Tulisikia kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji Marekani, Rais Kikwete alipewa masharti kadhaa na madaktari waliomfanyia upasuaji juu ya utaratibu wa kufanya katika kipindi cha miezi mitatu, ambapo moja ya masharti aliyopewa ni kutofanya kazi ngumu.
Katika ukurasa wa Facebook wa gazeti la Mwananchi, wamepost picha na story inayosomeka hivi; “..MAZOEZI:
Rais Jakaya Kikwete akifanya mazoezi katika Viwanja vya Ikulu, Dar es
Salaam, kutekeleza ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara
tatu kwa siku ili kuimarisha afya yake, baada ya upasuaji mwezi uliopita
nchini Marekani. Picha na Ikulu..“
0 comments:
Chapisha Maoni