Jumamosi, 23 Mei 2015

IRELAND YAFANYA MAAMUZI KUHUSIANA NA NDOA ZA JINSIA MOJA

wapiga kura wajitokeza kwa wingi nchini Ireland ili kuamua kuhusu kuhalalishwa kwa ndoa za watu wa jinsia moja. Wapiga kura wengi wameripotiwa kujitokeza kwenye kura ya maoni nchini Ireland ya kuamua iwapo ndoa za watu wa jinsia moja zinaweza kuhalalishwa . Katika sehemu nyingine ukiwemo mji mkuu Dublin na miji mingine, idadi ya wapiga ilitarajiwa kufikia takriban asilimia...

ZAIDI YA WATU 40 WAUAWA MEXICO

Polisi nchini Mexico Takriban watu 43 wameuawa wakati wa ufyatulianaji wa risasi katika jimbo la Michoacan nchini mexico kati ya vikosi vya usalama na genge moja lenye silaha. Mapigano hayo yalianza wakati magari ya polisi yalipofyatuliwa risasi kwenye barabara moja kuu katika kijiji kilicho karibu na mpaka na jimbo la Jalisco. Moja ya megenge hatari zaidi ya madawa...

REAL MADRID YAWASILIANA NA BENITEZ

Rafael Benitez Mkufunzi wa kilabu ya Napoli Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa makocha wataokumrithi Carlo Ancelotti katika kilabu ya Real Madrid. Ancelotti anatarajiwa na wengi kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi hii. Mazungumzo kati ya Real Madrid na Benitez yanaendelea huku kandarasi ya Benitez katika kilabu ya Napoli ikitarajiwa...

DAVID LUIZ:'NIMEWAHI KUSHIRIKI NGONO'

David Luiz kushoto  Mlinzi wa klabu ya Paris St-Germain David Luiz amevishtumu vyombo vya habari kwa kukosa heshima baada ya kukanusha madai kwamba yeye hajawahi kushiriki katika tendo la ngono. Ripoti hizo zilianza kusambaa baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28 kusema katika instagram kwamba yeye na mpenziwe ''wako tayari kungojea''. Aliiambia...

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye #TuzozaWatu2015.. Pichaz na list yote ya washindi iko hapa

 Kilichosubiriwa kwa hamu na watu wengi ni tukio zima la Tuzo za Watu ambapo fainali yake ilikuwa jana MAY 22 2015.. Kutokana na utaratibu uliowekwa washiriki wote waliteuliwa na watu na baadae mchakato ukakamilika kwa kuwapigia kura washiriki hao. Yes.. jana usiku shughuli yote ilikuwa pale Hyatt Regency, hapa nina baadhi ya PICHAZ ambazo nimekuwekea pamoja...