Jumapili, 6 Julai 2014
Hii ndio idadi ya waliokufa baada ya mji wa Lamu Kenya kukumbwa na mashambulizi ya risasi.
Wizara ya mambo ya ndani Kenya imesema kuwa zaidi ya watu 29 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makazi ya Pwani ya nchi hiyo karibu na mpaka wa Somalia.
Watu 20 waliuawa katika eneo la Gamba kaunti ya Tanariver huku tisa wengine wakipoteza maisha kufuatia mashambulizi ya kufyatuliana risasi katika kituo kimoja cha kibiashara kaunti ya lamu karibu na mpaka wa Somali.
Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo ambapo inadaiwa watu walikuwa wakiangalia mechi za kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Mashuhuda wanasema watu kadhaa wenye silaha walifika katika kituo cha biashara katika eneo la Hindi jimbo la Lamu, mapema siku ya jumamosi jioni na kuanza kufyatua risasi za moto.
Mashambulizi katika eneo Lamu mapema mwezi uliopita yalisababisha vifo vya watu 60, wakati wanamgambo wa al shaabab wakivamia hoteli na vituo vya polisi. Na mleta habari wako Nickson Luvega.
Degree ya heshima ya udaktari aliyopewa mwanamuziki Oliver Mtukudzi.
Mwanamziki mkongwe wa kimataifa nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ametunukiwa tuzo ya tatu iliyobeba heshima ya udaktari kutokana na kuwa mshauri na balozi mzuri wa muziki.
Mwaka 2003 alitunukiwa tuzo kubwa ya heshima na chuo kikuu cha Zimbabwe kwa kutambua miongo kadhaa ya mchango wake na kujitolea katika kujenga muziki na msukumo wasanii wa kizazi kipya nchini Zimbabwe huku akionyesha ushawishi kwenye kazi za wasanii hao.
Oliver Mtukudzi ni mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Zimbabwe ambaye amevuma sana na kuvuka mipaka kutokana na nyimbo zake zinazohamasisha amani na kutoa burudani barani Afrika ambapo amekua akitumika kama alama katika taifa hilo haswa kwa upande wa sanaa ya nchini Zimbabwe. Na mimi mletaji wako mahiri Nickon Luvega.