Leo ni siku ambayo mwili wa Marehemu Kapteni John Damian Komba umepumzishwa katika makaburi ya Kijijini kwao Lituhi, Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Leo kwenye kipindi cha Power Breakfast Clouds FM, alisikika Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumzia mchango wa Marehemu Komba kwenye suala la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi.
“Kwenye mgogoro wetu wa Malawi tulimchukua Kapteni Komba kwenda kutoa ushuhuda unaoonyesha kwamba Ziwa Nyasa kwa kweli mpaka ni katikati, ndio alikwenda kutoa ushuhuda.. Kapteni Komba alieleza
kwamba toka enzi za mababu zake na mabibi zake makaburi ya wazee wake
yako ndani ya maji, ukifika pale Lituhi na huwa wanachukua mitumbwi
wanakwenda kunyunyizia na kutoa baraka zao makaburi yale yako ndani ya
maji na bado yapo misalaba iko kule kwa hiyo akawa anauliza na yale
makaburi sasa yawe mali ya Malawi?“
Maji
ya Ziwa Nyasa yanakuja kwenye ardhi miaka yote na huchukua Shule,
huchukua Mahakama na makaburi ya wazee mbalimbali, huu ni ushuhuda
alioutoa Kapteni Komba tulipokwenda Malawi na ushuhuda uliochukuliwa na wasuluhishi kuonyesha kwamba Ziwa lile linakula ardhi ya Tanzania.
Komba
lilimleta hilo na alizungumza vizuri sana kwa hiyo katika diplomasia ya
mgogoro wa Ziwa Nyasa kati yetu na Malawi huyu alikuwa miongoni mwa
watu waliozungumza kwa niaba ya watu wanaokaa kwenye mwambao wa Ziwa
Nyasa kwamba mpaka kwa kweli upo pale katikati“
Aliwahi
kualikwa kwenda kusaidia kampeni kwa nyimbo zake, kwa hamasa zake na
wengine waliogopa wakimuona ameingia kwenye nchi, wanatuletea barua
kutuambia bwana muondoeni haraka sana.. akikupigia kampeni kushindwa
haiwezekani.. tumepoteza mtu, tumepoteza shujaa, tumepoteza mkereketwa,
tumepoteza kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele kukiletea chama cha
mapinduzi ushindi miaka nenda rudi“– Waziri Bernard Membe.
0 comments:
Chapisha Maoni