Wahenga walinena kuwa “penzi ni kikohozi kulificha hauwezi” hakika wazee wetu hawakukosea Mapenzi ni hisia ambazo huwezi kuzizuia kwa namna yeyote ile kwani huanza kwa siri baina ya wawili lakini baadaye huwa sio siri tena, vivyo hivyo kwa mwanamke anayekupenda kwa dhati huwa na tabia hizi;
1. Utaona mabadiliko katika muonekano wake. Ukitaka kumfahamu msichana ambaye yupo katika mapenzi kama alikuwa hajipendi kwa maana kuwa rafu hata akiwa katika mazingira ya nyumbani basi katika kipindi hiki atakuwa msafi kuanzia mwili mavazi na hata nywele ataweka kila staili itakayompendeza ili kukuvutia.
2. Anajali kama mwanamke anakupenda atakujali hatopenda kuwa mbali na wewe kama atagundua upo katika tatizo, atakufanya ufahamu yupo kwa ajili yako pale utakapomhitaji.
3. Anajitoa kwa ajili yako. Atachukua muda wake mwingi kuwa na wewe atafanya vitu ambavyo unavipenda na kuviacha vya kwake pale inapobidi
4. Huwa muwazi kwa kila anachokifanya nini anapanga kufanya na nani anakutana naye kwa wakati gani.
5. Wewe ni mvulana pekee anayetazamia uje kuwa mume wake anazungumzia mambo mengi kuhusu maisha ya baadaye kama vile ndoa watoto wangapi atatamani kuzaa pamoja na familia yenu iwe vipi.
6. Anapenda kuwa na wewe muda mwingi. Msichana mwenye mapenzi hufanya haraka kumaliza shughuli zake ili asipoteze muda mwingi akashindwa kukuona tena kwa siku hiyo. Anaweza kuacha hata shughuli zake ili aje kukaa na wewe hata kama mkutano wenu hauna maana na faida kwake.
7. Anakushika kwa hisia, msichana aliyezama katika mapenzi huwa na hisia ndio maana hupenda kukushika kila sehemu yako ya mwili kwa hisia za kweli akihitaji na wewe uhisi anachohisi kupitia mguso wake.
8. Atakutambulisha kwa ndugu jamaa na rafiki zake
, hupenda kila mtu wake wa karibu akufahamu hivyo hupenda kukutambulisha kwa kila mtu haoni aibu kufanya hivyo kwa kuwa anatarajia utakuwa wake wa kudumu.
Jumapili, 1 Mei 2016
Home »
» DALILI ZA MWANAMKE ANAYEKUPENDA KUTOKA MOYONI
DALILI ZA MWANAMKE ANAYEKUPENDA KUTOKA MOYONI
Related Posts:
Aliyejifungua Watoto 3 Anaomba Asaidiwe kwani naye ni Mgonjwa wa Pumu MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia k… Read More
Waziri Makamba Awasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianavyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali. Kau… Read More
Wasafi Wadaiwa Kumpora Producer Frag Ngoma ya 'Bado' iliyoibwa na Harmonize Feat. Diamond Producer Frag kutoka Uptown Music ametumbua jipu baada ya kuibuka na kusema kuwa yeye ndiye aliyetengeneza wimbo wa Bado wa Harmonize na Diamond. Frag aliiambia Enewz kuwa pamoja na kazi kubwa aliyoifanya kuhakikisha ngoma… Read More
Donald Trump Asema Uchina “inaibaka” MarekaniMgombea mkuu wa chama cha Republican Donald Trump ameshutumu Uchina na kusema imekuwa “ikiibaka” Marekani kupitia sera zake za kibiashara. Ameambia watu waliohudhuria mkutano wa kisiasa Indiana kwamba Uchina imekuwa ikitekele… Read More
Baada ya Kutoka Marekani Mtoto Getrude Clement Akaribishwa Bungeni LeoGetrude Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali Hivi … Read More
0 comments:
Chapisha Maoni