Siku
moja baada ya shirikisho la soka nchini TFF kumtangaza mchezaji
Emmanuel Okwi kuwa huru na hivyo anaweza kusajiliwa na klabu ya Simba –
leo hii uongozi wa klabu ya Yanga umeitisha mkutano wa waandishi wa
habari na kuzungumza juu ya uamuzi wa keshi yao dhidi ya Okwi.
Uongozi wa Yanga umesema utapinga maamuzi
ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya
kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga,
Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo
yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua
sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la
mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya
TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi
ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika,
walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji
huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi
yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira yalikuwa
yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba
hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo
kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi
limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama
utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa
wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti
wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na
taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa
kimaslah
0 comments:
Chapisha Maoni