Jumatatu, 8 Septemba 2014

Kilichoikuta Taifa Stars kwenye mechi dhidi ya Burundi hiki hapa

stars-1Timu ya taifa ya Tanzania leo ilikuwa jijini Bujumbura Burundi kukupiga na timu ya taifa ya nchi hiyo kwenye mchezo wa kirafiki.
Taifa Stars leo hii imeambulia kipigo cha mabao 2-0 katika mechi yake ya kirafiki iliyomalizika hivi punde mjini Bujumbura.
Hii ni mara ya pili Stars inafungwa na Warundi hao ambao ndani ya mwezi mmoja tu na ushee, waliifunga Stars mabao 3-0 jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo ya leo , Burundi ilipata mabao yote katika kipindi cha kwanza.
Bao la kwanza lilifungwa na Saido Ntibazonkiza katika dakika ya kwanza tu.

Bao la pili lilifungwa na Yusuf Ndikumana ‘Lule’ katika dakika ya 29.

Dr. Hamisi Kigwangalla atangaza nia ya kugombea Urais 2015, zisome hapa points zake.

 
 September 7 2014 Dr. Hamisi ambae ni mbunge wa Nzega kwa ruhusa ya CCM alikutana na Waandishi Dar es salaam akiwa ameongozana na mke wake pamoja na watoto wao na kisha kuweka wazi kwamba yuko tayari kugombea kiti cha Urais kwa tiketi ya CCM 2015.
Yafuatayo ndio ameyasema:
  1. ‘Leo nitasema neno zito kidogo, litabadilisha sura ya historia yangu milele… kinachotokea hapa kina maana kubwa sana kwa watu wenye historia inayofanana na mimi, wale ambao wameyajua maisha ya shida na kukosa uhakika toka wakiwa tumboni mwa wazazi kutokana na hali za uchumi wa familia zao’
  2. ‘Nimeyajua maisha ya mtu mnyonge na masikini kwa kuyaishi na sio kwa kusoma ama kusikia, ninajua mtu akiongelea njaa anamaanisha nini’
3.’Watanzania wanataka kupata huduma bora za afya, elimu, maji, miundombinu…… ukienda kwa Wafanyabiashara wakubwa pale Pugu viwandani ama kwa Matabibu wenzangu hospitali ya taifa Muhimbili au kwa Wafanyabiashara pale sokoni Kariakoo wote watakwambia hawapendi kuona kodi zao zikitafunwa na wachache wasio waadilifu’
HK 16
4.’Watu hawatarajii serikali itabeba mizigo yao yote lakini wanaamini kabisa kwamba tukibadili vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali na uchumi wetu, tunaweza kwa kiasi kikubwa kubadili mwelekeo mzima wa maisha ya baadae na kuiondoa Tanzania miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani’
  1. ‘Na mimi kama Watanzania wenzangu wengi nina imani kubwa kabisa kwamba tunaweza kubadili mustakabali wa taifa letu, kufungua milango ya maisha bora zaidi kwa Watanzania, tutatoa fursa sawa kwa kila Mtanzania kuishi kwa matumaini kwamba atabadili maisha yake wakati wowote ule kuanzia leo, tutaweza kuamsha ari ya kila Mtanzania kuongeza bidii kwenye kazi’
  • ‘Ninaamini kabisa kutokea ndani ya mifupa yangu kuwa tukifanya uchaguzi sahihi wa vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha uchumi wetu na serikali yetu……. haya ninayoyasema sio ndoto za mchana’
  • h13 
    Baada ya kuyazungumza yake ya moyoni baadhi ya Waandishi walipata nafasi ya kumuuliza maswali ambapo hili lilikua mojawapo >>> ‘Umetangaza nia kwamba unagombea Urais lakini sijasikia unapitia chama gani au utasimama binafsi?……… na kama ni chama, mpaka sasa hakuna chama chochote ambacho kimefungua milango kwa Wanachama wake kutangaza nia, kwa kufanya hivyo huwezi kuona unakiuka taratibu za chama?
    JIBU: ‘Nitapitia chama cha mapinduzi, sijawahi kuwa Mwanachama wa chama chochote kile cha siasa zaidi ya CCM na sijawa na fikra za kubadili chama, natangaza nia ya kugombea Urais kupitia chama changu cha CCM, hii ya kwamba sasa hivi ni mapema mno kutangaza nia kwa sababu vyama havijafungua milango ya watu kutangaza nia, sio kweli…. watu wameweka nia za kuutaka Urais toka mwaka 1995 lakini pia kuweka nia sio kufanya kampeni, kinachokatazwa ni kuanza kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni kutangazwa’ – Dr. Hamisi Kigwangalla
    ‘Nimeamua kuweka wazi nia yangu, sitaki ule unafiki wa kujificha chini ya kivuli cha Ooooh!!….. nimeshauriwa, nimeombwa, nasubiri kuota, mimi ni mkweli na nimetia nia ya dhati kwamba nataka Urais’ – Dr. Kigwangalla
    h15 
    ‘Vipaumbele vyangu kama napata fursa ya kuwa Rais ni kuboresha huduma za jamii kama maji, afya, elimu… kipaumbele cha pili ni kujenga na kuimarisha miundombinu kama barabara, ndege, reli na bandari…….. kipaumbele cha tatu ni utawala bora, nchi haiwezi kuongozwa bila kuwa na utawala wa sheria yani kila mtu apate haki yake bila kudhulumiwa ‘ – Dr. Kigwangalla
    h14
    h9
    h8
    h5
    h2
    h3
    h1
    Dr. Hamis akilishwa keki yenye ramani ya Tanzania na mke wake kumalizia shughuli hii ya kutangaza nia.

