Kutoka
88.1 Mwanza ambapo Polisi wamekamata viongozi sita na wafuasi kadhaa wa
(CHADEMA) waliokuwa wakijiandaa kuandamana baada ya kukaidi amri ya
polisi kusitisha maandamano.
Ni September 25 saa 5.40 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao
kujipanga kwa maandamano yaliyokuwa yaanzie viwanja vya Sahara mpaka
ofisi za mkuu wa wilaya ya Nyamagana na kufanya mkutano mfupi wa hadhara
kufikisha ujumbe.
Purukushani ilidumu kwa zaidi ya dakika 120 ikiambatana na wafuasi
hao kupigwa virungu huku taarifa zisizo rasmi zikisema Polisi wamewatia
mbaroni watu 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Kwa mujibu wa ripota wa nguvu Paul Luvega, licha ya
kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado
halijatoa taarifa kamili ambapo John Nzwalile katibu wa CHADEMA Mwanza
amesema >>> ‘naweza kusema kwa
ujumla tumefanikiwa, Polisi ndio wameandamana kwa wingi kuliko hata
sisi, tokea asubuhi ukienda chooni au kunywa chai Askari kanzu
wanakufatili, ukinywa chai na wao wanajifanya wanakunywa chai‘
‘Niseme maandamano yetu yamefanikiwa kwa sababu yalikua yamepangwa
kwa akili kubwa sana, tuliandamana kuanzia kichwani… hatukuandamana
ovyoovyo, hawakujua tunaanzia wapi tunaishia wapi…. tumeshangaa Polisi
wamekuja na vifaa utadhani unaangalia movie ya vita’
‘Mpaka sasa taarifa nilizonazo mwenyekiti wangu wa Nyamagana
amekamatwa, Katibu mwenezi Nyamagana, Mwenyekiti kata ya Bugogwa, Katibu
wilaya ya Ilemela wamekamatwa…. watu ambao kosa lao ni kuwaambia
Watanzania kuna pesa inaliwa na Wabunge kwenye batili la katiba’
‘Kwa kauli moja ya chama niseme tu kwamba maandamano na migomo
isiyokua na kikomo itaendelea…. tunazidi kujipanga vizuri kuangalia
namna bora zaidi ya kuandamana, tunataka watu wetu watoke Wanasheria
wetu wanajipanga…. kuhakikisha wanatoka bila masharti’
0 comments:
Chapisha Maoni