Jumatatu, 28 Novemba 2016

Angalia Thamani yako, Yanini Kumng’ang’ania Asiyekupenda?


Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe  si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala humjali.

Muunganiko wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi.

Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana halisi ya mapenzi ipo kwa anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani. Ndani ya mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku.

Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hakupendi, bali unakuwa naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe maana yake hata uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi.

Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta na si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana mmoja aliyewahi kuniambia anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia  kuna msichana yupo anampenda na kumjali ila si yeye.

Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule mwingine, jamaa aliwahi kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana na yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu msichana.

Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza msichana huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa naye hivyo hivyo.

Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa. Kweli walikuwa pamoja. Ila  unajua kinachomkuta sasa?

Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine anamtumia huyu kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila kutafakari mara mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo itamfanya huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa.

Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?

Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.

Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.

Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako.

Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.

Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema wapendwa.

LADY Jay Dee Arusha Jiwe Kigazani Baada ya Kauli ya Ruge Kuwa Walishamalizana


Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo.

Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini kwa kuogopa kuingia matatani na kituo hicho chenye nguvu nchini, walifuta sauti yake.

“Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ? Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana  #SawaNaWao #TofautiNaHesabuZao,” aliandika Jide.

Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.

Ruge pia alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.

“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako' Afunguka Kuhusu Sakata la Kuwatukana Majirani Zake


Siku tatu baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo akisema anaishi kana kwamba hana jirani.“...Tunaishi kama majambazi tu, hujui jirani yako ni nani,” amesema.


Lusekelo amesema Yesu ambaye ni  mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi ya utumishi wake.


Amesema magazeti wa  mitandao ya kijamii hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpasha ila Mungu pekee.


Katika mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili nyingine za karibuni kanisani kwake, Ubungo Kibangu, mchungaji huyo aliingia kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla ya waumini kuanza kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.


Katika mahubiri hayo alisema haiogopi jela, bali anaogopa kuvunja sheria za nchi na wala alipokamatwa na Polisi haikumtisha wala kumvunja moyo, kwani viongozi wa dini wamekula kiapo hadi kufa.


Aidha, alisema wapo waliosema kuwa Mzee wa Upako alikuwa anatukana, alidai kuwa matusi yake yote ni maandiko na anayetaka ufafanuzi wowote akipata nafasi amuulize yameandikwa katika vitabu gani li apate kuelewa.

Alisema mpumbavu sio tusi hayo ni maelezo na Yesu alitukanwa sana, na hata ushenzi si tusi lina maana pana ya kwamba huna hofu ya Mungu, mjinga ana dhambi ya mauti, inayomsubiri kwenda peponi.

Hata hivyo, aliwausia waumini wa kanisa hilo kuwa kamwe wasimtukane mtu kwa umbo ama rangi yake kwa kuwa hakupenda kuzaliwa hivyo na waishi hivyo kwa kutenda mema kwa kuwa ufalme wa Mungu watauona.

Alisema tangu kutokea kwa tukio amekuwa akipigiwa simu na watu ambao hakuwategemea huku waandishi wakimtaka kuzungumzia chochote wakiwamo waandishi wa habari ambao alisema walikuwamo ndani ya kanisa hilo jana.

Akifafanua kilichotokea siku hiyo, alieleza kuwa alitoka saa 11 alifajiri bila kufafanua alikuwa akitokea wapi, ndipo alipokutana na watu wawili akiwemo Mmasai na dada mmoja alipowauliza wanatokea wapi katika eneo hilo ambalo wakazi wengi wa huko hutoka na magari yao, ndipo ugomvi ulipoanzia.

“Hawa watu wa magazeti wanataka kuuza magazeti, barabara hiyo nimeijenga mimi hivyo nilikuwa na haki ya kuwauliza maana ni kibarabara... washenzi wakubwa wanaandika tu, halafu wanasema nimewatukana majirani kule hakuna jirani hajui wanaingia saa ngapi na wanatoka saa ngapi na hakuna hata habari za asubuhi. Kila mmoja anatumia gari lake,”alieleza Mzee wa Upako.


“Kwanza waliandika habari kwamba waumini hawatakuja kanisani badala yake wamejitokeza bila kukatishwa tamaa. Wakati mnajitokeza hapa mbele (kutoa sadaka), alipita mama mmoja amebeba mtoto, nilimwombea mwaka jana hapa kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto, sasa mbona magazeti yasiandike habari hizo?”


“Kwa nini wasiandike hayo mazuri ‘front page’ (ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani,matatani babu yako.”


“Najua na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme, nasubiri mmalize kwanza nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema, baada ya mwezi mmoja najua mtakuwa mmemaliza,”alisema.

Lowassa Awajibu wanasiasa waliodai ni mgonjwa na atakufa


Aliyekuwa  mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura kwa wingi licha ya baadhi kumsema vibaya kwa kumwita mgonjwa na kwamba angekufa.


Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo mjini Mbinga mkoani Ruvuma ambako chama hicho kipo katika ziara ya kufanya mikutano ya ndani.


Akizungumza ndani ya vikao hivyo, Lowassa pasipo kutaja jina la mtu yeyote alisema: “Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa sababu wote hata walionisema mabaya baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.”


Alisema kitendo cha wananchi kumpigia kura kwa wingi pamoja na kwamba alikuwa akizungumziwa vibaya juu ya afya yake, ni wazi kuwa walikubali kubeba lawama juu yake.


“Bila ujasiri na umoja wa dhati, hawa jamaa wataendelea kutupiku… lakini niwashukuru vile vile kwa kukubali kubeba lawama juu yangu, wapo waliosema huyu ni mgonjwa atakufa, bado mlinipigia kura nyingi ila Mungu ndiye hupanga yote,” alisema.


Pamoja na hayo, Lowassa aliwataka wanachama wa Chadema kuendelea kuwa na ujasiri na kudumisha umoja kwa kuendelea kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.


Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuzungumza juu ya watu ambao walihoji kuhusu mwenendo wa afya yake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.


Baadhi ya wanasiasa, hususani wale waliokuwa wakimpinga, walijaribu kuionyesha na hata kuiaminisha jamii kwamba mwanasiasa huyo ni mgonjwa na hafai kuongoza nchi.


Wapo ambao walidiriki kusema kwamba Ikulu si hospitali na wala hakuna gari la kubebea wagonjwa.


Miongoni mwa wapinzani wake ni baadhi ya wanasiasa wakubwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo viongozi waliosikika katika majukwaa ya kampeni  mwaka jana wakiwashawishi wananchi kutomchagua Lowassa kwakuwa hata akipata urais hatotawala muda mrefu atakufa.


Wapo waliokwenda mbali na kusikika wakimwambia Lowassa Ikulu si wodi ya wagonjwa, hivyo hafai kupatiwa nafasi ya urais kulingana na afya aliyonayo.


Mikutano ambayo Lowassa ameitumia kuzungumzia suala hilo, inafanyika nchi nzima pamoja na kuwahusisha wajumbe wa ngazi mbalimbali za chama.


