Kikao cha Bunge la Tanzania
kilichoahirishwa siku ya jana Novemba 29 ni moja ya vikao ambavyo
vilivuta hisia za watu wengi na kutengeneza historia nyingine mpya
kutokana na mjadala wa ishu ya Escrow, baada ya kikao hicho kuahirishwa
Wabunge Ezekiel Maige, Aeshi Hilary, David Kafulila na Mchungaji Peter Msigwa walizungumzia kuhusu maamuzi ya Bunge hilo.
“…Tumekuwa
na Bunge la kipekee sana katika muda wangu wa kuwa Mbunge karibu miaka
nane sasa, hii ni experience yangu ya kwanza kuwa na kipindi kigumu kama
hiki. Bunge limekuwa kwenye mtihani wa ama kuamua kulinda viwango vyake
vya utendaji wa miaka yote au kuamua kuwa na viwango tofauti…” —Ezekiel Maige.
“…
Niwaombe Watanzania wawe wavumilivu kila kitu kina wakati wake na muda
wake… Nilipongeze Bunge, nipongeze kamati ya usuluhishi vilevile
nimpongeze Waziri Mkuu kwa kukubaliana na haya, ninaamini Serikali
itachukua hatua zake…”– Aeshi Hilary.
“…Niliamini
siku zote kwamba kuna makosa yamefanyika katika utoaji wa fedha zile na
chunguzi za CAG, PCCB, na hatimaye kamati ya PAC zimeonyesha hivyo na
hatimaye Bunge limeweza kuchukua hatua hii. Kuna changamoto nyingi
katika kupambana na mambo kama haya, kuna vitisho, kudhalilishwa mimi
niliitwa ‘tumbili’ na kuna watu walitishia kuniua, lakini yote kwa
ujumla wake ni changamoto katika kupambania yale ninayoamini…” –David Kafulila.
“…
Tumetimiza wajibu wetu kuishauri Serikali, tumeona watu wengine
hawakutimiza wajibu wao… Upande wetu wa upinzani tuling’ang’ania kwamba
watu wawajibike, niwasihi wananchi tuendelee kushirikiana kwa sababu
mwisho wa siku hii ni nyumba ya kwetu sote mtu yeyote asiyetimiza wajibu
wake lazima abebe mzigo wake …”—Mchungaji Peter Msigwa.
0 comments:
Chapisha Maoni