Mkufunzi Gus Poyet aliihangaisha
timu ya Chelsea na kuwajaribu viongozi hao wa Ligi kupitia mchezo mzuru
wa timu yake Sunderland.
Chelsea ilishindwa kuliona lango la Sunderland kupitia ngome mahsusi ya Sunderland iliowazuia washambuliaji wake.Shambulizi kali ambalo nusra liiweke Chelsea kifua Mbele ni lile lakKiungo wa kati Willian ambalo liligonga chuma cha goli na kutoka nje.
Hatahivyo Mshambuliaji wa Sunderland pia naye alipiga mkwaju mkali uliogonga chuma cha goli la Chelsea huku Sunderland ikidhibiti safu ya kati na kuimarisha mashambulizi yake katika ngome ya Chelsea.
Mchezo huo ulikamilika na sare ya bila kwa bila na kuifanya Sunderland kuwa timu ya kwanza kuwazuia viongozi hao wa Ligi kufunga tangu msimu huu uanze.
Katika matokeo mengine Arsenal ilizuia kupoteza kwa mara ya tatu mafululizo pale walipoishinda West Brom ugenini.
The Gunners kama wanavyojulikana walianza mechi hiyo wakiwa na alama za chini zaidi baada ya kucheza mechi 12 katika kipindi cha miaka 32,lakini cichwa kizito cha mshambuliaji Danny Welbeck, kilihakikisha vijana wa Arsene Wenger wanatia kibindoni alama tatu.
Katika uwanja wa Old Trafford,bao la Robbin Van Persie Robin liliimarisha ushindi wa Manchester United dhidi ya Hull City na kuzima midomo ya wale waliokuwa wakijiuliza maswali mengi kuhusu hali ya mchezaji huyo msimu huu.
Miongoni mwa wakaosoaji wake ni kocha Louis Van Gaal ambaye aliyemuorodhesha mshambuliaji huyo katika mechi hiyo licha ya kudai kwamba alikuwa na mchezo m'baya wakati wa mechi kati ya Arsenal na Manchester wikendi iliopita.
Manchester United ilipata ushindi wa mabao 3-0 kupitia wachezaji wake Chris Smalling na nahodha Wayne Rooney.
katika matokeo mengine
Burnley 1 - 1 Aston Villa
Liverpool 1 - 0 Stoke
QPR 3 - 2 Leicester
Swansea 1 - 1 Crystal Palace
West Ham 1 - 0 Newcastle
0 comments:
Chapisha Maoni