Ijumaa, 3 Oktoba 2014

MICROSOFT YAZINDUA WINDOWS 10


Kampuni ya Microsoft imezindua programu mpya ya Windows 10 ambayo imeipiku Windows 9.
Kampuni hiyo pia inatarajia wateja wake watarudi kwani wengi walikuwa wakisitasita kuboresha oparesheni zao tangu Windows 8.
Windows 10 itaingiliana na vifaa vingi hususan kutokana na uwezo wake wa kubadilisha ukubwa wa programu yake.

Usafiri wa treni kuboresha uchumi TZ?

Haba na Haba inaangazia hali ya usafiri wa treni nchini Tanzania. Kwa kuwa mwelekeo uliopo katika sekta ya uchukuzi kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mizigo mizito na mingi inayosafirishwa umbali mrefu inatumia usafiri wa reli. Je uboreshwaji wa usafiri wa treni unawezaje kuboresha uchumi na maisha ya mtanzania?

Picha 3 za jinsi Waziri mkuu wa Uganda alivyonyang’anywa ulinzi nyumbani baada ya kutimuliwa kazi.

ug1 
Jana ndio Waziri mkuu mpya wa Uganda Ruhakana Rugunda kaapishwa ila kabla yake alikua ni Amama Mbabazi ambae alifutwa kazi wiki kadhaa zilizopita baada ya kukaa madarakani toka May 2011 akitokea kwenye Uwaziri wa Ulinzi.
September 18 2014 ndio Rais Museveni alimuandikia Spika wa bunge barua kumuarifu kuwa ameamua kumuondoa waziri mkuu huyo na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekua Waziri wa Afya ambae kwa sasa ana umri wa miaka 67.
ug2 
Kwa mujibu wa ripota wa TZA (youngluvega.blogspot.com ) waziri huyu alietimuliwa alikua Waziri mkuu wa nne toka Rais Museveni aanze kuitawala nchi hiyo January 1986 ambapo mpaka sasa amewahi kuwa na Makamu wa Rais wanaofikia wanne.
Picha zote hizi zinaonyesha wakati Serikali ya Uganda ilipomnyang’anya ulinzi wa Wanajeshi waziri huyu mkuu baada ya kufutwa kazi ambapo kwenye hii picha ya chini anaeonekana ni mke wake akilalamika kwa kutoamini kilichotokea kwani mume wake na Rais Museveni wamekua marafiki wakubwa.
Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba kuna mambo mengi yaliyosababisha kufutwa kazi kwa waziri huyu mkuu lakini mambo hayo hayajawekwa wazi.
ug3
Nyuma hii unayoiona ni nyumba anayoishi na inayomilikiwa na Waziri huyu mkuu aliefutwa kazi.

Kinshasa:Chimbuko la virusi vya HIV

Kinshasa mwaka 1955, janga la HIV lilikuwa linatesa mjini humu na kote nchini DRC hasa mkoa wa Katanga 
Ugonjwa wa ukimwi uligunduliwa miaka ya 1920 mjini Kinshasa, nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo. Wanasayansi wameeleza.
Wanasayansi wa kimataifa wanasema ongezeko la watu,vitendo vya kukutana kimwili na shughuli za usafirishaji kwa njia ya reli zilifanya virusi vya ukimwi kuenea.
Ripoti inasema kuwa biashara ya ngono, ongezeko kubwa la watu na vitu vyenye ncha kali kama sindano kwenye zahanati huenda kulichangia kusambaa kwa ugonjwa huo DRC.
Wakati huo huo reli ilikuwa ina watu takriban milioni moja waliokuwa wakiingia na kutoka kwa wingi jijini Kinshasa kwa mwaka,wakisambaza virusi kwenda kwenye miji mingine.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.
 
Inaarifiwa virusi vya HIV ni sawa na virusi vya Sinium vinavyopatikana katika Sokwe  
Ukimwi ulitambulika kuwa janga kimataifa mwaka 1980 na uliathiri takriban watu milioni 75.
Ugonjwa huu una historia ndefu barani Afrika , lakini ulipotokea ugonjwa huu bado ni mjadala mrefu.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Oxford na chuo cha Leuven, nchini ubelgiji walitafiti chanzo cha ugonjwa wa ukimwi wakisema kuwa ulianzia kwa Sokwe.
Virusi vya HIV ni sawa na virusi vinavyopatikana kwa Sokwe ambavyo vinajulilkana kama Simian ambavyo vinadhaniwa vilitoka kwa Sokwe na kuambukizwa binadamu kupitia kwa damu wakati wakitafuta nyama ya wanyamapori.
Virusi hivyo vilikuwa na muundo tofauti na muundo huo ulikuwa unabadilika kila wakati. Virusi vya kwanza viliwaathiri maelfu ya watu nchini Cameroon.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.

