Ijumaa, 5 Desemba 2014
Home »
» MKUU WA USALAMA WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHINA AKAMATWA
MKUU WA USALAMA WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHINA AKAMATWA
Aliyekuwa mkuu wa usalama nchini China Zhou Yongkang amefukuzwa kutoka Chama cha Kikomunisti na atafunguliwa mashtaka huku kukifanyika uchunguzi wa ufisadi. Zhou alikuwa kiongozi wa kitengo cha usalama cha China kabla ya kustaafu miaka miwili iliyopita na atakuwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa chamani kutuhumiwa kwa madai ya ufisadi na kufunguliwa mashtaka. Uamuzi wa kumkamata na kumtimua afisa huyo mkuu wa Kamati kuu ya chama cha Kikomunisti yenye wanachama 9 ulifikiwa katika mkutano wa baraza kuu la chama hicho lenye wanachama 25 hapo jana, kufuatia uchunguzi rasmi uliofanyika mapema mwaka huu. Zhou anatuhumiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na "kukubali kiasi kikubwa cha hongo" na "kujihusisha na vitendo vya uasherati na wanawake kadhaa". Washirika na jamaa kadhaa wa Zhou pia wanachunguzwa kwa madai ya rushwa.
0 comments:
Chapisha Maoni