Jumatatu, 2 Mei 2016

Baada ya Kutoka Marekani Mtoto Getrude Clement Akaribishwa Bungeni Leo

Getrude Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali
Hivi karibuni Getrude alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika New York Marekani ambapo leo Bungeni amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude amesema kuwa amefarijika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini makubaliano ya Paris.
Katika kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrude amewaasa vijana hasa wanafunzi kusimamia suala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwanafunzi huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.


Waziri Makamba Awasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.


Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianavyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Makamba amesema kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa mifuko ya plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali inayosababisha athari kubwa katika mazingira.
“Asilimia kubwa kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.
Akiwasilisha hotuba yake, Waziri Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa wala kuingizwa.
Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.
Waziri Makamba amesema kuwa kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na kupewa Na. 29.


Donald Trump Asema Uchina “inaibaka” Marekani

Mgombea mkuu wa chama cha Republican Donald Trump ameshutumu Uchina na kusema imekuwa “ikiibaka” Marekani kupitia sera zake za kibiashara.
Ameambia watu waliohudhuria mkutano wa kisiasa Indiana kwamba Uchina imekuwa ikitekeleza “wizi mkubwa zaidi kuwani kutekelezwa katika historia ya dunia.”
Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, amekuwa akiituhumu Uchina kwa kuchezea sarafu yake ili kuwa na ushindani wa kibiashara duniani inapouza bidhaa nje ya nchi.
Hilo, amesema, limeathiri sana wafanyabiashara na wafanyakazi wa Marekani.
“Hatuwezi kuruhusu Uchina iendelee kuibaka nchi yetu, na hilo ndilo tunafanya (kwa wakati huu),” alisema mkutanoni Jumapili.
"Tutabadilisha mambo, na tuna uwezo, msisahau. Tuna nguvu sana dhidi ya Uchina.”
Katika manifesto yake ya kampeni, Bw Trump ameahidi kufanikisha mkataba bora wa kibiashara baina ya Uchina na Marekani ambao utawezesha “wafanyabiashara na wafanyakazi kutoka Marekani kuweza kushindana”.
Obama: Trump haelewi sera za kigeni
Ametaja malengo manne ambayo yanahusisha kutangaza Uchina kuwa taifa linalochezea sarafu yake na kusitisha utoaji wa nafuu za wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya nchi ambazo anasema ni haramu.
Aidha, anaitaka Uchina kufikisha kikomo mfumo duni wa masharti ya leba na uhifadhi wa mazingira.
Takwimu za karibuni zaidi kutoka kwa serikali ya Marekani zinaonesha pengo la kibiashara baina ya Uchina na Marekani lilipanda na kufikia $365.7bn (£250.1bn) mwaka jana. Kufikia Februari mwaka huu, pengo hilo lilikuwa limefika $57bn tayari.
Hii ni mara ya kwanza kwa Trump kutumia neno “ubakaji” akizungumzia biashara na Uchina, lakini amejulikana kwa kutumia maneno makali kwenye kampeni yake.
Alikabiliwa na mamia ya waandamanaji jimbo la California Ijumaa kabla yake kutoa hotuba katika mkutano wa chama cha Republican Ijumaa.
Alilazimika kutumia mlango wa nyuma kuingia.
Waziri mkuu wa Uchina Li Keqiang amesema Wachina wanafuatilia kwa karibu uchaguzi nchini Marekani.
Hata hivyo anasema wengi wanamtazama Bw Trump kama mtu wa kuenziwa badala ya adui.


DAYNA NYANGE AITAMANI NDOA

Biblia Takatifu kitabu cha Mathayo 19:3 unasema “Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, kwa hiyo wao si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe.”
Ndoa ni moja ya heshima kubwa hapa duniani ambayo kila binadamu hutamani kupata heshima hiyo kwani imeelezwa katika Vitabu vya Dini kuwa ndoa ni moja ya nusu ya matendo yako kama utatekeleza vile inavyopaswa, je uko tayari kuoa au kuoelewa? Dayna Nyange anahaya ya kusema.
Mkali huyo wa “Natamani” ameongea kupitia XXL ya Clouds Fm Kipengele cha 255 cha Perfect Chrispin, Nyange anatamani kuwa katika maisha ya ndoa lakini mara nyingi ndoa huwa chungu.
KWANINI CHUNGU?
Dayna ameeleza kuwa unaweza kuingia katika ndoa lakini usifikie yale uliyoyaazimia haswa kutokana na uminifu kuwa mdogo miongoni mwa wapendanao .
“Kuingia moja kwa moja katika ndoa inahitajika ujipange kwanza japo nahitaji lakini maisha yaliyopo ndani ya ndoa ndio huwa magumu tumshirikishe Mungu wakati tunapotaka kuoa au kuolewa ama katika kukaribia suala la ndoa” amesema Dayna Nyange


