Ijumaa, 16 Machi 2018

Huu Hapa Ukweli Mchungu Kwa Wadada Wanaolalamika Hawana Bahati za Kuolewa....

Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini? Wanawake wanadhani wana bahati mbaya?

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi WA kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.

Kweli huenda we ni mtoto WA kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja..anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anaeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!

Una mpuuza Na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambae ni baba fulani na ni mume WA Fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda toka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?

Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?

DADA maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa Leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna MTU aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika...Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.

Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa. Mwaka WA ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo ?

Related Posts:

  • Van Gaal:tuna mlinzi wa kati mmoja tu  Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal. Kocha wa machester United, Louis van Gaal amesema Manchester united ina mlinzi wa kati mmoja tu mwenye uzoefu wakati huu kikosi hicho kinapotarajia kukipiga na west ham kat… Read More
  • Hukumu ya muuguzi aliesababisha kifo cha mjamzito mwaka 2009.  Kwenye moja kati ya taarifa kubwa za Kenya September 25 2014 ni pamoja na hii ya Muuguzi mmoja ambae kesi yake ilianza kusikilizwa toka mwaka 2009 nchini humo kwenye kaunti ya Kyambuu. Kituo cha Radio Jambo kimerip… Read More
  • Waaga mchuano baada ya kuagizwa kuvua hijab Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa kikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia. Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa vikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia yanayofanyika huko Korea Kus… Read More
  • 'VIPIMO VYA SKETI KIGEZO CHA SARATANI'  Baadhi ya watafiti wana sahuku ikiwa vipimo vya sketi vitamtahadharisha mwanamke kuhusu tisho la Saratani. Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupa… Read More
  • KILICHOWAKUTA CHADEMA WALIOANDAMANA MWANZA Sept.25   Kutoka 88.1 Mwanza ambapo Polisi wamekamata viongozi sita na wafuasi kadhaa wa (CHADEMA) waliokuwa wakijiandaa kuandamana baada ya kukaidi amri ya polisi kusitisha maandamano. Ni September 25 saa 5.40 asubu… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni