Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi amemtumia salamu za pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape
Nnauye kufutia kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na
Michezo katika serikali ya awamu ya tano.
Katika salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF
ina imani nae katika nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika michezo
na haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya mpira wa miguu
nchini.
Aidha pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti
wa chama cha soka moa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa
hiyo, na James Bwire mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya
wa manispaa ya Nyamgana.
Malinzi amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo
walizozipata za kuwatumikia watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira
wa miguu nchini anawatakia kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.
0 comments:
Chapisha Maoni