Wakati
mkataba wake wa mkopo ukiwa umebakisha miezi nane kuisha, usajili
Radamel Falcao kwenda Manchester United umechukua nafasi kwenye vyombo
vya habari.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya
Uingereza ni kwamba Man United imekubaliana rasmi mahitaji binafsi na
mchezaji huyo kwa ajili ya kukamilisha usajili wa kudumu wa mchezaji
huyo wa Colombia.
Taarifa zinaeleza kwamba Man United
wanafanya jitihada zote kumaliza suala la usajili wa Falcao ili kuepuka
kila kilichotokea miaka mitano iliyopita katika usajili wa Carlos Tevez.
United walimsajili Falcao kwa mkopo kutoka Monaco siku ya mwisho ya usajili wa wakati wa kiangazi.
Wakiwa tayari wameshalipa ada ya mkopo wa
£6million kwa klabu ya Ufaransa, United pia walishakubaliana kimsingi na
Monaco kuwalipa kiasi cha £43.5m ikiwa wataamua kumchukua Falcao
kiujumla mwishoni mwa msimu.
Leo sasa imeripotiwa kwamba mkurugenzi
mkuu wa United Ed Woodward tayari amekubaliana na wawakilishi wa Falcao
kumlipa mshahara wa £250,000 kwa wiki mchezaji huyo pamoja, bonasi na
haki za taswira yake.
Manchester United pia imekanusha taarifa kwamba itakatisha mkataba wa mkopo wa Falcao ikiwa mchezaji huyo ataumia tena goti.
0 comments:
Chapisha Maoni