Jumatatu, 6 Aprili 2015
Chelsea yashinda huku Costa akijeruhiwa
Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose
Mourinho amesema kuwa ilikuwa hatari kumchezesha mshambuliaji Diego
Costa baada ya kujeruhiwa wakati wa ushindi wa Chelsea wa 2-1 dhidi ya
kilabu ya Stoke City siku ya jumamosi.
Costa alichukua mahala pake
Oscar wakati wa mapumziko huku mabao yakiwa 1-1, lakini alicheza kwa
dakika 10 pekee kabla ya kulazimika kutoka nje baada ya kupata jeraha
jengine.''Kama matokeo yangalikuwa 2-0 asingecheza.Lakini ilibidi tumchezesha .Kitengo changu cha matibabu kiliamua kumchezesha'', alisema Mourinho.
Amsema kuwa mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa wiki mbili .
Hii inamaanisha kwamba Costa ataikosa mechi dhidi ya QPR tarehe 12 mwezi Aprili na ile dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 18 mwezi Aprili.
SHAMBULIZI GARISSA:SERIKALI YAJITETEA
Serikali ya Kenya imeitetea idara
yake ya usalama kufuatia shutma kwamba ilichelewa kukabiliana na
shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa.
Shambulio hilo lilisitishwa baada wapiganaji wanne waliohusika kuuawa na maafisa wa polisi saa 15 baada ya kuvamia chuo hicho.Lakini naibu wa rais William Ruto anasema kuwa kundi la kwanza la polisi liliwasili katika chuo hicho saa moja baada ya shambulizi.
Amelipongeza jeshi la Kenya KDF kwa kile alichokitaja kua hatua za haraka.Lakini vyombo vya habari vimekuwa vikisema kuwa vikosi maalum vilivyowaua wapiganaji hao vilichelewa kufika katika eneo hilo kutokana na mfumo wa usafiri waliotumia.
Pia kuna madai kwamba maafisa wa polisi walifeli kuchukua hatua za dharura baada ya kupewa habari kwamba mmoja ya wauaji ambaye sasa ametambuliwa kama Abdirahim Abdullahi ni wakili na mwana wa chifu mmoja katika eneo la kazkazini mashariki.