RAIS KABILA AMFUKUZA KAZI WAZIRI ALIYEPIGA PUNYETO OFISINI

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila amemfukuza kazi Naibu Waziri wa Posta na Mawasiliano, Enock Sebineza kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kuvuja kwa video mitandaoni ikimuonesha akijichua nyeti zake akiwa ofisini.
Taarifa iliyotolewa na Televisheni ya Taifa nchini humo (RTNC) imemnukuu Rais Kabila akisema Waziri Ruberangabo ameliaibisha taifa kutokana na kitendo alichokifanya katika ofisi ya umma bila woga.
Wananchi wa Kongo wamemtaka Waziri huyo ajiuzulu baada ya video hiyo kusambaa mitandaoni tangu mwishoni mwa wiki ikimuonesha waziri huyo akijichua ofisini kwake licha ya uwepo wa bendera ya nchi hiyo na picha ya Rais Kabila.


RANIERI KUIKOSA MECHI YA CHELSEA NA TOTTENHAM

Boss wa Leicester City Claudio Ranieri anauwezekano mkubwa asiangalie mechi ya Chelsea na Tottenham hii leo kwa sababu atakuwa ndani ya ndege kutoka Italia.
Mbweha hao weupe kutoka Kings Power watachukua ubingwa Premier League kama Tottenham itashindwa kuifunga Chelsea ugenini Stamford Bridge leo.
“Ningependa kuangalia mechi ya Tottenham lakini nitakuwa kwenye ndege natokea Italia,” Alisema Ranieri. “Mama yangu ana umri wa miaka 96 na napenda kula naye chakula cha mchana leo kabla sijarudi Uingereza kwa hiyo nitachelewa.”
Kocha huyo raia wa Italia hajawahi kushinda taji la ligi katika kazi ya ukocha, lakini Leicester ina kila dalili ya kumpa nafasi hiyo ikiwa hadi sasa inahitaji pointi mbili tu ili kutangaza Ubingwa kufuatia sare yao ya 1-1 na Manchester United hapo jana.
“Katika mawazo yangu, Tottenham itashinda mechi zote tatu, “ alisema. “Mimi nafikiria mechi dhidi ya Everton ni lazima tuendelee kucheza kwa makini ili tuendelee kushinda. “


Lulu Michael:Mastaa Bongo Mtaishia Kuchambana Instagram tuu


ZA uso laivu! Staa mwenye mvuto Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa mastaa wengi Bongo wataishia kuchambana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram badala ya kutafuta elimu ili siku moja wapate nyadhifa serikalini.
lulu2342 (1)
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Lulu alisema kwamba, amegundua kuwa elimu ndiyo kila kitu hivyo amewasihi mastaa wenzake waache kuchambana na kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii badala yake watafute njia ya kujikwamua kielimu.
Bonyeza HAPA kudownload application ya UDAKU SPECIAL kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Labels: Bongo Movies , Lulu Michael
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
“Jamani mmemuona mwanamama mwenzetu Dk. Tulia alivyojinyakulia unaibu spika? Hiyo ndiyo raha ya elimu. Mastaa kazi kutukanana kwenye mitandao ya kijamii na kuweka picha, mwisho wenu utakuwa hivyohivyo,” alisema Lulu.


Meya wa Kinondoni Agawa Bure Maeneo ya Biashara Leo na Kufuta Umiliki wa Vibanda na Vizimba 100

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob amezua taharuki kwa wamachinga wa ubungo na kukimbia biashara zao wakiambatana naye mithili ya Maandamano mara baada ya kutangaza kufuta umiliki wa vizimba na mabanda takriban 100 yaliyokuwa yakimilikiwa na watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika soko la Mawasiliano Maarufu kama Simu 2000 akiagiza wapewe bure.
Mstahiki Jacob aliyefuatana na watendaji wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu akiongea na wamachinga mmoja mmoja na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi ubungo maji akiwaelimisha umuhimu wa oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia za juu na kuanza kwa usafiri wa mabasi ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale alipotaja Manispaa kuwa na masoko 26 yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia Mikataba ya kupangisha wakati wamejiagawia bure.
Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob amesema katika kuhakikisha wafanya biashara wadogo wanatengewa maneo yao watafanya uhakiki katika masoko yote kubaini viongozi na watendaji waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili masoko yatumiwe na walengwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku mtendaji wa kata ya ubungo Bw. Gilbati Mushi akieleza hatua hiyo kudhirisha utawala bora.


Zitto: Millioni 50 za Magufuli Kila Kijiji ni Hadaa Kwa Wananchi.

MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Serikali ya Awamu ya Tano imewahadaa wananchi kuhusu kuwapa Sh. milioni 50 kila kijiji/mtaa huku akiamini ahadi hiyo haitekelezeki.
Zitto alisema ahadi hiyo "kimahesabu, haitekelezeki."
"Kwanza kwenye bajeti ya Waziri Mkuu, fungu lililotajwa la Sh. bilioni 59 halipo. Na hata kama lipo Tamisemi wanakodai wao (Ofisi ya Waziri Mkuu), halitoshi kuvikopesha vijiji vyote Tanzania," Zitto alisema na kuongeza:
"Sh. bilioni 59 katika mwaka wa fedha 2016/17 maana yake vijini 1,000 tu vitapatiwa fedha. Kama serikali inatekeleza ahadi hiyo kwa vijini 1,000 kila mwaka, maana yake ni kwamba katika miaka mitano ya Rais Magufuli Ikulu, ahadi hiyo itatekelezwa katika vijiji 5,000 tu.
"Huku ni kuwahadaa wananchi. Tanzania ina zaidi ya vijiji 15,000. Kwa fungu linalotengwa, vijini zaidi ya 10,000 havitapata fedha hii."
MASHARTI MAGUMU
Wakati Zitto akitoa tahadhari hiyo, imebaini kuwepo kwa vigezo vya kupata fungu la Sh. milioni 50 za kila kijiji/mtaa ni vigumu.
Akihitimiha mjadala wa makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2016/17 wiki iliyopita Majaliwa, alivitaja vigezo saba vitakavyotumika kugawa fedha za mradi huo, huku vyote vikionekana vitakuwa na ugumu kunufaisha wananchi wengi hasa katika maeneo ya vijijini.
Majaliwa alisema mradi huo unalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa njia ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia ushirika wa kuweka na kukopa katika vijiji.
Alivitaja vigezo vya kukopeshwa fedha hizo kuwa ni kikundi cha kifedha kiwe kimesajiliwa na Halmashauri na Tume ya Ushirika, kikundi kiwe na Katiba, uongozi uliochaguliwa kidemokrasia na kupata mafunzo ya mikopo pamoja na kikundi hicho kuwa chini ya Asasi ya Kiraia inayotambulika na yenye uzoefu wa shughuli za mikopo.
Majaliwa alikitaja kigezo cha nne kuwa ni kikundi husika kionyeshe uzoefu wa kukopeshana kwa muda wa mwaka mmoja tangu kuanzishwa na historia ya urejeshaji mikopo ya asilimia 95 na cha tano ni kuwa dhamana ya serikali itakuwa kwenye kiasi cha msingi cha mkopo na si kwenye kiasi riba.
"Kigezo cha sita ni kikundi kuweka amana ya akiba ya fedha kwenye benki katika akaunti maalumu (Fixed Deposit) asilimia 10 ya mkopo," alisema.
Majaliwa alisema kigezo cha saba ni kuzingatiwa kwa Sheria ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2013 kuhusu mkopo kwa SACCOS.
Alisema serikali imeandaa mpango wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala hilo hususan masuala ya ujasiriamali na biashara
Chanzo: Siasahuru.com


Prof. Tibaijuka: Rais Magufuli Aache Kutumbua Nyama Akayaita Majipu..Wengine Tunatolewa Kafara na Mtandao Hauguswi

Akiongea na Count Down ya Clouds Fm Prof Tibaijuka amesema yeye ni muhanga wa ufisadi. Amesema kuna mtandao wa mafisadi unaotoa watu kafara na wenyewe hauguswi.
"Naafiki kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi, labda itasaidia kukamatwa na kushitakiwa mafisadi wenyewe. Maana wengine tunatolewa kafara na mtandao hauguswi, labda zitaachwa kukamuliwa nyama na kuziita majipu". Alisema Prof Tibaijuka.
My take:
Mtandao huu ni upi? Unalindwa na nani? Hivi Prof ni msafi au anajitetea?


Mch. Peter Msigwa, kwa Mahojiano ya ITV Jana Umechemka

Kama vile amesahu ahadi za Ukawa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Jana Msigwa alipinga vikali swala la elimu bure huku akipata kigugumizi kujibu kwa ufasaha Maswali ya Muandishi wa ITV. Kwa hili kweli kabisa Mimi nimekushusha kabisa kwasababu Muitikio wa elimu bure ni mkubwa sana na kila mtu anafaidi keki ya Taifa kupitia hili la elimu bure na bila shaka ni jambo bora kabisa kumpa mtoto wa kitanzania elimu.
Pili ni kupinga swala ya Kubana matumizi hasa kutotumia hela kwenye sherehe na kuzielekeza kwenye Maendeleo ni jambo jema kabisa kila mtu analisapoti kasoro wewe tu Mtumishi. Magufuli anania ya dhati kuua Siasa za kuropoka ropoka . Zije siasa za watu wabunifu kama Professa J maneno machache vitendo vingi.