Jumanne, 23 Septemba 2014

Msikiti uliozua utata wafungwa A.Kusini

Bwana Taj Hargey anasema msikiti huo unawalenga watu wenye mawazo chanya 

Msikiti ambao unasemekana kuunga mkono watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, na ambao pia wanawake wataruhusiwa kuswali ndani,umefungwa.
Afisaa mmoja mjini Cape Town, anasema kuwa msikiti huo umevunja sheria za baraza la jiji kwa kukosa nafasi za kuegesha magari ya waumini.
Msikiti huo, ulifunguliwa rasmi siku ya Ijumaa wiki jana licha ya kukosolewa na waumini wa kiisilamu katika eneo uliko.
Mwanzilishi wa msikiti huo, Taj Hargey, alisema kuwa msikiti huo utasaidia katika kupambana na kuenezwa kwa itikadi kali za kidini.
''Tunafungua msikiti huu kwa watu walio na muonekano chanya kwa baadhi ya mambo wala sio wenye muonekano finyu,'' alisema bwana Hergey kabla ya ufunguzi wa masikiti huo.
Kadhalika bwana Hargey alikana kwenda kinyume na mafunzo ya dini ya kiisilamu.
Maafisa wa baraza la jiji wamekanusha madai kuwa kufungwa kwa msikiti huo ni kwa nia mbaya.
 Msikiti huu umefungwa kutokana na kukosa nafasi za kuegeshea magari
"swala hili linazua sana hisia, baadhi ya maafisa wa baraza la jiji, ambao ni waisilamu wangeteka kuunga mkono kufungwa kwa msikiti huo, lakini wasio waisilamu wangependa kuuona ukiwa wazi, lakini cha muhimu hapa ni kwamba, tungetaka kuona sheria ikifuatwa, '' alisema afisa mmoja wa baraza la jiji.
Inaarifiwa kuwa bwana Hargey hakuomba idhini ya kuruhusu jengo lililokuwa likitumiwa kama sehemu ya kuweka vitu kubadilishwa na kuwa msikiti.
Kuambatana na masharti ya baraza la jiji, kila sehemu ya maombi inapaswa kuwa na sehemu ya kuegeshea magari ya waumini lakini msikiti huo hauna sehemu hiyo.
Shughuli ya kuwasilisha maombo ya kuwezesha kuwepo sehemu ya kuegeshea magari huenda ikachukua hadi miezi sita.
Bwana Hargey aliambia BBC kwamba anaamini kuwa kila kitu kiko shwari.
Wanawake wataruhusiwa kuswali pamoja na wanaume na hata kuongoza maombi.

Ebola:Watu kusalia nyumbani S:Leone

Serikali iansema ikiwa juhudi z akupambana na Ebola zitashuka, madhara yatakuwa makubwa zaidi 

Rais wa Sierra Leone amesema kuwa serikali inatafakari kutangaza awamu ya pili ya amri ya kutotoka nje kote nchini ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola.
Rais Ernest Bai Koroma, amesema kuwa kwa sasa ameridhika na mafanikio yaliyotokana na kuwazuia watu kutoka nje kwa saa 72 .
Awamu ya kwanza ya amri hiyo ilimalizika Jumapili.
Alisema kuwa maafisa wakuu walizuru zaidi ya nyumba milioni moja na kuwapata watu wengi ambao walikuwa wameathiriwa na ugonjwa huo.
Pia walipata mili ya watu waliokuwa wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani limesema kuwa hadi pale hatua zaidi zitakapochukuliwa kukabiliana na janga la Ebola, visa vya maambukizi huenda vikaongezeka.

Visa vya mapenzi haviishi…. huyu wa Dodoma kamuua mke kwa rungu, chanzo?

Screen Shot 2014-09-23 at 8.05.41 AM 
Siku hizi mapenzi yamekua kama karata hivyo kila mmoja anacheza ajuavyo au awezavyo kwenye huu uwanja mpana ambao kwa kiasi kikubwa miaka inavyosogea ndio vifo vingi hutokea kutokana tu na visa vya mapenzi.
Taarifa kutoka Dodoma na kuthibitishwa na Polisi, zinahusu Wananchi kupatwa na hasira na kumuua Mwanaume aliyemuua mke wake kwa kumpiga na rungu tumboni kwenye kijiji cha Mzogole.
Mwanamke aliyeuwawa ana umri wa miaka 48 Mwajuma Chomola na mume wake ambae ndio mtuhumiwa ana umri wa miaka 55 anaitwa Richard Kodi ambapo kwa mujibu wa gazeti la HabariLEO, Mwanaume huyu alifariki dunia wakati akihudumiwa hospitali ya wilaya ya Mpwapwa.
Wakati uchunguzi ukiendelea, matokeo ya awali yanaonyesha chanzo cha yeye kumuua mke wake waliekua wakiishi pamoja ni wivu wa kimapenzi na kwamba ishu ilianzia pale Mwanamke alipochelewa kurudi nyumbani akitokea kwenye sherehe iliyofanyika kwenye kijiji hichohicho wanachoishi lakini mume alidhani mke kaenda kwengine.
Yaani sio kwamba alimfumania bali alihisi tu mke wake kaenda kwengine ndio sababu iliyomfanya akachukua haya maamuzi, mara nyingi kwenye mapenzi kumekua na kesi nyingi zinazosababisha Wanawake kupigwa au kuuwawa kwa sababu tu Mwanaume anahisi vitu kama hivi bila kuwa na ushahidi.

Safari za Treni Tanzania kuongezeka.

Screen Shot 2014-09-23 at 9.43.10 AM 
Dr. Harryson Mwakyembe ni miongoni mwa Mawaziri ambao wanazungumziwa sana na vijana pamoja na Watanzania wengine kwenye marika mbalimbali kutokana na jinsi anavyochapa mzigo ndio maana sio ajabu hata kumsikia akitajwa kwenye nyimbo za Wakali wa bongofleva.
Kwenye Exclusive na millardayo.com Waziri Mwakyembe amethibitisha kwamba itafikia time Tanzania usafiri wa Treni utakua bora na wengi watakimbilia huko kutokana na mabadiliko yanayofanyika.
Anasema ‘Usafiri wa Treni umeanza kuimarika na baada ya muda sio mrefu tutaanza kufanya safari nne au tano kwenda Kigoma na Mwanza, watu watapanda Treni

Huyu ndio msanii staa wa kimataifa anaekuja Fiesta Dar 2014.


Screen Shot 2014-09-23 at 3.40.20 PM 
Wakati Tour ya Fiesta ikiwa inazunguka kwenye mikoa mbalimbali Tanzania ambapo weekend hii ni Mbeya na Songea, ametangazwa msanii wa kimataifa ambae ni rasmi atapanda kwenye stage ya Fiesta Dar es salaam October 2014 Leaders Club Kinondoni.
Rapper T.I ndio msanii wa kimataifa kwenye stage ya Fiesta October 18 2014 akiwa ni mkali ambae kwa sasa anamiliki chati za muziki kwa single yake ya No Mediocre