Vurusi vya HIV 

Idadi kubwa ya wanaume waliokuwa wanafanya kazi mijini na idadi ya wanaume ndio ilikuwa kubwa kuliko wanawake na hivyo biashara ya ngono ikawa kubwa sana.
Mmoja wa watafiti Profesa Pybus anasema kuwa mambo mawili yanesaidia kupunguza maambukizi. Kwanza hamasisho la serikali kuwatibu wagonjwa kwa maradhi tegemezi.
Jambo la pili ingekuwa mfumo wa usafiri ambao uliwawezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine huku ugonjwa ukienezwa zaidi.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi vielendelera kuenezwa kwa nchi jirani ya Brazzaville na mkoa wenye madini wa Katanga ambao ulikuwa kitovu cha ugonjwa huo.
Virusi havikukomea tu nchini Congo bali vilianza kuenezwa kote duniani

Picha za palikofanyika birthday party ya Diamond… kabla watu hawajaingia

D 2 
Party ilifanyika Golden Jubilee Towers Dar es salaam ambapo kama hujaona pichaz za kilivyohappen unaweza kuchek post iliyotangulia kabla ya hii kwenye hii siku kubwa ya Diamond aliyotimiza miaka 25 ya kuzaliwa.
D 3
D 4
Screen Shot 2014-10-03 at 12.28.18 PM
Screen Shot 2014-10-03 at 12.28.11 PM
d 5

Mambo 10 aliyoyasema Madee kuhusu ishu yake ya kuwekwa Polisi.

Screen Shot 2014-10-03 at 12.07.41 PM 
Madee alikamatwa na Polisi saa kadhaa zilizopita baada ya tukio la yeye kuibiwa simu akiwa kwenye gari tena likitembea ambapo waliohusika ni watu wawili wakiwa kwenye pikipiki saa tisa usiku akitoka Kigamboni Dar es alaam kufanya show hivyo akawa anavuka bahari ili aelekee nyumbani.
Baada ya kuchoropoa hiyo simu jamaa wa pikipiki walianza kukimbia hivyo na dereva wa Madee akaanza kukimbizana nao na kufanikiwa kuwagonga alafu pikipiki ikaanguka ila jamaa wa nyuma aliechoropoa simu akafanikiwa kukimbia ila yule aliekua anaendesha wakambeba na kwenda nae maskani Tiptop kwa lengo la kumuhoji ili wampate aliekimbia na simu.
Madee 1
Hii ni wakati Madee alipofatwa na kukamatwa na Polisi mtaani kuhusu hii kesi, aliandikwa kwenye page yake ya insta ‘hivi niliua au niliibiwa simu?’ (picha imepigwa na globalpublishers.info)
Kilichomfanya Madee akamatwe na kuwekwa Polisi ni madai yake kwamba kesi hiyo imegeuzwa na sasa yeye ndio anaonekana mwenye makosa kwa kumteka huyu jamaa waliekwenda nae Tiptop Manzese.
Haya ndio mambo 10 anayoyasema Madee.
1. Nilikaa Polisi kwa zaidi ya saa 32, nililala na kuamkia huko.
2. Kule ndani haupo huru ndio maana kuna mateso, unapangiwa muda wa kulala na hautakiwi kuongea kwa sauti kubwa… mle ndani watu wanatolewa njee saa moja usiku tunahesabiwa pale nje alafu mkishaingizwa ndani kimyaaaa.
3. Kwenye room niliyoshikiliwa nilikua na watu kama 30 hivi ila sijui kwenye room nyigine ya pili sijui kulikua na watu wangapi sababu sikuingia.
4. Nilianza kushangiliwa nilipotokeza tu pale kwa juu wakati naingizwa machizi waliponiona mimi wakaanza kuimba ule wimbo wangu wa ‘majuto ni mjukuu‘ niliozungumzia ishu za Polisi.
5. Nilivyofika kule nilikuta kumejaa ila kumbe kuna sehemu tayari nilishawekewa na machizi sehemu poa tu upepo unaingia fresh tu sema ndio hivyo mazoea mazoea tu huwezi kulala….
Hii picha Madee aliipiga na kuiweka instagram muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana na kuandika 'Am Freeeeeee' akimaanisha yuko huru
Hii picha Madee aliipiga na kuiweka instagram muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana na kuandika ‘Am Freeeeeee’ akimaanisha yuko huru
6. Mle ndani hakuna vitanda zaidi ya sakafu tu nilitamani hata nijaribu kupeleka maombi niwapelekee machizi mikeka kidogo wawe wanalalia.
7. Nilisimamishwa Mahakamani September 25 kwa mara ya kwanza sababu jamaa wamejaribu kutengeneza vitu vingine viwili tofauti na ilivyokua, wanasema mimi nimemteka mtu na pikipiki yake nikaenda kumjeruhi na washkaji zangu ila ukweli ni kwamba huyu jamaa alikua na rafiki yake kwenye pikipiki wakanipora simu yangu wakati nikiwa nimekaa kwenye gari.
8. Baada ya hapo dereva wangu mtundu akakimbia akaiblock pikipiki na kuigonga wakaanguka lakini yule aliekua amechukua simu akakimbia ila aliekua anaendesha tukamkamata tukampakiza kwenye gari na kuondoka nae mpaka maskani ya Tiptop ila nikampigia simu mama yake nikamwambia mwanao yuko hapa njoo uongee nae aturudishie simu yetu.
9. Mama yake alikuja akaondoka na kusema anakwenda kumtafuta aliechukua simu lakini cha kushangaza Mama asubuhi akaja na Polisi wakamchukua jamaa na kumpeleka Magomeni wakati huo mi nilikua nimekwenda Mwanza kwenye show.
10. Niliporudi kutoka Mwanza nikakimbilia Polisi Magomeni kwenda kuulizia napataje haki yangu nikaambiwa hili shauri linahamishiwa Kigamboni, nilipokwenda Kigamboni Polisi nikakuta hiyo kesi kwamba Madee kamteka mtu nikawekwa ndani, hii ni kama mara yangu ya nne au ya tatu nawekwa Polisi…. hizo nyingine zilishatokea zamani ambapo ya mwisho ilikua miaka sita au saba nyuma, hii kesi ya sasa ipo Mahakamani.

