Moja kati ya matukio yaliyochukua headline ni hili tukio la kukamatwa Daktari feki, Dismas Macha katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI)
akiwa amevaa sare za kazi kama Daktari ambapo hii inakuwa mara ya pili
kukamatwa akiwa anachangisha rambirambi kwa Madaktari akidai kuwa
amefiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo ya MOI, Dk Othman Wanin Kiloloma amesema; “Tumekuwa
tuna tatizo kubwa la kuletewa watu wanaokuja wao na kujitia ni
madaktari wakiomba watu pesa, wakiomba waweze kupewa takrima na hata
michango mingine na wamefikia hatua sasa ya kuwatapeli hata madaktari
wenyewe kwa kuomba michango na vitu vingine“
Leo
tumewaita Waandishi wa Habari kuwaeleza kisa cha mtu ambee amekuja na
kujitia yeye ni Daktari wa sehemu ya taasisi na anaomba michango
mbalimbali, na mtu huyu sii mara ya kwanza amekuwa akishikwa Muhimbili
sehemu tofauti kwa wakati tofauti kwa hiyo tumewaita ili muweze
kumtambulisha kwa jamii asiweze kudanganya watu wengine kwamba yeye ni
Daktari”– Dk. Kiloloma.
Mwananchi mmoja ambaye alikuwa mmoja ya watu walishuhudia mtu huyo kukamatwa amesema; “Suala
la Madaktari feki tatizo kubwa lililopo sio Madaktari feki kama hivyo
kuna Mahakimu feki, Madaktari feki, ukishaona mahali popote anatokea mtu
feki ujue kuna maslahi na tatizo kubwa linalojitokeza kwenye Hospitali
ni ukifika Madaktari wenyewe halisi wanataka fedha ili wakuhudumie, kwa
hiyo yoyote anaweza kujifanya feki kwa maana anakusanya fedha za
Watanzania alafu anatoweka kwa hiyo anakuwa amekula fedha…“
0 comments:
Chapisha Maoni