Jumamosi, 13 Septemba 2014

MFUNGWA AKUTWA NA SIMU MWILINI

 Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ya Kenya imekuwa kero kubwa kwa maafisa wa magereza. Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza kukuweka katika hali ya kufa kupona. Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. ...

Shearer asema Welbeck atang'ara Arsenal

 Mshambuliaji wa Arsenal Danny Wellbeck kushoto  Mshambuliaji mpya wa kilabu ya Arsenal Danny Welbeck anaweza kufunga mabao 25 kwa msimu mmoja ,hayo ni matamshi ya aliyekuwa mshambuliaji wa England Allan Shearer. Wellbeck mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na kikosi cha The Gunners kutoka kilabu ya Manchester United kwa kitita...

WAATHIRIWA WA MABOMU MBAGALA WALALAMIKA

Nyumba iliyoharibiwa na bomu kama inavyoonekana. Mkutano kati ya waandishi habari na Waathirika wa Mabomu Mbagala, ambao umefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mbagala Kuu ,jijini Dar-Es-Salaam mapema leo . Waathirika hao wapatao 1,361 kati yao 25 wameishapoteza maisha kutokana na athari za mabomu hayo. Mlipuko huo wa mabomu ni tukio lililotokea tarehe 29 April...

Alichokiandika Steve Nyerere kuhusu kujiuzulu uongozi Bongo Movie.

  Kupitia mtandao wa picha yaani Instagram aliyekuwa Rais wa Bongo Movie Unity,Steve Nyerere  leo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwenye klabu hiyo ya Bongo Movie huku akishindwa kuweka sababu iliyomfanya kujiuzulu.   Katika maelezo yake chini ya picha yake ameandika>>’Napenda kuwashukuru ndugu zangu wote wasanii wenzangu kaka zangu mama zangu...

MAMA MZAZI WA NEY WA MITEGO AMTILIA SHAKA MWANAE

  Mama mzazi wa mkali wa bongofleva Nay wa Mitego ameongea kwa mara ya kwanza na millardayo.com na kusema ana wasiwasi na mwanae ambae hivi karibuni ametoa video mpya aliyoifanya nchini Kenya. Amekiri kweli kwamba siku kadhaa zilizopita ilibidi amwite na kumuweka chini Nay wa Mitego akitaka amueleze kama ni kweli amejiunga na ‘freemason’ ambayo wengi wanaitafsiri...

EPL: Matokeo ya Man City vs Arsenal haya hapa

Baada ya mapumziko ya takribani siku 14, hatimaye ligi kuu ya England imerejea tena leo kwa mchezo mkali kati ya Man City dhidi ya washika bunduki Arsenal. Mchezo uliopigwa kwenye dimba la Emirates ulikuwa mkali na wa kusisimua kwa timu zote zikipoteza nafasi kadhaa za ushindi. Matokeo ya mwisho ya mchezo yalikuwa sare ya 2-2. Sergio Aguero alianza kuifungia City katika...

EPL: Matokeo ya Chelsea vs Swansea City

Mchaka mchaka wa ligi kuu ya England umeendelea tena jioni hii kwa mchezo uliowakutanisha vilabu viwili vilivyokuwa vikishika nafasi ya kwanza na ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya England – Chelsea dhidi ya Swansea. Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la nyumbani la Chelsea Stamford Bridge umeisha kwa ushindi wa 4-2 kwa vijana wa Jose Mourinho. Swansea walikuwa wa...

La Liga: Matokeo ya FC Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao

Ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa – FC Barcelona waliikaribisha Athletic Bilbao kwenye dimba la Nou Camp. Mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita umeisha kwa matokeo ya ushindi wa 2-0 kwa FC Barcelona. Akiwa anahitaji magoli mawili tu kufikisha jumla ya magoli 400 katika maisha yake ya soka, Lionel Messi alishindwa...

EPL: Kilichoikuta Liverpool dhidi ya Aston Villa hiki hapa EPL: Kilichoikuta Liverpool dhidi ya Aston Villa hiki hapa

Kwa mara ya nne mfululizo klabu ya Liverpool imekuwa ikikosa matokeo chanya kwenye uwanja wa nyumbani wa Anfield kila inapocheza na kikosi cha Paul Lambert – Aston Villa. Leo hii wakiwa nyumbani Liverpool huku ikiwachezesha kwa mara ya kwanza Mario Balotelli na Adam Lallana ndani ya Anfield, kikosi cha Brendan Rogers kimepoteza mechi ya pili ya msimu baada ya kukubali...