Mlinzi wa klabu ya Paris St-Germain
David Luiz amevishtumu vyombo vya habari kwa kukosa heshima baada ya
kukanusha madai kwamba yeye hajawahi kushiriki katika tendo la ngono.
Ripoti
hizo zilianza kusambaa baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea
mwenye umri wa miaka 28 kusema katika instagram kwamba yeye na mpenziwe
''wako tayari kungojea''.Aliiambia BBC focus kwamba.''Dini yangu,ubaatizaji wangu,nafurahia.
Watu wanasema maneno kila mahala kuhusu iwepo mimi sijawahi fanya tendo la ngono.''Ukweli ni kwamba mimi nishawahi kushiriki katika tendo hilo''.
Aliongezea:Watu wengine katika vyombo vya habari hawaheshimu maisha ya watu.
Mimi ninawaheshimu wenzangu kwa hivyo sina bughudha ya aina yoyote.
0 comments:
Chapisha Maoni