Home »
» ILICHOSEMA CLUB YA SIMBA JUU YA IVO MAPUNDA KUVUNJIKA
Zikiwa
zimebakia wiki mbili kabla ya kukutana na mahasimu wao wa jadi, Simba
imepata pigo kubwa katika timu kwa sababu kipa namba moja wa timu hiyo
Ivo Mapunda amevunjika kidole mazoezini Zanzibar jana asubuhi na
anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki nane.
Hatoweza kusimama golini wakati tiu yake ikicheza na Yanga October 12
2014 ambapo daktari wa Simba SC Yassin Gembe amesema Ivo aliumia wakati
anachupia mpira katika mazoezi ya asubuhi na kwa bahati mbaya mpira
ukamgonga kwenye kidole kidogo cha mwisho mkono wa kulia.
Gembe amesema Ivo alitoka mazoezini baada ya tukio hilo na baadaye
akapelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo ambako baada ya vipimo
ikagundulika amevunjika sana.
“Si kuvunjika kwa mzaha, amevunjika
sana na anatakiwa kupumzika kwa wiki nane, baada ya hapo aanze taratibu…
ina maana makadirio ya kurudi tena uwanjani ni hadi baada ya miezi
mitatu‘ – Gembe.
Kuumia kwa Ivo kunatoa nafasi kwa makipa chipukizi Hussein Sharrif
‘Cassilas’ na Peter Manyika kujibidiisha ili kuziba pengo lake ambapo
sasa Ivo anafanya idadi ya wachezaji majeruhi ambao ni tegemeo Simba
kufikia wanne baada ya Paul Kiongera anayetakiwa kuwa nje wiki sita,
Haroun Chanongo na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
Related Posts:
Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye Apata Ajali Mbaya ya Gari
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea
jijini Dar es Salaam.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi &… Read More
Hatimaye Mama Maria Nyerere Ampigia Kampeni Magufuli
CCM tayari wameshatengeneza video ya mama Maria Nyerere akiwaomba akina
mama wotewampigie kura Magufuli. Video hii iko inasambaa Whatsup.
Kaongea mengi kuwa ni mchapa kazi na Mwadilifu. Swali langu kwa bibi
angu mama Ma… Read More
Magufuli Asimamisha Jiji La Dar.......Asema Tanzania Inahitaji Rais Mkali. CHADEMA Wampokea Kwa Ishara Ya Vidole Viwili Juu
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema
nchi inahitaji rais mkali ili mambo yaende huku akishangazwa na mmoja wa
vigogo kufungua kesi kupinga mradi wa maji.
Amesema watu wa aina hiyo wataki… Read More
UKAWA Watishia Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Jumapili
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachoungwa mkono na Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimetishia kutoshiriki katika Uchaguzi
Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, R… Read More
Muonekano wa Gari ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, Toyota Land Cruiser Baada ya Kupata Ajali Mbaya Jana Usiku
Muonekano wa gari ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye,
Toyota Land Cruiser baada ya kupata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani
kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.
… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni