Rais John Magufuli anaongoza  kura za kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa 
Person of The Year’, ambayo hutolewa kwa watu walioonyesha mchango kwa 
jamii.
Huku zikiwa zimebaki siku 21 kwa mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa, Rais 
Magufuli anachuana na Rais wa Mauritius,  Ameenah Gulib;  Mwendesha 
Mashtaka wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela; Mwanzilishi wa Capitec Bank,
 Michiel Le Roux na Taifa la Rwanda.
Mpaka jana jioni, Dk Magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 75 
likifuata Taifa la Rwanda na nafasi ya tatu alikuwa Madonsela wa Afrika 
Kusini.
Rais Magufuli anayetimiza mwaka mmoja madarakani wiki ijayo, utendaji 
wake umeonekana kuwagusa wananchi wa kipato cha chini, hasa kwa falsafa 
yake ya Hapa Kazi, uwajibishaji na mikakati yake ya kubana matumizi ili 
kuokoa fedha kwa kuzuia sherehe zisizo na tija.
Jumatano, 26 Oktoba 2016
Home »
 » Rais Magufuli Aongoza Kura Kuwania Tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni