Ijumaa, 17 Machi 2017

Jinsi ya Kuishi na Mwanamke Asikuloge au Kukupa Limbwata..!!!

                          

Nipo tena kwa Mara nyingine katika kubadilishana uzoefu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu mahusiano,kuna jambo limekuwa likiniumiza kichwa sana ni swala zima la kulogwa au kupewa limbwata na mwanamke.

Nidhahiri kabisa mambo haya katika jamii yetu yanafanyika kwa baadhi ya wanawake huwa wanawafanyia wanaume,na tatizo hilo limezidi kushamiri zaidi kutokana na ongezeko kubwa la waganga wa kienyeji.

Nimefanya research kwa baadhi ya waganga wameniambia wateja wao wakubwa ni wanawake na shida kubwa wanayokuwa wanahitaji ni kuolewa au kuwadhibiti wanaume zao.

Nami mekuja kugundua wanaume wengi huwa wanafanyiwa madawa ila wakati mwengine mungu huwalinda hawazuriki bila ya wao kujua na wanaume wengi ambao wapo katika hatari hiyo ni wale wenye kipato kidogo ambacho kinarizisha.

Sasa basi nimejaribu kutafuta prevention za ki psychology, ambanzo hazihusiani na mambo ya kishirikina ambazo zinaweza kukusaidia uepukane na janga hilo nimejaribu kutumia experience yangu ni kama zifuatazo:

Kwanza kabisa kama mwanaume unapoanza mahusiano ya kimapenzi na mwanamke unatakiwa umwambie mwanamke vitu ambavyo huvipendi na moja katika ya vitu ambavyo utamwambia hupendi ni mambo ya kishirikina na unatakiwa umsisitizie kwamba endapo kama wewe utagundua yeye anapenda mambo ya kwenda kwa waganga umwambie siku hiyo ndio itakuwa mwisho wa mapenzi yenu.

Jambo la pili ukiwa unaishi na mwanamke ndani usipende kula chakula peke yako hata kama umechelewa kurudi umerudi labda saa sita usiku mwambie mke wako mle wote chakula cause peke yako hujazoea kula au kama mna mtoto wenu ama ndugu wa mwanamke kula nae chakula.

Kwa kufanya hivyo mwanamke atajua hupendi kula peke yako na unampenda yeye na ndugu zake kumbe unalako moyoni unajilinda na limbwata,jambo la tatu pendelea kufanya ibada ukitaka kula na ukitaka kulala na mshirikishe mkeo katika ibada na wakati mwingine msomee maandiko ya vitabu vya mungu ambayo yanakataza ushirikina na adhabu zake watakazo zipata wanaofanya mambo hayo,mengine mnaweza mkaongezea.

Note:Mwanamke anaweza akawa sio mshirikina lakini akashawishiwa na marafiki zake akufanyie hivyo,kwa hiyo kama mwanaume ni bora ukachukua tahadhari mapema.

Kama Huwezi Kuachana Naye Usijaribu Kuchungulia Mawasiliano Yake....!!!


Kuna siku nilijifanya Mjuaji nikadukua mawasiliano ya mchepuko wangu niliyokutana nayo huko sasa ni hatari tupu, sms ya kwanza kuingia jamaa anampongeza kwa shughuli yao ya jana kuja huku whatsaap shughuli nzito nikajikuta naumwa ghafla pressure inanipanda mara nikaona dunia inazunguka mara nataka kuaga dunia ikabidi majirani zangu wafanye mawasiliano na mchepuko wangu maana walikuwa wanaufahamu ile unakuja home. baby jamani unaumwa nn? aiseeeh nikiuangalia homa inanizidia nikifikiria kuucha siwezi.............kilichoendelea.....................ila mpaka sasa nadunda nao course niliona bora tu nijikaze 

Vijana Tuache tabia ya kudukua mawasiliano ya tunaowapenda wakati jeuri za kuwaacha hatunazo, huo ni ushauri tu kama jasiri endelea kupanga mikakati ya kudukua mawasiliano ya mke au mchumba ako soon tu itabaki story

Alikiba Kuweka Muziki Wake Wasafi.com ni Sawa na Safari ya Mwezini..!!


Kwa takribani miaka mitatu sasa mafahari wawili wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo Flava Alikiba na Diamond Platinumz wamekuwa katika bifu zito sana, licha ya wao kujaribu kila siku kuukwepa ukweli huo. Hakuna kati yao ambaye amewahi kujitokeza hadharani na kukiri uhasama kati yao lakini ni wazi kuwa watu hawa hawapikiki chungu kimoja.

Mara kwa mara watu wa karibu wa Diamond wakiwemo watu walio kwenye management yake hususan, mameneja Sallam na Ricardo Momo, wamekuwa wakimtupia vijembe Alikiba. “Wao wakipost tembo, sisi tunapost show” na “waambie dada zao Kariakoo waje Ulaya” ni baadhi tu ya mistari ambayo Diamond amewahi kusikika akiimba ikiwa ni kuelekeza mashambulizi upande wa Alikiba na kambi yake.

Hivi karibuni Diamond akiwa kwenye Interview ya kipindi cha 360 cha Clouds FM, alikaririwa akisema kuwa hana tatizo na Alikiba, ni mtu anayeheshimiana naye na hata uongozi wake uko katika mazungumzo na uongozi wa Alikiba ili Kiba aweze kuuza nyimbo zake kwenye mtandao wa wasafidotcom ambao ni mradi mpya wa Diamond.

Baadaye usiku kupitia akaunti yake ya Instagram Alikiba aliandika caption zenye utata zilizotafsiriwa na mashabiki na wadau mbalimbali kuwa zimelenga kujibu maneno hayo ya Diamond Platnumz.

Wamarekani wana sera zao mbili ambazo wanazitumia sana katika kulifanya taifa lao kuendelea kuwa taifa kubwa duniani. Sera ya kwanza; njia pekee ya kumshinda adui ni kumfanya rafiki, ya pili; wamarekani hawahitaji rafiki dhati wala adui kweli, zaidi ni kutimiza interest zao.

Hivyo watakufanya rafiki ili wapate watakacho na utarudi kuwa adui wakishatimiza azma yao. Lakini Waingereza pia wanasema numbers don’t lie. Nimejaribu kufuatilia rekodi za nyuma za Alikiba katika mtandao wa mkito.com nikagundua kuwa Alikiba ni record breaker. Mwana iliweka rekodi, Chekecha Cheketua iliweka rekodi. Hata nyimbo ya Nisamehe aliyoshirikishwa na Barakah Da Prince pamoja na nyimbo ya Kajiandae aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz zimeingia kwenye Top 5 ya ngoma zilizopakuliwa zaidi kwenye mtandao wa Mkito mwaka 2016.

Kwa rekodu hizi ni dhahiri Diamond anahitaji amani na Alikiba kwasababu za kibiashara zaidi. Anatambua fan base aliyonayo Alikiba itabust zaidi mtandao wake, pesa atakayopata ni kubwa, pia number of visitors itaongezeka kwa kasi kwani kila mtu atataka kuamini ni kweli Ali yumo? Haikushangaza kuona editing kwenye mitandao ikionesha kua profile ya Alikiba ipo kwenye wasafidotcom.

Kwa hali ilivyo sioni na sidhani kama management ya Alikiba itaweza kukubali kuuza nyimbo kwenye mtandao wa Diamond. Kwanza wanajiamini sababu wameshauza kabla na kuweza kuweka baadhi ya rekodi kwenye mtandao wa Mkito. Pili kutoka kwa mfululizo wa mashambulizi ya maneno kutoka kwa Dimond na management yake kwenda kwa Alikiba itakuwa ni fedheha kubwa kwa mashabiki wa Ali kama Ali na uongozi wake utakubaliana na suala hili. Na ndio maana nasema sera za kimarekani za Dimond zimedunda kwa Alikiba

Mwanamitindo afariki dunia kwa kugongwa na treni



Mrembo wa miaka 19 aliyefahamika kwa jina la Fredzania Thompson amegongwa na treni wakati akipiga picha.

Fredzania alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha Blinn na alikuwa na ndoto za kuwa mwanamitindo mkubwa duniani. Mzazi wa mrembo huyo, Akamie Stevenson ameliambia shirika la habari la CNN, “Bila shaka hilo ndio jamba ambalo alilokuwa akilitaka kulifanya katika maisha yake. Ndiyo shughuli aliyoanza kuifanya siku aliyofariki dunia.”

Hata hivyo msemaji wa polisi wa Navasota, Justin Leeth amesema mpaka sasa hawajagundua tatizo lolote juu ya kifo hicho kama kilikuwa cha hila yoyote.

Lissu aachiwa kwa dhamana ya bondi ya Sh10m


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo (Ijumaa) imemuachia, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema)  kwa dhamana ya bondi ya Sh10 milioni.

Lissu amedhaminiwa na maelezo ya awali yatasomwa Aprili3, mwaka huu.

Leo asubuhi, Lissu alisomewa mashtaka matano na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi  likiwamo ya kutoa maneno  yenye nia ya kuhimiza hisia za kidini ambayo yangeweza kupelekea uhasama baina ya jamii za Watanzania.

Lissu  ambaye anajiwakilisha yeye mwenyewe mahakamani hapo aliomba maelezo hayo ya awali yasomwe Jumatatu, ili aweze kuhudhuria uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unaotarajia kufanyika kesho.

Baada ya Video Inayodhaniwa ni ya Mwanae Kusambaa Ikimuonyesha Akifanya Mapenzi na Jibaba,Kajala Afunguka Haya Mapya..!!!1


Muigizaji wa Filamu Tanzania Kajala Masanja amewafungukia wanaomsema kwamba ameshindwa kumlea binti yake ' Paula'  na kusema anatamani awaoneshe watu hao malezi anayompatia binti yake huyo.

Akipiga story na eNewz, Kajala amedai kuwa hawezi kushindwa kumlea mtoto wake na kwamba malezi anayompatia binti yake ni tofauti na yale watu wanayoyazungumzia katika mitandao ya kijamii na kuongeza kuwa binti huyo analelewa katika maadili, yanayotakiwa.