USAJILI WA KUDUMU FALCAO MANCHESTER UNITED HABARI KAMILI HII HAPA

1412288001100_wps_42_Manchester_United_4_v_QPRWakati mkataba wake wa mkopo ukiwa umebakisha miezi nane kuisha, usajili Radamel Falcao kwenda Manchester United umechukua nafasi kwenye vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza ni kwamba Man United imekubaliana rasmi mahitaji binafsi na mchezaji huyo kwa ajili ya kukamilisha usajili wa kudumu wa mchezaji huyo wa Colombia.
Taarifa zinaeleza kwamba Man United wanafanya jitihada zote kumaliza suala la usajili wa Falcao ili kuepuka kila kilichotokea miaka mitano iliyopita katika usajili wa Carlos Tevez.
United walimsajili Falcao kwa mkopo kutoka Monaco siku ya mwisho ya usajili wa wakati wa kiangazi.
Wakiwa tayari wameshalipa ada ya mkopo wa £6million kwa klabu ya Ufaransa, United pia walishakubaliana kimsingi na Monaco kuwalipa kiasi cha £43.5m ikiwa wataamua kumchukua Falcao kiujumla mwishoni mwa msimu.
Leo sasa imeripotiwa kwamba mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward tayari amekubaliana na wawakilishi wa Falcao kumlipa mshahara wa £250,000 kwa wiki mchezaji huyo pamoja, bonasi na haki za taswira yake.
Manchester United pia imekanusha taarifa kwamba itakatisha mkataba wa mkopo wa Falcao ikiwa mchezaji huyo ataumia tena goti.

HII NI KUHUSU WANAJESHI KUPIGANA NA POLISI TARIME JUZI, WANGAPI WAMEUMIA? KISA?

Risasi 
Hii ni taarifa kutoka Tarime mkoani Mara ambako watu 12 wamejeruhiwa wakati wa mashambulizi ya kurushiana risasi kati ya askari wa JWTZ kituo cha Nyandoto na polisi wa kituo cha stendi.
Kwa mujibu wa magazeti ya Nipashe na Mwanachi leo, hii ishu ilitokea wakati Wanajeshi hao walipokua wakijaribu kumchukua Mwanajeshi mwenzao aliyekamwatwa na polisi hao kwa kosa la kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia (Helmet).
Mashambuliazi hayo ya kurushiana risasi na kupigana ngumi na mateke yalitokea juzi jioni katika kituo hicho cha stendi ambapo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Tarime alithibitisha kupokea majeruhi 12 na kati yao wawili ni askari wa JWTZ, Polisi saba na raia watatu.
Kamanda wa Polisi Tarime alisema Mwanajeshi huyo licha ya kukiuka taratibu za barabarani aliwatolea lugha za matusi polisi hao jambo lililowalazimu kumkamata kwa nguvu na wanajeshi wenzake kuingilia kati na kusababisha vurugu.
Alisema Wanajeshi watatu ambao hawakutajwa majina wameshikiliwa na polisi kwa kuvunja utaratibu wa usalama huku Mkuu wa Wilaya hiyo John Henjewele akilaani kitendo hicho cha kurushiana risasi za moto hewani na kusema ni cha utovu wa nidhamu na kilikwamisha shughuli za watu kwa muda sababu ya kuhofia usalama wao.