarakimu moja na ndivyo alivyoahidi JPM, lakini pia walishauri kuwa gharama za makato hayo ya zaidi yalingane.
“Nimeamua kusema hivi maana naona wabunge wengi wa (vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi) Ukawa wanacheza ngoma ya Magufuli. Wanaanza kujitapa (kwamba) upinzani tulishauri jambo hili tangu mwaka 2011,” anasema.
“Wengine wanapiga picha hadi hotuba ya kambi ya upinzani iliyozungumzia jambo hilo. Waambieni wakae kimya na wasiendelee kuongea vitu wasivyovijua.”
Mtaalamu wa masuala ya kodi, Dk Mariam Nchimbi alisema kiwango cha mshahara kingepandishwa ni wazi kingesaidia wengi kujipanga vyema, ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa kodi zinazostahili.
“Ni wazi kwamba kwa hatua hiyo ya Rais imewasaidia kwa kiasi fulani wale wanaolipwa mishahara ya kiwango cha kati, lakini wale wa kiwango cha juu pia walipaswa kupunguziwa japo kwa asilimia 28 badala ya 35 inayokatwa sasa,” alisema.
Lakini wachambuzi wengine waligeukia suala la kukuza uchumi wakisema ndilo litakalosaidia mfanyakazi kunufaika na mshahara wake.
Profesa Humphrey Moshi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema mshahara wenye nafuu kwa maisha ya wafanyakazi wengi utapatikana kutokana na uwepo wa viwanda vya kutosha pamoja na kilimo kuimarishwa.
“Kuna mambo mengi ya kuangalia ili mfanyakazi awe na mshahara ambao unampa unafuu wa maisha,” alisema Profesa Moshi.
“Pato la Taifa linahusika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama litajengewa mazingira ya kukua, itakuwa vyema. Inatakiwa viwanda vichangie pato hilo kwa asilimia 25 na si asilimia nane kama ilivyo sasa.”
Alisema anaamini baadhi ya viwanda hivyo vitakuwa vya kusindika mazao, kutakuwa na kilimo cha biashara ambacho kitaongeza tija.
“Ninaamini kuwa mbali na maeneo hayo, viwanda vingine vingi vinaweza kuendelezwa kama vya usindikaji mazao ya kilimo na uzalishaji ,” alisema.
Alisema kwa upande wa Serikali mshahara wenye nafuu ya maisha kwa watumishi wake unapaswa kujengewa mazingira labda kwa kuweka idara maalumu ambayo inaangalia viwango vya mishahara.
“Kwa ilivyo sasa ni wazi kuna watumishi ambao wananufaika kama alivyowahi kueleza Rais. Yaani watu wanalipwa mishahara kama wapo Ulaya. Sasa mfano unaweza kukuta mtu kaajiriwa hapa UDSM ni msomi kwa viwango, lakini analipwa Sh3 milioni wakati mwenye digrii aliye Benki Kuu analipwa Sh6 milioni,” alisema.
Profesa Moshi alihoji kwa viwango hivyo viwili tofauti, nini kimetumika kuamua mwenye elimu kubwa alipwe kidogo na mwenye elimu ndogo alipwe zaidi.
Alisisitiza kuwa Serikali inapaswa kuzibana bodi za taasisi zake ambazo zimejijengea mazingira ya kulipa mishahara ya mamilioni ya fedha bila kujali hali ya nchi kwa ujumla.
Msomi mwingine, Dk Ulingeta Mbamba kutoka Shule ya Biashara ya UDSM, alisema Serikali inabidi idhibiti mfumuko wa bei.
“Ni wazi kwamba hata kama Serikali itaongeza mshahara, bidhaa zikawa zinapandishwa kiholela, hakuna siku kiwango cha mshahara kinaweza kutosheleza maisha ya watumishi,” alisema.

Wasafi Wadaiwa Kumpora Producer Frag Ngoma ya 'Bado' iliyoibwa na Harmonize Feat. Diamond

Producer Frag kutoka Uptown Music ametumbua jipu baada ya kuibuka na kusema kuwa yeye ndiye aliyetengeneza wimbo wa Bado wa Harmonize na Diamond.
Frag aliiambia Enewz kuwa pamoja na kazi kubwa aliyoifanya kuhakikisha ngoma hiyo inakuwa poa lakini bado WCB wakamzima na hawakumlipa hata senti tano na kuambulia elfu thelathini pekee ya nauli.
“Kawaida nikifanya kazi uptown music lazima saini zangu ziwepo lakini kwa kule wasafi saini zangu hazikuwekwa, na sijajua kwasababu gani hazikuwekwa wangeweka tu ata ile saini ya jina langu ili kunitengezea heshima kwa watu wengine ”, alisema Frag.

