Jumanne, 3 Machi 2015

Waziri MEMBE amesema huu ni mchango wa Marehemu Kapteni KOMBA kwenye mgogoro wa Ziwa Nyasa

IMG_0231 
Leo ni siku ambayo mwili wa Marehemu Kapteni John Damian Komba umepumzishwa katika makaburi ya Kijijini kwao Lituhi, Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Leo kwenye kipindi cha Power Breakfast Clouds FM, alisikika Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumzia mchango wa Marehemu Komba kwenye suala la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi.
Kwenye mgogoro wetu wa Malawi tulimchukua Kapteni Komba kwenda kutoa ushuhuda unaoonyesha kwamba Ziwa Nyasa kwa kweli mpaka ni katikati, ndio alikwenda kutoa ushuhuda.. Kapteni Komba alieleza kwamba toka enzi za mababu zake na mabibi zake makaburi ya wazee wake yako ndani ya maji, ukifika pale Lituhi na huwa wanachukua mitumbwi wanakwenda kunyunyizia na kutoa baraka zao makaburi yale yako ndani ya maji na bado yapo misalaba iko kule kwa hiyo akawa anauliza na yale makaburi sasa yawe mali ya Malawi?
Maji ya Ziwa Nyasa yanakuja kwenye ardhi miaka yote na huchukua Shule, huchukua Mahakama na makaburi ya wazee mbalimbali, huu ni ushuhuda alioutoa Kapteni Komba tulipokwenda Malawi na ushuhuda uliochukuliwa na wasuluhishi kuonyesha kwamba Ziwa lile linakula ardhi ya Tanzania.
Komba lilimleta hilo na alizungumza vizuri sana kwa hiyo katika diplomasia ya mgogoro wa Ziwa Nyasa kati yetu na Malawi huyu alikuwa miongoni mwa watu waliozungumza kwa niaba ya watu wanaokaa kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa kwamba mpaka kwa kweli upo pale katikati
Aliwahi kualikwa kwenda kusaidia kampeni kwa nyimbo zake, kwa hamasa zake na wengine waliogopa wakimuona ameingia kwenye nchi, wanatuletea barua kutuambia bwana muondoeni haraka sana.. akikupigia kampeni kushindwa haiwezekani.. tumepoteza mtu, tumepoteza shujaa, tumepoteza mkereketwa, tumepoteza kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele kukiletea chama cha mapinduzi ushindi miaka nenda rudi“– Waziri Bernard Membe.

Jumapili, 1 Machi 2015

Nimekuwekea matokeo ya EPL hapa, yakiwemo ya Man UTD vs Sunderland

(null)
Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha katika ligi kuu ya England tangu kuanza kwa mwaka 2015, klabu ya Manchester United leo iliwakaribisha kwenye uwanja wao wa nyumbani Sunderland.
Mchezo huo wa raundi ya pili ya EPL, umemalizika muda mfupi na kikosi cha Louis van Gaal kimepata ushindi wa magoli 2-0.
Wayne Rooney alifunga magoli yote mawili na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi hiyo kufunga magoli zaidi ya 10 katika misimu 11 mfululizo.
Matokeo mengine kwenye ligi hiyo yapo kama inavyoonekana kwenye picha:
(null)

Alichofanya Kapteni Komba kwa familia yake siku mbili kabla ya kifo chake

capt Komba 
Kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kapteni John Komba ambaye amefariki dunia akiwa hospital ya TMJ February 28 kilitanguliwa na kitu ambacho kinadhaniwa kama kilikua ni ishara ya siku yake ya mwisho.
Claudia John Komba ambaye ni mtoto wa 9 kati ya watoto 11 wa marehemu John Komba ameongea na youngluvega.blogspot.com na kuelezea baadhi ya vitu ambavyo kwao imekua kama kauli ya mwisho kutoka kwa Baba yao ambayo aliitoa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.
Claudia amesema >>>‘Taarifa ilinifikia mida ya saa 9 akasema anajisikia vibaya ambapo wakati yupo njiani akawa anaweweseka sana, tulipofika TMJ hospital walipofanya vipimo walisema ameshafariki’
youngluvega.blogspot.com Kabla ya hapo kulikua na ripoti ya mzee kuugua?
Claudia John Komba: ‘Zilikuwepo baba alikua amekaa ilikua mida ya asubuhi akawa analalamika anajisikia vibaya tukampeleka hospitali, tukagundua sukari imepanda sana na presha imepanda sana, akatolewa akawa anaendelea vizuri’
‘Juzi tarehe 26 february ilikua siku yangu ya kuzaliwa, akaita watoto wote akasema nataka kufanya birthday sababu birthday nyingi huwa zinanipita nakua nipo nje, akatukusanya watoto wote, aliongea maneno ya mwisho akatusihi watoto tupendane tusiweke  matabaka kwamba huyu mdogo huyu mkubwa alisema yeye hana mkataba na Mungu’.

Maneno ya Thiery Henry kuhusu ndoto za kumrithi Arsene Wenger

Arsenal's Captain, Frenchman Thierry Hen 
Mchezaji mkongwe wa Arsenal, Thiery Henry amefichua kuwa ndoto yake kuu ni kumrithi kocha wa timu hiyo Arsene Wenger katika klabu hiyo.
Mchezaji huyo wa zamani ambaye ndiye anayeongoza kwa idadi ya mabao katika klabu hiyo akiwa na magoli 228, aliripotiwa kupewa nafasi ya kuanza kufundisha soka katika chuo cha ukufunzi wa soka katika klabu  hiyo mapema mwezi huu.
Raia huyo wa ufaransa amekiri kwamba ana mipango ya kumrithi Wenger wakati kocha huyo atakapoamua kustaafu.
Sijui ni kwa muda ganiWenger anataka kuendelea kuwa kocha wa Arsenal, lakini ni sharti niwe mzoefu wa kutosha kuchukua wadhifa huo,kuwa kocha wa Arsenal ni ndoto yangu kubwa,lakini nafaa kujifunza mwanzo,hicho ndicho kitu muhimu,”-Thiery

Hizi ni picha za Miss CBE 2015 jinsi ilivyofana Dar es Salaam…

.
Chuo cha usimamizi wa Fedha CBE usiku wa Feb 28, 2015 walikua wakimtafuta Miss CBE ambaye kwao ni kama kumtafuta mwakilishi wao ambaye atakwenda kuwawakilisha kwenye ngazi zinazofuata za mashindani haya ya urembo.
Ambapo katika mashindano hayo ya kutafuta mlimbwende mshiriki (12), Neema Sissamo aliibuka kuwa Miss CBE 2015 huku nafasi ya pili (2) ikachukuliwa na Namie Haule, nafasi ya tatu ikachukuliwa na Mariam Omary .
Hapa kuna picha mbalimbali zikiwemo za Jux na Young wakitumbuiza kwenye usiku huo wa kumtafuta Miss CBE 2015.