Wapiga kura wengi wameripotiwa
kujitokeza kwenye kura ya maoni nchini Ireland ya kuamua iwapo ndoa za
watu wa jinsia moja zinaweza kuhalalishwa .
Katika sehemu nyingine ukiwemo mji mkuu Dublin na miji mingine, idadi ya wapiga ilitarajiwa kufikia takriban asilimia 60.Wataalamu wengi wa Ireland walio katika mataifa ya kigeni walirudi nyumbani kupiga kura.
Wale wanaounga mkono ndoa za jinsia moja walitarajia watu wengi kujitokeza.
Ikiwa kura hiyo itafanikiwa Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kupitia upigaji kura.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo.
0 comments:
Chapisha Maoni