"Sijashindwa kumlea mtoto wangu, natamani wangekuwa wanaona malezi ninayompatia Paula kwani kila wanachokiona na kukisikia kwenye mitandao ni tofauti sana na ninavyomlea". Kajala alisema.

Kajala ameongeza kwamba katika jambo linalomuumiza ni watu kutumia jina la binti yake hyo na kujifanya ni  yeye na wakati mwingine kuweka vitu hasi ambavyo vinamfanya mtoto wake achukuliwe tofauti katika jamii.

Aidha  muigizaji huyo ameongeza kuwa serikali inapaswa kushughulikia matatizo yanayotolewa na watumiaji wa mitandao  kwa umakini wa hali ya juu  ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu ya kutosha.

“Ile akaunti siyo ya Paula kwanza, kwani hajawai  kuwa na simu au kumiliki, nimeshawahi  kuwaambia wamiliki wa ukurasa huo wabadilishe jina au waandike ni ‘fanpage’ lakini naona wamegoma , Baba  yake naye amejaribu kuzifunga lakini bado zinaendelea kutumika mpaka sasa nimechoka ila bado hatujajua tuchukue hatua gani". Kajala aliongeza.

Paula ambaye ni mtoto wa muigizaji huyo pamoja na Producer P- Funky Majani aliwahi kukutwa na mkasa wa kufananishwa na binti aliyerekodiwa akiwa mtupu na kusambazwa mitandaoni.

Fahamu Maajabu ya Nanasi Ambayo Yatakuacha Kinywa Wazi..!!!



BAADHI ya watu wamekuwa wakidai tunda la nanasi kuwa siyo salama kwa akina mama wajawazito, ingawa suala hili bado halijathibitishwa kitaalamu, kwani wapo wanaokula na haijawahi kuripotiwa madhara. Linatumika kama tunda ama juisi na lina faida mbalimbali kwa afya ya mwanadamu.

BAADHI YA FAIDA HIZO NI PAMOJA NA:

Lina vitamini A, B na C, madini ya chuma, calcium, copper na phosphorous ambayo yote ni muhimu sana katika afya ya mwanadamu.Tunda hili husaidia kutengeneza damu, kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles).

Hutibu matatizo ya tumbo, bandama na ini, husaidia kusafisha utumbo mwembamba, hutibu homa, vidonda mdomoni, magonjwa ya koo, hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu, hutibu kikohozi, kutetemeka na uoga (Anxiety). Leo nimeandika tiba ya nanasi kwa sababu ni mjadala mkubwa ulioibuka kuwa tunda hili lina madhara, lakini nikuhakikishie msomaji hakuna madhara ya kukufanya

Laurence Masha Ajitoa Kugombea Urais TLS, Amuunga Mkono Tundu Lissu


Mgombea Urais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) Ndg. Laurence Masha amejitoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa hoja kuwa anaamini uwezo wa Lissu katika kuiongoza TLS.

Amewaomba mawakili wote waliopanga kumpigia kura wampigie Tundu Lissu. 

ARUSHA: Mgombea urais wa TLS, Laurence Masha ametangaza kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho na kudai anamuunga mkono Tundu Lissu 

Ndoto za Mbwana Samatta Kucheza na Mau United Zawekwa Pending


Ndoto za mshambuliaji wa timu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mtanzania Mbwana Samatta za kukanyaga katika dimba la Old Trafford la Manchester United zimesubirishwa baada ya matokeo ya droo ya robo fainali kombe la Europa kwenda kinyume na matamanio yake.

Hamu ya Nahodha huyo wa Taifa Stars ilikuwa ni kuona timu yake ya Genk inapangwa kukutana na Man United katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, ili atimize ndoto yake mojawapo ya kucheza katika uwanja wa huo maarufu na uliotoa mastaa wengi duniani.

Samatta baada ya mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ambao timu yake iliibuka na ushindi wa 5-2 na kutoa nafasi kubwa ya kufuzu robo fainali, alinukuliwa akisema "Moja kati ya ndoto zangu ni kukanyaga katika dimba la Old Trafford, kwahiyo naomba kila siku timu yetu ikivuka, ipangwe na Manchester United"

Hata hivyo, katika droo iliyochezeshwa leo, KRC Genk imepangwa kuanzia nchini Hispania dhidi ya Celta Vigo, na mchezo wa marudiano utapigwa nchini Ubelgiji.

Ili timu hiyo ikutane na Man United msimu huu, inapaswa kwanza kuitoa Celta Vigo, huku ikiomba Man UNited pia ifuzu nusu fainali, halafu droo iwakutanishe.

Kutokana na ukweli kwamba timu ya Man United ndiyo yenye mashabiki wengi zaidi duniani, ingeweza kuwa ni fursa adhimu kwa Samatta kujitangaza zaidi, kwa kuwa watu wengi hawapitwi kutazama mchezo wowote unaoihusu timu hiyo iliyo chii ya kocha Jose Mourinho.