    Picha 16 za ajali nyingine ya Basi Dodoma leo, alikuwemo pia meneja wa Dr. Cheni

    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.50 PM
    Aliekuwemo kwenye hili basi ndio amenitumia hizi picha na kuniambia watu wasiozidi watano wamefariki dunia wengine zaidi kujeruhiwa baada ya basi lao kuanguka Mkange Berega.
    Basi linaitwa Air Bus na limepata ajali likielekea Dodoma kutokea Morogo na ni baada ya kifaa cha usukani kushindwa kufanya kazi ambapo muda mfupi baadae anasema alisikia tu dereva akipiga kelele na kisha kikafata kishindo, basi likaacha njia na kwenda bondeni.
    youngluvega.blogspot.com inaendelea kufatilia ili kupata taarifa kamili ili kujua idadi ya vifo na majeruhi pamoja na taarifa nyingine ambapo ajali hii imetokea siku tatu baada ya Waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe kufungia kampuni mbili za mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yaliyogongana na kuua 39 Musoma.
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.59 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.28.08 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.28.16 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.39 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.32 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.24 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.17 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.09 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.27.02 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.26.52 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.26.41 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.26.33 PM
    Huyu mama ana watoto Mapacha, hapa alikua analia baada ya kushindwa kumuona mtoto wake mwingine.
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.28.27 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.28.16 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 2.28.08 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 3.29.59 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 3.30.06 PM
    Screen Shot 2014-09-08 at 3.30.22 PM 
    Na mtayarishaji wako Nickson Luvega.

    BAADA YA OKWI KUIDHINISHWA SIMBA, HIKI NDIO WALICHOAMUA YANGU

    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe (kulia) akimtambulisha mshambuliaji Emmanuel Okwi kurejea katika klabu hiyo jijini Dar es Salaam jana. Picha: Halima Kambi 
    Siku moja baada ya shirikisho la soka nchini TFF kumtangaza mchezaji Emmanuel Okwi kuwa huru na hivyo anaweza kusajiliwa na klabu ya Simba – leo hii uongozi wa klabu ya Yanga umeitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuzungumza juu ya uamuzi wa keshi yao dhidi ya Okwi.
    Uongozi wa Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji  kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.
    Mwenyekiti wa Kamati  ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
    Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.
    Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
    “Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
    Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.
    Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslah