Ijumaa, 13 Novemba 2015

Soma Story ya Kusikitisha ya Huyu Dada, Mume Wake Anamlazimisha Kufanya Mapenzi ya Watu Watatu na Amegundua Kuwa ni Shoga Pia


Kutoka Instagram:

MMH DUNIA HII INA MAMBO KWAKWEL.COZZ LEO NIKO KI EMOTION ZAID EMBU NGOJA NI SHARE NA NYIE BAADHI YA STORY NAZO POKEA INBOX...kuna dada nilikuwa naongeaga nae ila kutokana na sababu zangu nisingependa mtaja jina...naomba nikuletee Story yake ya kusikitisha Hapa Chini:
.
Masta hata ukinipost kweny wall yako mungu nishaidi ila tangu nimekujua umekuwa mkarimu sana kwangu ndio maana leo hii nimeamua kukufungukia ili unisaodie tu kimawazo maana kadri siku zinavyo zidi kwenda ndivyo nazid changanyikiwa...

Kama nilivyo kwambia nimeolewa huu mwaka wa 3 mimi na mume wang tumejuana huu unaenda mwaka wa 5,masta ilianza kama utan baada nilipo jifungua mtoto wang wa kwanza alipo fikisha miez 8 skumoja mume wng alinitamkia habar ya ku invite 3 person in our bedroom nilijua utani so tukajibizana na alipoona sikupenda idea akaanza jichekesha na kusema he was joking yakaisha...ila baada ya miez kadhaa aliirudia hii mada tena ila this time alijipanga na kuni Converse sana yan alinipa darasa la uwakika nikajikuta nakubali,masta kesho yake kwel akaja na mdada mashallah mpaka nyumban chumban kwangu kikatokea cha kutokea ila baada ya hapo nilijiona mjinga sana nililia siku nzima but nilikuwa dhaifu cz usiku wake baby akanileta pochi jipya la prada nikaridhika...

Mchezo ulikuwa ni huo kwa takriban kama miez 6 nahis nilijikuta nazoea mpa nilipo jikuta nina mimba, for his respect mwenyewe alinitamkia kuwa we need to stop..ila skumoja rafiki yake alikuja home amelewa na walikuwa wamegombana baada ya kutapeliana na alianza kumcharukia huku akimwita GAY sikutilia maanan cz nilijua ni mikwaruzano tu na pombe masta baada ya kujifungua mtoto wangu wa 2 in 6 month ananitamkia tena huo mchezo this time nilikuwa mkali coz tayari mtoto wang wa 1 alishaanza kuongea na sikutaka kaone huo ujinga pili habari zilikuwa zinasambaa kuwa mimi na mume wang tunahuo mchezo..basi Masta nyumba ikaanza waka moto kila siku kelele iskumoja alinitamkia kuwa either i like it or not ataendelea kufanya coz hiyo ndio furaha yake...

Wakat nimerudi Tanzania kwaajiri ya holiday siku ya kurudi marekan tulichelewa ndege Transit na coz hatukuwa na simu ya mawasiliano mimi na wanangu tulirudi home kwa kumshtukia baada ya kuingia ndani nilimkuta mume wangu akifanya mapenzi na watu wawili mmoja alikuwa mwanamke yule wa mwanzo ambae alimleta first time mwengine mwanaume, that was the most painful thing nimewahi shuudia Masta nilihisi moyo umestop nilianguka chini huku nikiwa nimembabe mtoto wangu mdogo kifuani...nimekuja stuka niko hospital.

Kinacho niuma zaidi dada yangu baada ya kutoka hospital nilikuwa tayari kumsamehe mume wangu kama angeliniomba msamah lakini haikuwa hivyo baada ya Two Montn ananiambia nichague moja NIENDELEE KUWA NA YEYE NA NIKUBALI MATAKWA YAKE YA KUINGIZA WATU NDANI AU TUACHANE...Masta nilikosa jibU na kujikuta natoa machozi aliniambia kuwa ananipa muda nijifikilie lakini sasa masta maneno ya watu kusema kuwa ni gay yalikuwa ya kizidi ila sababu sikuwa na uelewa mzuri wa haya mambo nilikuwa nikibisha coz mume wang alikuwa na uwezo wa kunibebesha mimba...mpaka siku nyingine tena nilimfumania kweny gari lake akiwa na mwanaume mwenzie wakifanya uchafu wao...

Dadangu roho inaniuma na siku nyingi sana nilikuwa natafuta njia ya kutoa hili dukuduku moyon coz sijawah muelezea mtu masta naogopa walimwengu watanicheka coz always huwa wananisema naringa na kujifanya kuwa nina pesa kisa navaa vitu vya gharama...baada ya hilo tukia mume wangu kwa mdomo wake alinitamkia kuwa yeye anai enjoy kufanya mapenz na wanaume pamoja na wanawake at the same time so kama mke anataka nimsapoti...hivi navyo kwambia atanaka divorce kisa nimekataa kukubaliana na yeye na kuhusu watoto he doesnt seems to care masta wanangu bado wadogo na wakiume wameshazoea kila siku daddy daddy daddy coz ana waspoil mume ananambia nikiachana nae hataki kujua anything about me na watoto atakuwa anatuma tu pesa...shida sio pesa masta NISAIDIE NIFANYE NINI NAHISI NAKUWA KICHAA SOON...naogopa kuwaadisia ndugu na rafiki zangu Masta
.
.
MWISHO...DUH EMBU TUMSAIDIE HUYU DADA KIMAWAZO

Maalim Seif azugumza na Balozi wa EU na viongozi wa UKAWA....Atoa Msimamo Mzito

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea kauli yake ya kutotambua kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao cha mashauriano na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Maalim Seif amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bw Jecha Salim Jecha hana mamlaka ya kufuta uchaguzi huo, na kinachohitajika na kuendelea na mchakato wa kuhakiki kura zilizobakia na mshindi kutangazwa.

Kuhusu tamko lililotolewa na serikali juu ya kufutwa rasmi kwa uchaguzi huo kupitia tangazo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali tarehe sita mwezi huu, Maalim Seif amesema tamko hilo limekosa uhalali tangu lilipotolewa na Mwenyekiti wa ZEC.

Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF amesema Chama chake hakijalizingatia tamko hilo na wala hakijadili uwezekano wa kurejewa kwa uchaguzi huo, kwa madai kuwa uchaguzi ulikamilika bila ya kuwepo malalamiko kutoka chama chochote cha siasa na wala Tume ya Uchaguzi.

Mapema akizungumza baada ya kikao hicho cha mashauriano, aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa amesema kikao hicho kilichojadili Mkwamo wa kisiasa Zanzibar kimekwenda vizuri.

Hata hivyo amesema ufafanuzi zaidi utatolewa Jumapili ijayo ambapo viongozi hao wanakusudia kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kikao hicho Maalim Seif alifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Filberto Seregondi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuelezea hatua zinazochukuliwa kukwamua mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Balozi Seregondi ambaye anamaliza muda wake wa utumishi hapa nchini,aliambatana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Tanzania kutoka Umoja huo.

Maskini..Lowassa Asalimu Amri Kwa Polisi...Atoa Ujumbe Huu Hapa Kwa Wafuasi Wote wa Ukawa Kuhusu Mkutano Wake

Maskini..Lowassa Asalimu Amri Kwa Polisi Kuhusu Mkutano aliokuwa aufanye kuongea na Wananchi...Atoa Ujumbe Huu Hapa Kwa Wafuasi Wote wa Ukawa Kuhusu Mkutano Wake

Watanzania Wasiwekeze Kila Kitu Kwa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu

Mbwana Samatta (kushoto) pamoja na Thomas Ulimwengu (kulia)

Stars inatoka katika kambi ya wiki moja na siku kadhaa nchini Afrika Kusini itawakabili ‘Mbweha wa Jangwani’ baada ya kufuzu hatua ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1 dhidi ya Malawi mwezi uliopita.

Kwa mara ya kwanza Stars itaingia uwanjani kucheza na timu bora zaidi Afrika ikiwa na mfungaji bora wa ligi ya mabingwa Afrika, namzungumzia kijana wa miaka 22, Mbwana Samatta.

Sina shaka kuhusu uwezo wa Samatta ambaye nilimshuhudia Jumapili iliyopita akiipa ubingwa wa Afrika upande wa vilabu timu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Sitazungumzia sana mechi yenyewe lakini ningependa kuwaambia Watanzania wenzangu kuwa hatupaswi kuamini moja kwa moja katika uwezo wa mchezaji mmoja au wawili katika timu na ili kuishinda Algeria wachezaji wote kuanzia kwa golikipa hadi mchezaji wa mwisho katika safu ya ushambuliaji wanapaswa kucheza katika kiwango cha kufanana.

Samatta anazungukwa na nahodha wa timu ya taifa ya Zambia ambayo Jumatano hii iliifunga Sudan 1-0 jijini, Khartoom. Namzungumzia kiungo mshambuliaji Rainford Kalaba, pembeni ya Samatta pale TP Mazembe anacheza na mchezaji pekee wa timu ya Taifa ya Ivory Coast anayecheza barani Afrika, Roger Assale, Mghana, Solomon Asante, n.k

Kiujumla, Samatta anazungukwa na ‘rundo’ la wachezaji wenye vipaji ambao wanajituma sana ndani ya uwanja kwa muda wote wa mchezo. Huduma ambayo ‘Samagoal’ amekuwa akiitoa klabuni kwake ni tofauti kidogo na ile ambayo Watanzania wamekuwa wakitaraji kutoka kwa mchezaji huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji 10 bora wanaocheza ndani ya Afrika kwa mwaka huu wa 2015.

Kwa nini Samatta wa TP Mazembe ni tofauti na huyu anayeichezea Stars? Ubora wake ni uleule, tofauti ni kwamba, akiwa TP anakutana na wachezaji wenye vipaji kama yeye ambao pia hucheza kwa nidhamu, kujituma na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

Mafanikio ya Samatta na ‘patna’ wake Thomas Ulimwengu ndani ya klabu yao wiki iliyopita ni ya ‘mfanowe’. Ni wachezaji wa kwanza wa Kitanzania kucheza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Afrika. Katika michezo miwili ya fainali kati ya TP Mazembe na USM Algers ya Algeria, Samatta amefanikiwa kufunga magoli mawili kati ya manne ya TP na kutengeneza goli lingine moja.

Ushindi wao wa taji la mabingwa Afrika umewafanya Watanzania wengi kujenga imani kwamba, Stars inaweza kuishinda na kuitoa Algeria! Kila kitu kinawezekana katika mchezo wa soka, lakini ukitazama aina ya wapinzani ambao tunakwenda kucheza nao ni sawa na ‘mlima mrefu’ ambo tunapaswa kuupandaa.

Ulimwengu anacheza kwa kupambana sana akiwa klabuni kwake TP Mazembe na amekuwa akicheza hivyo hivyo hadi timu ya Taifa Stars. Lakini Samatta anahitaji ‘muunganiko’, anahitaji wachezaji wenzake wacheze kwa asilimia ya juu. Anahitaji wachezaji ambao wana uwezo wa kuusoma mchezo. Kila Mtanzania ukimuuliza hivi sasa kwanini anaamini Stars itashinda dhidi ya Algeria anakwambia “Mbwana Samatta”.

Lakini mchezo wa mpira wa miguu si kama mchezo wa ngumi au tenis, mtu anapambana mwenyewe. Akiwa mzuri anapata matokeo. Lakini mchezo wa mpira wa miguu unahitaji sana uwezo wa kiuchezaji wa mchezaji mwingine. Ukitaka kuuona uwezo halisi wa Samatta katika timu ya Taifa ni lazima, Shomari Kapombe, Nadir Haroub, Kelvin Yondan, Ally Mustapha wote wacheze inavyotakiwa katika idara zao.

Timu ambayo Samatta aliifunga magoli mawili katika fainali ya CAF Champions league haina hata mchezaji mmoja katika timu ya Taifa ya Algeria! Inamaanisha kuwa wanategemea zaidi mkusanyiko wa wachezaji wao wanaofanya vizuri barani Ulaya. Algeria ina wachezaji wanaofanya vizuri katika ligi kuu England, Hispania, Ureno na kwingineko.

Algeria wamekuja na ‘timu kabambe’, Rais M’Bolhi (Antalyaspor/Uturuki), Azzedine Doukha (JS Kabylie), Malik Asselah (CR Belouizdad). Viungo: Mehdi Zeffane (Rennes/Ufaransa), Mohamed Khoutir Ziti (JS Kabylie), Faouzi Ghoulam (Napoli/Italia), Djamel Mesbah (Sampdoria/Italia), Carl Medjani (Trabzonspor/Uturuki),Aïssa Mandi (Reims/Ufaransa), ukweli itakuwa mechi ngumu kwa Stars kuliko Algeria.