Uwepo wa Lowassa katika mikutano hiyo imesababisha watu wengi kukusanyika wakitaka kumuona.


Hata Lowassa anapokuwa anaondoka katika eneo hilo kuelekea mahali kupumzika, wananchi wamekuwa wakiunga msafara kwa kumfuata nyuma.


Mikutano hiyo inatajwa kuwa sehemu ya operesheni ya siku 40 inayofanyika nchi nzima iliyopewa jina la ‘Amsha Amsha

WATUMISHI Waliosoma Vyuo Vikuu Bila Sifa Kufukuzwa Kazi


Baada ya matamko kadhaa kadhaa ya serikali kuhusu Sekta ya Elimu nchini hatimaye leo limeibuka jingine la kutimua watumishi wote wa umma waliojiunga na vyuo vikuu na kutunukiwa "degree" bila kuwa na sifa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako wakati akifungua maonesho ya vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU) yanayofanyika viwanja vya Karimjee, jijini Dar.

Maonesho hayo yanashirikisha vyuo 61 ambapo 12 kati ya hivyo ni kutoka nje ya nchi.
Katika taarifa yake Ndalichako amesema Wizara yake inawasiliana na idara ya Utumishi ili kuwabaini watumishi wote waliojiunga vyuo vikuu bila sifa na wafukuzwe kazi. "Kama wewe ni mfanyakazi uliyesoma moja ya vyuo vikuu ukafaulu lakini hukuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu, tutakunyofoa hukohuko kwenye ajira yako" Alisema Ndalichako.

Kufuatia agizo hilo la Ndalichako, watumishi wote waliosoma vyuo vikuu kwa kupitia foundation courses kama Pre Entry/Remidial/Certificates, etc,wataondolewa kazini. Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa ya kusoma degree. Amesema kuwa kama mtu hakupata points za kumuwezesha kujiunga chuo kikuu hata asome foundation course bado hatapata sifa, namna pekee ya kupata sifa ni kurudia mtihani wa kidato cha sita.

Agizo hilo pia litawagusa watumishi waliojiunga na elimu ya juu kwa ufaulu linganishi (equivalent pass) ambapo kwa wale waliotoka diploma na wakasoma degree bila kufikisha GPA iliyowekwa na NACTE watatimuliwa. Pia waliotoka kidato cha sita na kupata nafasi vyuo vikuu moja kwa moja lakini hawakufikisha "cut off points" zilizowekwa na TCU wataondolewa katika ajira zao.

Prof.Ndalichako amesema zoezi hilo litaanza baada ya kumaliza zoezi la uhakiki wa sifa kwa wanafunzi wanaopata mikopo. "Tukimaliza hawa wanaopata mikopo, tutahamia wasiopata mikopo kuona kama wana sifa za kusoma vyuo vikuu, baadae kwa wafanyakazi. Hata kama hukupata mkopo, lakini ulisoma chuo kikuu bila sifa hauko salama" Alisisitiza Ndalichako.

PAUL Makonda Atoa Siri " Wapo Wanaoshinda Kwa Waganga na Wanaovaa Hirizi Wasitumbuliwe"


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amendelea na ziara zake za kutatua kero za Wananchi ambapo leo ameianza wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na Watumishi wa Umma wa Wilaya hiyo, Makonda alisema kuwa wapo wanaoshinda kwa waganga na wanaotumia hirizi ili kujikinga wasitumbuliwe.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya hiyo DC Ally Hapi amesema kuwa atahakikisha anawashughulikia watendaji ambao hawawajibiki ipasavyo katika nafasi zao.

HIZI Hapa Sababu Tatu za Jiji la Mbeya Kuwa la Pili Kwa Wingi wa Makanisa Afrika

Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo lina makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.

Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.

Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.

Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.

“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo.

Mwananchi.

Kiwanda cha Saruji cha Dangote Kimesitisha Uzalishaji wa Simenti...Sababu Hizi Hapa


Kiwanda cha Saruji cha Dangote kimesitisha uzalishaji kutokana kuelemewa na gharama za uendeshaji hatua inayowaacha watumiaji wake njia panda.

Mwezi uliopita Kiwanda hicho kilililamikia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini(TPDC) kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara

Pia kiwanda hicho kinapinga uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo yapo chini ya kiwango na bei ghali.

Jumatano, 23 Novemba 2016

Ndoa Ina Mwaka Sasa Inanishinda, Sina Hamu ya Kufanya Tendo la Ndoa na Mke Wangu

Naombeni ushauri jamani,

Nimeoa na ndoa yangu ina mwaka sasa. Mke wangu ana tabia nzuri sana kiasi kwamba kila mtu ananisifia kuwa nimepata mke bora.Tatizo linakuja kitandani, yaani si enjoy chochote kile kutoka kwake najikuta sina hamu naye kabisa hali inayopelekea niwe nasingizia naumwa ili asiombe mechi.

Na nilimuoa kwa sababu ya tabia yake na hatukusex mpaka ndoa! Nashindwa kutoka nje kwa sababu ya heshima niliyonayo ndani ya jamii na pia kuheshimu ndoa yangu na isitoshe kwa sasa tuna mtoto mchanga. Ana maumbile makubwa na pia maji mengi nimefikia hatua hata abaki uchi mbele yangu sisimki kabisa.

Nimecreate account fake ili nipate ushauri please

Jamani nifanyeje kwani si enjoy kabisa maumbile yake?

Aunt Ezekiel: Achana na Mimi Wewe Wema Sepetu

MASTAA wawili waliokuwa mashosti siku za nyuma, Aunty Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wameingia kwenye msuguano tena hivi karibuni huku hali ikionesha kuwa mastaa hao kwa sasa ndiyo basi tena.

Hali hiyo imetokea juzi baada ya Aunty kuweka picha ya kumtakia siku njema ya kuzaliwa rafiki na msanii mwenzake, Maimartha Jesse kwa kuandika, “Happy bday Kipenzi cha Roho yangu …..Unajua kama Nakupenda cha zaidi Naomba Yesu Akutunze milele.”

Katika post hiyo, followers kadhaa wa Aunty walikomenti akiwemo staa mwenzake kwenye tasnia hiyo, Wema Sepetu aliyekomenti “Yesu atamtunza…” Baada ya hapo, Aunty akaibuka na kumtolea povu Wema akimchana “Achana na mm ww @wemasepetu“ hali iliyoibua maswali na mijadala mingi mitandaoni, huku watu wakitaka kujua kwa nini Aunty amemshushua hivyo Wema.

Inasemekana kwamba, chanzo ni Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Wema kumsema vibaya Aunty kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram. Kwa hali ilivyofikia mpaka sasa inaonesha sio rahisi tena kwa waigizaji hao kuelewana.

Tangu siku za hivi karibuni, Wema alipokosana na rafiki yake Muna Love na kumsema vibaya kwa kutumia video aliyojirekodi na kuisambaza mitandaoni, Wema kwa sasa amekuwa akijitahidi kuwa karibu na Aunty ili warudishe urafiki wao wa zamani japokuwa jitihada zake zinaonesha kugonga mwamba baada kuambulia maneno mazito kutoka kwa Mama Cookie.

SAKATA la Oparesheni UKUTA: Viongozi wa Dini Waendelea Kusubiri Maombi Yao Kujibiwa na Rais Magufuli

Viongozi wa dini nchini waliopanga kumwona Rais John Magufuli kwa mazungumzo kuhusu hali ya siasa nchini wanaendelea kusubiri maombi yao kujibiwa licha ya kupita zaidi ya siku 90 sasa.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo  jana alisema: “Siwezi kusema Rais amekataa kuonana nasi, hapana. Labda ni kwa lile tulilokuwa tuende kumuona nalo (Ukuta) lakini kwa mazungumzo mengine milango ya Rais iko wazi,” alisema.

Wazo la viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kutaka kuonana na Rais lilibuniwa Agosti ili kuzuia maafa ambayo yangejitokeza baada ya Chadema kutangaza kufanya maandamano waliyoyapa jina la Ukuta, Septemba Mosi.

Hata hivyo, Dk Shoo alielekeza atafutwe Katibu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Dk Leonard Mtaita kwa maelezo zaidi akisema ni mmoja wa wanaoratibu suala hilo.

Dk Mtaita alipotafutwa kwa mara ya kwanza Septemba azungumzie kama barua waliyopeleka kwa Rais imejibiwa alisema tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na kusababisha maafa makubwa litachelewesha mpango wao wa kukutana na Rais.

Hata hivyo alipotafutwa tena jana, Dk Mtaita aliomba atafutwe mwenyekiti mwenza wa kikao kilichoibuka na wazo hilo ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim.

“Tumewaachia wenzetu walioko Dar es Salaam, Sheikh Salim ndiye mwenyekiti mwenza na yeye yuko Dar na ndiye alijitolea kufanya mawasiliano na Mheshimiwa Rais,” alisema Dk Mtaita.

Sheikh Salim alipotafutwa ili aeleze alipofikia kufanikisha kuonana na Rais alijibu kwa kifupi tu: “Sisi tuko katika kusubiri. Barua tulishatuma kwa Mheshimiwa Rais. Tunasubiri tu”.

Msemaji wa Serikali, Hassan Abass alipoulizwa alitaka atafutwe Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa kwa kuwa ndiye msemaji wa Rais.

“Mtafute Msigwa maana yeye yupo karibu na Mheshimiwa (Rais Magufuli) na anajua ratiba zote,” alieleza.

Alipotafutwa, Msigwa aliwataka viongozi hao kuendelea kusubiri kwa kuwa kila kitu kina utaratibu wake na pia inategemea ratiba ya Rais.

“Kama wameandika, wasubiri watajibiwa,” alisema Msigwa.

Viongozi wa Chadema wanaposoma Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa wanaona wana haki ya kufanya mikutano ya ndani na hadhara na maandamano mradi tu Jeshi la Polisi litaarifiwe siku na mahali pa shughuli hiyo.

Rais Magufuli alipiga marufuku siasa za ushindani hadi mwaka 2020 jambo ambalo Chadema waliamua kujitokeza kupinga kwa maandamano.

Mbali ya Rais Magufuli, Jeshi la Polisi lilitangaza kuwa ni marufuku kufanya mikutano na maandamano.

Hali hiyo iliyotishia kuwepo makabiliano yenye maafa ndiyo iliyowaibua viongozi wa dini ambao walichukua hatua kwanza kuwasihi viongozi wa Chadema na pili kuwataka wasubiri mrejesho.

MBUNGE Godbless Lema Aingia Siku ya 22 Mahabusu

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameendelea kusota katika mahabusu ya Gereza la Kisongo mjini hapa akiingiza siku ya 22 leo baada ya jana kukwama katika azma yake ya kutaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliomnyima dhamana.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Moshi ndiye aliyetupilia ombi la Lema, hivyo kumfanya arejee mahabusu huku mawakili wake wakihaha kuhakikisha wanakata rufaa ili kuomba dhamana hiyo katika ngazi nyingine ya kisheria.

Aidha, Jaji Moshi ameridhia ombi la Lema kupitia kwa mawakili wake Sheck Mfinanga na Peter Kibatala la kukata rufaa mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe na hatimaye Lema kupata dhamana baada ya kupitiwa na jaji atakayepangiwa.

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo, Jaji Moshi alisema kimsingi hoja ya mawakili wa Lema ya kutaka mahakama hiyo kuitisha faili na kulipitia haina msingi wowote kisheria hivyo anaitupilia mbali hoja hiyo na kutoa rai kwa mawakili hao kukata rufaa Mahakama ya Rufaa ili dhamana ya Lema isikilizwe.

“Mahakama hii haiwezi kupitia faili la kesi hii ya Lema ya kupata dhamana hivyo siwezi kupitia faili hili, bali nashauri mkate rufaa ili iweze kusikilizwa,” alisema Jaji Moshi.

Awali Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu la kuitaka wasisikilize maombi ya Lema ya kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 kwa madai yapo makosa ya kisheria yaliyofanywa awali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa lengo la kumnyima dhamana mbunge huyo.

Akiwasilisha hoja zake mbele ya Jaji Moshi katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Kadushi akisaidiana na Materu Marandu alisema anawasilisha hoja mbili za pingamizi za mahakama hiyo kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Alisema kimsingi maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 yanakinzana na kifungu cha 43 (2) cha sheria ya Mahakama ya Mahakimu. Katika kesi hiyo, Lema anashitakiwa kwa kutoa maneno ya kumtusi Rais katika maeneo tofauti.

Kadushi alisema uamuzi unaopinga kufanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kukubali kutompa dhamana Lema ni uamuzi mdogo na haukuwa na sababu za kukataa dhamana.

“Mahakama yako inafungwa mikono na kifungu hiki kufanya mapitio au uamuzi mdogo, hivyo tunaomba mahakama itupilie mbali maombi hayo,”alisema Kadushi ambaye wakati akiwasilisha hoja zake alikuwa akinukuu mashauri mbalimbali ya kesi zinazofanana na hiyo.

Aidha, Kadushi alisisitiza kuwa wao wanatambua haki ya kukata rufaa ipo wazi kwa mleta maombi ila itakuwa jambo geni kama mahakama itawapa nafasi kusikiliza maombi yao. Alisema hoja ya pili ya pingamizi lake, linatokana na mleta maombi kutokidhi matakwa ya kisheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Katika sheria ya makosa ya jinai, kifungu cha 359(1) ya mwaka 2002 kuwa mtu asiporidhika na maamuzi ya mahakama ya chini kama ilivyo katika kesi hiyo, kamwe hawezi kuwa na mbadala wa mapitio ya rufaa.

Akijibu hoja hizo Wakili anayemtetea Lema, Peter Kibatala akiwa na jopo la mawakili wenzake, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, John Mallya, Faraji Mangula na Charles Adiel, alipinga kuwekewa pingamizi hilo na kuomba mahakama isikilize maombi yao.

Alisema wao wamefungua maombi hayo kuiomba Mahakama Kuu kuitisha jalada la kesi ya mahakama ya chini ili kuona uhalali wa kutotekelezwa kwa uamuzi wa kutoa dhamana, kwani kilichokuwa kinasubiriwa ni masharti ya dhamana.

“Huyu mshitakiwa alipewa dhamana , ila kabla ya mahakama haijatoa masharti ya dhamana, upande wa serikali ukasimama kabla mahakama haijaweka masharti ya dhamana ambayo lazima ifanye hivyo, wakasema wameonesha nia ya kukata rufaa na mahakama ikakubaliana nao bila kutekeleza amri yao,” alisema Kibatala.

Aliomba mahakama hiyo itupilie mbali pingamizi la serikali na kuiomba kuendelea na kazi iliyokusudia kuifanya ya kupitia maombi yao ili kutoa dhamana kwa mshtakiwa au iamuru mahakama ya chini kuendelea na uamuzi wake.

Wakili wa mbunge huyo baada ya maombi yao kugonga mwamba, walikuwa kwenye hekaheka ya kukamilisha kuandika rufaa ili kumnasua Lema atoke mahabusu.

Baada ya kutoka nje ya Mahakama Kuu, Wakili Mfinanga alisema wanamalizia kukamilisha taratibu za wao kukata rufaa Mahakama Kuu na wataomba rufaa hiyo isikilizwe kwa hati ya dharura ili kumnasua Lema mahabusu.

BAADA ya WCB Kutoa Wimbo , Ommy Dimpoz Atao Mapovu, Diamond Amjibu na Kuvujisha Siri ya Ugomvi Wao

Hii baada ya domo na mavoko kuachia ngoma povu likamtoka ommy akimshushia domo kuwa aache mziki wa ujanja ujanja akimanisha kuwa domo aache tabia zake za kununua view, tunzo kuwa awekeze kwenye mziki mzuri usio na ujanja ujanja naye domo hakuwa mbali akamjibu kuwa nae apunguze tabia za kipunga


Hata hivyo kama mnavyojua Diamond na uswahili wake hakutaka kuacha lipite kimya kimya akaamua kumjibu ommy dimpoz kwa kutupia dongo

VIDEO Mpya: Mabibi na Mabwana.. Tumealikwa Kuitazama Mpya ya Rich Mavoko ft. Diamond

WCB wanayofuraha kutualika kuitazama video mpya ya kijana wao Rich Mavoko ambayo kamshirikisha Boss wake Diamond Platnumz, ukishamaliza kuitazama video hii ni ruhusa kuacha na comment yako umeionaje na wimbo wenyewe ili wakipita baadae wajue watu wao wameipokeaje.

Nimekuta Mafuta ya KY na Babcare Kwenye Mkoba wa Mchumba Wangu

Ni jambo limenishangaza kifupi sina tabia ya kumfuatilia mpenzi wangu iwe kwenye simu au kwenye mambo mengi but hii ilinibidi tuu.

Wakati mchumba wangu alipokuja kwangu weekend hii na kushinda siku tatu nikajitoa ufahamu ili nisiishi kama fala nikajikuta nikiwa room nikachukua mkoba wake nikawa naangalia nilihamaki baada ya kukuta mafuta ya KY na babycare, mawazo yalinipeleka mbali sana kwa kweli hadi kupelekea kuvuta picha tuwapo faragha mbona my wangu sehemu zake za siri siyo kavu labda huwa anakauka (lubricant)?

Sasa nikakosa jibu ila nikaogopa kumuuliza maana ningeweza kuzua mengine. Sasa nijikaze nimuulize au nitumie njia gani kumuuliza au haya mafuta ya ulainishaji anatembea nayo kwa ajili gani na hajawahi kutumia na mimi...

Jumanne, 22 Novemba 2016

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya


Kafeina ni nini?:

1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’.
Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina.

Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini.

Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya.

2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics).
Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai, kahawa au soda.

Madhara yake ni nini?, Moja; kama unakunywa kinywaji na muda si mrefu unalazimika kwenda kukitoa inamaanisha kinywaji hicho hakikutumika vema na mwili. Pili; kumbuka ulikunywa kikombe kimoja na umeenda kutoa viwili, hivyo umekopwa maji mwilini mwako na ukumbuke kuwa MAJI NI UHAI.

3. Kafeina husababisha KANSA.
Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini. Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi asidi.

Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.

4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamin mhimu mwilini.
Kafeina ambayo ni kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.

5. Kaffeina husababisha kisukari.
Mwili una vyanzo 3 vya nguvu ambavyo ni Sukari, Mafuta, na Maji/Chumvi. Tumesema kaffeina ni kikojoshi, hivyo kaffeina hupelekea upotevu usio wa lazima wa maji mwilini, mwili unapokosa maji kama chanzo chake cha nguvu, moja kwa moja huhamia kuitegemea sukari kama chanzo chake cha nguvu na mwishowe kisukari lazima kitokee.

6. Uchovu sugu.
Wapenzi wengi wa chai ya rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa au chai. Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.

Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili. Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka (Unahamaki) kushughurika na tatizo. Hali hii hatimaye inaweza kupelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.

Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa mwilini kwa ajili ya matumizi yake ya dharura.

Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng. Kuna majina mengine mengi ya visisimuwaji hivi kama vile, kokwa za guru, kokwa za cola na mfalme wa yote ni guarana. Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.

Ungaunga wa guarana hutumika kutengenezea vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye vifungashio vya dawa hizi.

Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe ‘(gluconeogenesis)’.

Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa. Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine. Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.

Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.
Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.

Kituo cha Sayansi kwa maslahi ya umma (Center for Science in Public Interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.

‘Madawa na wewe’, kwa mjibu wa Dr. Earl Mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl Mindell’s New Vitamin Bible’ (zaidi ya nakala milioni 10 zimeuzwa), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi au teja (addicted) wa hiyo kafeina’.

Madhara ya chai ya rangi na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha inakuwa haiishi.

Namna ya kuepuka kaffeina kwenye kahawa na chai:
Badala ya kutumia majani hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako; unaweza kutumia tangawizi na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini.

Kwahiyo unapoinywa chai ya tangawizi siyo tu unaepuka madhara ya kaffeina peke yake, bali pia unakuwa umekunywa dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!. Unaweza pia kuweka mdalasini, mchaichai, kukamulia ndimu, pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea) ambavyo vinapatikana kwa wingi katika soko la Kariakoo Dar – Es – Salaam na Zanzibar.

Kajala: Sijawahi Kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na Paul Makonda


Msanii wa filamu za kibongo, Kajala Masanja amevunja ukimya na kufunguka kuhusu maneno yaliyokuwa yanazunguka mwa muda mrefu mitaani yakimtaja kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda tangu akiwa DC wa kinondoni alipokuwa akishirikiana kwa karibu na msanii huyo kwenye shindano la kusaka vipaji vya wasanii wa Wilaya ya Kinondoni lililojulikana kama Kinondoni Star Search.

Katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Kajala alipoulizwa kuhusu madai ya kuwa na uhusiano na Makonda, alijibu kwa haraka na kwa kifupi: “Hapana sijawahi kutoka naye kabisa. Hilo halipo.”

RC Makonda aliwahi kuzungumzia madai hayo akiwa bado Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ambapo alisema ni propaganda zinazoelezwa na wabaya wake wa kisiasa ambao wamekuwa wakisaka mbinu za kumchafua kila kukicha.

“Ni muda mrefu tu, walianza kipindi kile wakati wa Bunge la Katiba nilipokwenda Bungeni na mwigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, wakasema natembea naye, wakanyamaza. Sasa wamehamia kwa Kajala baada ya kufanya naye kazi", alisema Makonda.

“Hakuna ukweli wowote wanatungatunga tu mambo, watakuwa na sababu zao kwa sababu mtu kama Kajala, maneno yameibuka baada ya kufanya naye project ya kutafuta vipaji vya wasanii.“

"Nimeshirikiana na wasanii wengi wa kiume katika project hiyo lakini kwa kuwa wameona mwanamke ni Kajala peke yake, wanasema vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Najua kuna wengine wanaoeneza haya mambo wanatumika kisiasa lakini mimi sijali".

Bibi Mbaroni Kwa Kumlisha Kinyesi Mjukuu Wake


MWANZA: BIBI mmoja aliyejulikana kwa jina la Amina Hamisi (56) mkazi wa Mtaa wa Mahina, Kata ya Butimba, Jijini Mwanza, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kumlazimisha mjukuu wake Rehema Sadiki (7) kula kinyesi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Augustino Senga amedai kuwa tukio hilo limetokea Novemba 11, mwaka huu ambapo mtoto huyo alikwenda chooni kujisaidia na kushindwa kumwagia maji ili kuondoa kinyesi chake ndipo bibi yake ili kumuadhibu alimuamuru kula kinyesi hicho kitendo ambacho mtoto huyo alikitekeleza.

Baada ya tukio hilo kutokea raia wema walitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.

Kamanda Senga ametoa wito kwa wakazi wa jiii la Mwanza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kudhibiti vitendo vya kikatili hasa kwa watoto wadogo na kuongeza kuwa ukatili ni kosa kisheria hivyo wananchi waache kufanya vitendo hivyo na watakao bainika sheria itachukua mkondo wake.

Mwana FA Aleta Msiba Mkubwa Kwa Kina Dada wa Mjini Kwa Huu Wimbo Wake Mpya...Dume Suruali ft. Vanessa Mdee


Jana Mwana Fa ameachia ngoma yake ambayo ni mwiba mchungu kwa kina dada wa mjini wanaopenda na kuishi kwa kuombaomba. Ngoma inaitwa Dume Suruali.

Nihonge nanunua nini? Kwa nini yani? Kwa kipi nsichokijua ina TV ndani?

Asante FA kwa hii fimbo ya kufungia mwaka haswa kipindi hiki cha Magufuli #TeamDumeSuruali

Dume Suruali ft. Vanessa Mdee - Mwana FA

Chemical: Kwanini Watu Wanashindwa Kuamini Kuwa Mimi ni Bikira?


Rapper wa kike mwenye swaga za hatari Chemical amesema anashangazwa kwa kitendo cha baadhi ya watu wanaompinga kuwa hajawahi kufanya mapenzi.

Hitmaker huyo wa ‘Am Sorry Mama’ amekiambia kipindi cha Kubamba cha Times FM, kuwa aliwahi kuwa na mpenzi lakini waliachana kwa kuwa alikuwa na haraka ya kufanya mapenzi.

“Sijawahi kufanya mapenzi hata siku moja. nimeachana na mpenzi wangu kwa sababu hataki kusubiri, nipo single sasa hivi. Sijui watu kwanini hawaamini wanahisi ni kitu ambacho hakiwezekani aisee,” amesema Chemical.

Kwa sasa rapper huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Mary Mary’ aliouachia siku chache zilizopita.

Tunaheshimu Maamuzi ya Moses Machali Kuhamia CCM- Ole Sendeka


Baada ya kutolewa taarifa ya aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini, Moses Machali  kuhusu kuunga mkono serikali ya awamu ya tano hivyo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi, Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ole Sendeka amezungumzia uamuzi huo.

Haya ndio machache aliyoyatoa Msemaji wa Chama cha Mapinduzi baada Machali kuhamia CCM akitokea chama cha ACT.

“Sisi kama chama cha mapinduzi tunaheshimu uamuzi wake na hatua ya pili kumpokea kwenye chama katiba za kikanuni zitafuatwa na hasa ukizingatia mimi namfahamu ni mtu mwenye msimamo, kwahiyo naheshimu maamuzi yake na hatua zingine zitafuata kwa mujibu wa katiba na kanuni zetu za chama kuwapokea wananchama wanaoingia katika chama chetu kutoka upande wa vyama vingine,”amesema Sendeka.

Taarifa ya aliyekuwa mbunge wa Kasulu Mjini imetolewa na kiongozi huyo yeye mwenyewe.

Baba wa Kambo Anajisi Mtoto Miaka Tatu, Amuua


MTOTO mdogo mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Nyamihaga Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma amekufa baada ya kunajisiwa na baba yake wa kambo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kwamba wamemtia mbaroni mtuhumiwa Hamimu Saidi (27) mkazi wa kijiji hicho cha Nyamihaga.

Akitoa maelekezo kuhusu mkasa huo, Kamanda Mtui alisema mtuhumiwa alitekeleza dhamira yake hiyo wakati mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mke wa mtuhumiwa alipokwenda kisimani kuchota maji.

Alisema baada ya mwanamke huyo kurejea nyumbani kutoka kisimani alimshuhudia mtoto wake akilalamika sana wakati akitaka kujisaidia haja ndogo na ndipo alipomchunguza akagundua kwamba mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na kujeruhiwa kwenye sehemu zake za siri.

Kamanda Mtui alisema baada ya kugundua hilo, mama huyo wa mtoto alimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Maweni kwa matibabu, ambako iligunduliwa kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa na alikuwa amebanwa shingo wakati akifanyiwa kitendo hicho hivyo alikosa pumzi wakati akifanyiwa unyama huo.

Kamanda huyo alisema hata hivyo mtoto huyo alifariki katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni alipokuwa akitibiwa na kwamba baada ya uchunguzi wa kidaktari na uchunguzi wa Polisi, mwili wa mtoto huyo ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

“Kwa sasa mtuhumiwa Hamimu Saidi anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Kigoma wakati upelelezi ukiendelea ili taratibu za kumfikisha mahakamani zifanyike na kwamba anatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi huo utakapokamilika,” alieleza Kamanda Mtui.

Rais Mugabe Asema Anarogwa


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu , lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo.

Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu wapatao 400- walio piagania uhuru kwamba ikiwa atastaafu anapaswa kupewa fursa "inayofaa" kufanya hivyo.

Pia aliwakosoa baadhi ya viongozi wa chama chake cha Zanu-PF kwa kumuombea afe na kujaribu kumroga ili wachukue nafasi yake.

Malumbano ya ndani kwa ndani miongoni mwa wafuasi wa chama tawala ya kutaka kumrithi Bwana Mugabe yameongezeka huku kiongozi huyo akionekana kuendelea kudhoofika zaidi.

Lakini si mara ya kwanza Kwa Bwana Mugabe kuongelea kuhusu kuachia madaraka it's
Mwaka 2006 alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008.

Licha ya hayo aligombea na kushinda katika uchaguzi uliokuwa na ghasia ambao matokeo yake yalibishaniwa.

Kwa hivyo haijawa wazi ni lini , kama kweli Rais Mugabe ataondoka madarakani.
Mnamo mwioshoni mwa juma kamati za kikanda za chama tawala cha, Zanu-PF provincial zilimuidhinisha kama mgombea wake katika uchaguzi wa 2018 , ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.

Chama hicho kitaidhinisha uamuzi huo katika mkutano mkuu wa chama utakaofanyika mwezi ujao.
Kwa hiyo kwa sasa haionekani kama kweli anaangalia uwezekano wa kustaafu.

Wakili wa Serikali Amuomba Radhi Hakimu kwa Kushindwa Kumkamata Tundu Lissu


Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemuomba radhi Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumkamata mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio.

Wakili Mwita alifanya hivyo jana baada ya hakimu huyo, Thomas Simba kumuhoji sababu za kushindwa kutekeleza amri hiyo wakati hati ya kumkamata ilitolewa Novemba 3, 2016 na wakili huyo kuisaini. “Kwa nini hamkumkamata” Si mlikuwa na wajibu wa kumkamata? Mnamuogopa?” alihoji hakimu huyo.

Hata hivyo, pamoja na kuomba radhi hiyo mahakama imechukua hati ya kusafiria ya Lissu ili kudhibiti safari zake nje ya nchi kwa kuwa amekuwa akisafiri bila kuitaarifu mahakama.

Katika kesi hiyo, Lissu na watu wengine watatu wameshtakiwa kwa makosa matano ya uchocheza kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti la Mawio kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 28, 2016 na washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kabla ya uamuzi huo, Wakili Mwita alisema jana ilikuwa siku ya kesi hiyo kutajwa na kwamba upelelezi unakaribia kukamilika.

Kuhusu madai ya kudharau mahakama Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lissu aliiambia mahakama kuwa mteja wake yupo mahakamani, hivyo ametii amri ya mahakama na kwamba jukumu la dhamana ni kuhakikisha mshtakiwa anakuwapo mahakamani wakati wa kesi yake na kwamba uwepo wake ni kutii masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Wakili Mwita alidai kuwa kitendo cha Lissu kutofika mahakamani mara mbili mfululizo ni kama kuonyesha dharau kwa mahakama hiyo.

Mwita alidai kuwa Lissu ni mwanataaluma wa sheria na anafahamu taratibu za kufuatwa kama hafiki mahakamani na kwamba mdhamini si mbadala wa mshtakiwa mahakamani.

“Alipaswa kuandika barua kuitaarifu mahakama hii kama wakili kuwa ana kesi ya uchaguzi anayoiendesha Bunda na kuambatanisha na samansi ama orodha ya kesi. Tunaomba mahakama iheshimiwe na jukumu la kumfutia dhamana ama kutokumfutia dhamana Lissu bado lipo mikononi mwako mheshimiwa,” alieleza wakili huyo wa Serikali.

Akizungumzia hoja hizo, Hakimu Simba alisema Lissu ni wakili maarufu, msomi na anajua taratibu zote za mahakama, lakini wadhamini wake wanababaika, hivyo alimtaka aeleze sababu za kwenda Ujerumani bila kutoa taarifa mahakamani.

Lissu alijibu kuwa hakuwa na nia ya kuidharau mahakama, wala kuikimbia kesi inayomkabili bali alikwenda Ujerumani katika mazingira ya dharura.

Hakimu Simba alimwambia mahakama inafahamu kesi za uchaguzi na maelekezo yake, hivyo ikamuuliza sababu za kutotoa taarifa wakati alipokwenda kushughulikia kesi ya Bunda

“Nilipopata taarifa ya kwenda kuiendesha kesi hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya kutoka nchini Ujerumani na kwamba niliandika barua ya kuitaarifu mahakama na nilituma iletwe mahakamani kupitia wasaidizi wangu,”alisema Lissu.

Lakini Hakimu Simba alisema: “Hakuna barua iliyotufikia. Usituingize katika migogoro kutokana na nafasi yako katika jamii ya mwanasheria. Hatukuogopi labda upande wa mashtaka ndio wamekuogopa.

“Tunataka kufuata mfumo, hatutakuogopa na wala hatutakuonea. Hapa naona upande wa mashtaka wanapiga blaa blaa, tuelewane tunaichukua hati yako ya kusafiria ili ukitaka kusafiri tujue.”

Soudy Brown Afanyiwa Interview, Kumbe Alikuwa Anafanya Kazi TBC


Mzee wa Ubuyu Soudy Brownkafanyiwa interview na TBC amabapo ana dai ndio sehemu iliyomlea
amefungukia aanvyotukanwa instagram na anavyochulia
Pia amesema anapenda kuvaa mask kama swag tu, na akiivua anakuwa sio Soudy Brown tena 

Jumapili, 20 Novemba 2016

Wasira: Uzee Haunizuii Kudai Haki Yangu

Waziri wa muda mrefu na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira amewajibu wanaodai kwamba amelazimika kustaafu siasa baada ya mpinzani wake, Ester Bulaya kuwashinda wapigakura wanne waliokuwa wakipinga ushindi wake wa ubunge wa Bunda Mjini na kusema hajastaafu na uzee haumzuii mtu kudai haki yake.

Juzi, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilimpa ushindi Bulaya katika kesi ya uchaguzi hali iliyotafsiriwa na wadadisi wa kisiasa kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kisiasa wa Wasira.

Lakini jana, Wasira alipopigiwa simu na waandishi wetu kuelezea hatima yake ya kisiasa baada ya kesi hiyo, alisema wanaodai kuwa anatakiwa kustaafu siasa kwa sababu ni mzee hawana budi kuangalia kauli zao kwa sababu wapo wazee wengi anaowafahamu kwa majina na bado wapo madarakani.

“Suala la kusema nimestaafu siasa silijui na sijawahi kusema. Kesi hiyo inahusiana nini na siasa? Wapigakura wameona kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Hakuna uhusiano na uhusiano uliopo ni kwa sababu mimi ni shahidi na mimi niligombea,” alisema na kuongeza:

“Nataka wanipe ‘definition’ (maana) ya kustaafu siasa. Je, ni kunyamaza, nisitoe maoni. Mbona wapo watu walikuwa wanasiasa na bado wanatoa maoni ya kisiasa tena yenye manufaa makubwa?”

Dar Mpya ya Makonda: Makonda Aitaka Takukuru Kuchunguza Madai ya Ufisadi katika Mradi wa Nyumba ‘Avic Town’

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amenusa ufisadi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Avic ‘Avic Town’ na kuitaka taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuuchunguza mradi huo uliopo Kigamboni jijini humo.
makonda-new-jpg-oo

Hatua hiyo imefika baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakiishi eneo hilo na kutolewa pasipo kupewa fidia zao huku ekari 18 za Chama cha Mapinduzi (CCM),zikichukuliwa kwa matumizi katika mradi huo.

Akizungumzia hatua hiyo, Makonda amewataka watendaji wa serikali wanaohusika na taarifa za mradi huo kutoa taarifa sahihi katika vyombo vya dola kwani hataki kuona wananchi wakidhulumiwa haki zao.

“Sitaki kuona kigogo wala kijiti anahusika katika mradi huo. Nitasimamia na polisi waliohusika katika kuwatoa wananchi hawa waseme walitumia vigezo gani kuwatoa,”alisema.

Alisema wananchi walioondolewa eneo hilo wafike kwa Mkuu wao wa Wilaya huku akiitaka Takukuru kuchunguza mafaili ya mradi huo wa nyumba.

Akizungumza huku akilia mkazi wa eneo hilo ambaye pia ni mwathirika wa mradi huo, Pascalina Walioba alisema tangu mradi utambulishwe na kuanza kujengwa hawajalipwa stahiki zao.

“Mimi ni mwathirika wa mradi huo, tangu unaanzishwa na tukahamishwa kipindi hicho nilipaswa kulipwa Sh 700,000 lakini hadi leo sijalipwa na thamani ya fedha inaongezeka,”alisema na kisha kuangua kilio.

Mbunge wa Jimbo hilo, Faustine Ndungulile alisema kuwa wapo watu walikuwa wakidai kuwa ujenzi ule unahusisha nyumba za ulinzi wa usalama.

“Kuna hekari 18 za Chama cha Mapinduzi (CCM) zipo humo lakini tutalifualia,” alisisitiza Ndungulile.

Katika hatua nyingine Wilaya hiyo imeahidiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), hadi kufikia February mwakani watakuwana umeme wa uhakika.

Aidha wananchi wa eneo hilo walitolewa hofu juu ya upatikanaji wa maji safi kwani tayari maji yapo ya visima lakini hakuna mabomba ya kusafirisha maji hayo.

Akizungumzia mradi wa maji katika mji huo, Mwakilishi kutoka Shirika la Maji saifi na Maji taka(Dawasco),….alisema fedha zilizotengwa katika kusambaza maji katika wilaya hiyo ni Sh bilioni 40 huku fedha zinazoitajika ili kukamilisha mradi huo ni Sh bilioni 146.

Ijumaa, 18 Novemba 2016

Model Calisah Afunguka Baada ya Kusambaa Kwa Video yake Akimla ‘Denda’ Wema Sepetu

Weekend hii katika mitandao ya kijamii kumesambaa video inayomuonyesha malkia wa filamu nchini Wema Sepetu akiliwa denda na model Calisah.

Wawili hao ambao walitumia nguvu nyingi kufanya siri mahusiano yao, wameumbuka kupitia video hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Calisah amesema hajui ni nani ambaye amesambaza video hiyo mtandaoni kwani walikuwa nayo yeye pamoja na Wema.

“Nilikuwa nachati na Wema kawaida ghafla nikaona notification, kufungua ndio nikakuta hiyo video na mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kumuuliza Wema kwa sababu video nilikuwa nayo mimi na Wema,” alisema Calisah.

Pia model huyo amedai video hiyo imemsababishia matatizo katika familia yake pamoja na kumpoteza bibi yake kwa presha.

Lady Jay Dee Afunga Ndoa Tena..Apost Picha Akiwa Honey Moon

Msanii nguli na namba moja nchini kwa upande wa kina dada binti machozi, komamdo, anaconda, lady jay dee amefunga ndoa weekend hii kupitia mtandao wa I.G amepost baadhi ya picha akila honey moon uko Zanzibar

Michirizi Inayoonekana Kwenye Miili ya Akina Dada Inaashiria Nini?

Hivi Ile michirizi inayoonekana kwa baadhi ya kinadada nyuma ya goti wakiwa wamevaa sketi fupi huwa ni ishara ya utamu wao kama Mwana FA alivyoimba  "Michirizi ya utamu nyuma ya goti mimi hoi na moyo hai sio toi "  au ugonjwa wa ngozi?

Taarifa Kuhusu Kinachoendelea Kwenye Kesi ya Scorpion Mtoa Macho Mahakamani

Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion anayetuhumiwa kumsababishia upofu wa kudumu Saidi Mrisho umekamilika na hatimaye shauri hilo litasomwa Novemba 30 mwaka huu katika mahakama ya manispaa ya Ilala.

Njwete anatarajiwa kusomewa mashtaka yake baada ya yale ya kwanza kufutwa ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa baada ya kufunguliwa mashtaka mapya.

Huyu ndiye Scropion, kijana aliyejizolea umaarufu ambapo watu wengi hupenda kumshuhudia kila aingiapo na kutoka mahakamani huku kila mmoja akizungumza lake kwa kesi inayomkabili.

Alipoingia mahakamani leo, aliomba ufafanuzi wa wazi juu ya mashtaka yanayomkabili ambapo upande wa jamhuri kupitia kwa wakili wake Chesensi Gavyole walisema ushahidi umekamilika.

Kutokana na kuombwa ufafanuzi, Hakimu anayesimamia kesi hiyo Flora Haule amesema baada ya upelelezi huo kukamilika kesi hiyo itasomwa Novemba 30 mwaka huu, hivyo mshtakiwa atapata ufafanuzi wa mashtaka yake .

Ikumbukwe kwamba Oktoba 19 mwaka huu, Salum Njwete maarufu kama Scropion alifutiwa kesi na kisha kusomewa upya mashtaka yake kutokana na uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliyeomba kufanya hivyo baada ya hati ya awali kuwa na mapungufu ya kisheria

Dalili Muhimu za Mwanamke Aliefika Kileleni Mkiwa Faragha.