Aliyejifungua Watoto 3 Anaomba Asaidiwe kwani naye ni Mgonjwa wa Pumu

MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia kuwatunza watoto hao.
Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu ambao umemsababisha kuvimba mwili wote.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababisha kuwa na hali ngumu ya kimaisha ambayo inamfanya kushindwa kuwatunza vizuri watoto wake.
Alisema watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine walizaliwa kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma huku kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa mwisho kilo mbili.
“Hali yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu,ambapo wakati mwingine nalazimika kuwanywesha maziwa ya ngombe watoto hao pindi ninapozidiwa na ugonjwa huo”alisema .
Kwa upande wake baba wa watoto hao Sokoine Chipanta alisema pamoja na juhudi za kilimo hata hivyo mazao yake yalinyauka na jua.
Alisema kutokana na hali hiyo analazimika kutafuta vibarua ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kununua chakula pamoja na matunzo ya watoto hao.
Alisema kwa wale wote watakaoguswa na kuamua kumpa msaada wawasiliane naye kwa namba ya simu +255 652 744 510.

PENZI la Mwanamuziki Shaa na Master Jay...Shaa Afunguka Kinachoendelea Kwa Sasa....

Master J na Shaa wamekuwa kwenye uhusiano kwa miaka mingi sasa na wameendelea kuwa imara.
akini pamoja na kuwa hivyo, bado uhusiano wao wa kikazi una nafasi kubwa zaidi. Hali hiyo ndiyo imemfanya Shaa kujitahidi kutofautisha uhusiano wao na kazi kwakuwa kwake Master J ni bosi wake.
Master J na Shaa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye mradi wa Cocacola Popstars takriban miaka 10 iliyopita.
Bonyeza HAPA kudownload application ya UDAKU SPECIAL kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Labels: Master J , Shaa
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
“Bosi wangu meaning ni CEO wa MJ Records, label iliyonisaini na ananisupport sana namshukuru mwenyezi Mungu, ni CEO lakini ni one of my best friends, nimemfamu sasa for ten years,” Shaa alikiambia kipindi cha Chill na Sky.
“He is one of my close advisors, ananishauri sana na nasikiliza sana ushauri wake, akikataa kitu nazingatia, akiniambia fanya hivi nasikiliza. Kwahiyo kama Shaa, Master ni my CEO, my boss and my very close friend, kama Sarah hayo ni ya Sarah.”


Wabunge Watwangana Ngumi Bungeni..

Wanachama wa chama tawala cha Uturuki cha AK na chama kinachoungwa mkono na Wakurdi wamepigana ngumi bunge kuhusiana na mpango kuwaondolea kinga wabunge ya kutoshitakiwa.
Wabunge wakionyeshana umwamba Bungeni nchini Uturuki
Ngumi hizo ziliibuka bungeni wakati kamati ya bunge ilipokutana kujadili mabadiliko hayo yanayoungwa mkono na serikali ili kubadili Katiba kuwaondolea kinga hiyo wabunge.
Baadhi ya wabunge walikunjana mashati kwenye meza, wengine wakirusha chupa za maji na kurushiana ngumi bungeni.

Ole Wao Wanaowapa Ujauzito Wanafunzi-Ummy

Serikali imewaagiza Maafisa maendeleo ya Jamii na maafisa ustawi wa Jamii wa wilaya,kata na mikoa nchini kuwafatilia wanaume wanaowapa ujauzio wanaume wanaowapa ujauzito watoto wa shule na kuwafikisha Mahakamani.
Akizungumza leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema serikali haitamvumilia mwanaume yoyote anaempa mwanafunzi ujauzito.
Mhe. Ummy amesema kuwa serikali ya awamu ya tano itawachukulia hatua wanaume wote na hakutakuwa na huruma juu ya hilo huku akisisitiza wanawake ambao si wanafunzi ni wengi mitaani.
Hapo awali Akijibu Swali la Mbunge wa Ileje, Mhe. Janeth Mbene, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa tatizo la watoto kupewa ujauzito nchini linatokana na vishawishi wanavyokutana wakiwa njiani wakati wanakwenda mashuleni.