Wanaume wengi sana hua tunadanganywa na wenza wetu kua tumewaridhisha vya kutosha lakini ukweli hua hakuna kitu

Hua wanafanya kwa nia njema tu kwani wanaume hua tunajiskia amani sana kuambiwa umemfikisha mtoto wa kike kwani ni jambo la kishujaa kama trumph uchaguzi us

kwa uzoefu wangu,mwanamke aliefika kileleni hua anakua hivi bila hata kuuliza au kusubili kuambiwa

1.MWILI KUISHIWA NGUVU

mwanamke aliefika orgasm hua anaishiwa nguvu mwili baada ya safari ndefu ya mikito,ukiona baada ya sex msichana anauwezo wa kufanya kazi nzito nzito jua umefanya kazi butu sio mpaka uambiwe

2.KUPITIWA NA USINGIZI BAADA YA MECHI

ukiona ka beby kako kamepitiwa na usingiz gafla baada ya sex jua kaz imeenda sawia,ikumbukwe kufika orgasm ni mechanism inzito,

3.MUSCULAR CONTRACTION

mwanamke anaekalibia/ aliefika kileleni misuli hubana na kuachia ,hii ni kwa mwili mzima hadi kwenye vagina,hilitendo pia hufuatiwa na mwili kutoa jasho.
ukiona ivo ujue kazi zimeenda sawia

Wakuu huu ni uzoefu wangu niliopata nikiwa field,

Ukiona mpenz wako hajaonyesha izo dalili muhimu basi jua hakuna kitu

Kama unajua dalili zingine zile kuu na muhimu tiririka

Wazee Pigeni kazi tutokomeze fake orgasm tunazodanganywa na kupewa kiburi ili tutoe chapaa

Udhaifu Huu wa Ali Kiba Unamfanya Diamond Ang'are

Ni ukweli usiopingika wasanii Diamond na Alikiba ni lulu ya taifa kwa sasa hasa unapozungumzia suala la usambazaji wa muziki wa Bongo Fleva kwenda zaidi kimataifa na kuufanya uwe na thamani hata kwa wasanii wengine watakapofikia level zao.

Leo nazungumzia utofauti mkubwa wa wasanii hawa wawili ambao mimi kama #KÄ°JANAMZALENDO nimeuona, Alikiba anaimba vizuri kuliko Diamond lakini kupitia kigezo cha kuimba pekee hakiwezi kumfanya kuwa Msanii mzuri kuliko wengine but kuna mambo mbalimbali ambayo msanii yeyote anapaswa kuyafanya ili awe bora zaidi kuliko wenzake.

1 Alikiba amekuwa akiamini yeye binafsi anaweza kufika international bila kufanya kazi na wasanii wa nje ya nchi Jambo ambalo Si la kweli ili Msanii yeyote uweze kufanikiwa kimataifa lazima ufanye Collabo na wasanii wa level hiyo mfano Wizkid sasa Dunia inamjua kupitia Drake, Davido dunia inamfahamu kupitia Meek Mill,

2 kufanya media tour na Show za kimataifa; Miongoni mwa mambo ambayo Alikiba yanamfanya awe tofauti na Diamond, Alikiba hafanyi media tour za nje anafanya za ndani tu Ndani kila mtu anaufahamu uwezo wake so tunataka aupeleke nje ya Tz pia aanze kufanya matamasha ya kimataifa haiwezekani msanii unataka kwenda kimataifa halafu kwa mwaka Unaperfom Majukwaa matatu tu.

3 Kupunguza Collabo na wasanii wa kawaida; kitu kingine ambacho Kiba anapaswa kukizingatia ni kupunguza Collabo haÅŸa wa wasanii wa kawaida ambao wanataka kupata jina kupitia yeye simaanishi kwamba asikuze vipajj lakini anaweza kuwasaidia kwa kuwasaini kwenye Lebo yake ili bado awe na nguvu ya kuwasapoti.

4 Kuongeza Timu ya washauri: Kingine Kiba anapaswa kuongeza idadi ya watu anaofanya nao kazi ambao ni official lakini hata kuwafanya nao wawe mastaa ili popote wanapofanya interview nado yeye atajwe mfano Alichofanya DÄ°AMOND amembrand DESÄ°GNER, DANCERS ,MAMA, MTOTO, DADA kote huko bado jina lake linatrend

Mwanamke Afa Akiombewa Kwa ‘Nabii’, Akutwa Hana Nywele Kichwani Pamoja na Nyusi za Macho

Mwanamke mkazi wa Unga-Limited jijini hapa, Lightness Kivuyo ameripotiwa kufa wakati akifanyiwa maombi nyumbani kwa mchungaji aliyejulikana kama ‘Nabii Rajabu’ eneo la Kwa-Mrombo pia jijini hapa.

Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Juliana Kivuyo, Lightness alikuwa amesindikizwa nyumbani kwa nabii huyo nyakati za usiku na mumewe aliyemtambulisha kama Shafii Mohammed na kwamba wakati akifanyiwa ibada ya maombi, alianguka na kufariki miguuni mwa ‘Mtume,’ huyo.

“Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya kule kwenye maombi,” alisema Juliana na kuongeza kuwa alitoka mbio kwenda Kwa-Mrombo nyumbani kwa Nabii Rajab na kumkuta dada yake amelazwa kwenye kochi, akiwa bila nguo isipokuwa tu khanga alizofunikwa nazo.

Nabii huyo pia anadaiwa kumnyoa nywele zote pamoja na nyusi za macho wakati akimfanyia ‘huduma,’ hiyo.

Polisi jijini hapa wamethibitisha tukio hilo wakiongeza kuwa tayari watu wawili wamekamatwa kutokana na kifo hicho cha ‘maombi tatanishi.’

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo ameongeza kuwa atatoa taarifa kamili mara baada ya kikao chake na Mkuu wa Mkoa.

Mganga Mkuu katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo amekiri kupokea mwili wa marehemu, lakini akasema, “Kwanza walijaribu kutudanganya kuwa huyo mama alikuwa hai na kwamba aliletwa kwa ajili ya matibabu, lakini tukagundua kuwa walichokileta ni mwili mfu, hivyo tukampeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti!.”

Mkurugenzi wa Huduma ya Mazishi katika hospitali hiyo ya mkoa, Dk Francis Coster alisema mwili ulipelekwa hapo na mume wa marehemu ambaye alisisitiza kuwa mkewe hajafa, bali kazimia tu na kwamba mara nyingi huzimia kwa saa nyingi.

Dk Coster aliongeza kuwa ilibidi na wao wasiweke mwili kwenye jokofu na kuulaza kwenye machela kwa saa sita na ndipo wakaamua kuuweka kwenye droo za maiti, kwani ilikuwa wazi sasa kwamba asingeamka tena asilani.

Waganga hospitalini hapo wamekiri kuwa mwili wa marehemu uliletwa hospitalini hapo ukiwa umenyolewa upara, lakini ukiwa na mikwaruzo pamoja na uvimbe hususan maeneo ya mikono na kifua.

Baba mkubwa wa marehemu, Ally Kivuyo ambaye ndiye mlezi wa Lightness, alisema mume wa marehemu alimtaarifu juu ya kifo hicho na kuongeza; “Lakini baadaye nikaletewa taarifa nyingine kuwa Lightness kumbe alikufa wakati akifanyiwa maombi au vitu vingine, nyumbani kwa mtu anayeitwa ‘Nabii Rajabu,’ hapo basi ikabidi niwataarifu polisi ambao walikuja kumkamata mumewe pamoja na huyo anayejiita nabii au mtabiri.

Source: Habari Leo