Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii imeandaa kampeni kwa ajili ya ugawaji wa
vyandarua vya hati punguzo katika kaya nchini, inayotarajiwa kuanza
mwezi Aprili mwaka 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Wizara
hiyo Mhe.Dkt Kebwe Stephen, amesema kampeni hiyo imeanzishwa ili kuziba
pengo kutokana na kusitishwa kwa huduma ya hati punguzo iliyokuwa
ikifadhiliwa na Mennonite Economic Development Associates (MEDA) mapema
mwezi Juni 2014 .
Dkt.
Kebwe aliongeza kuwa jamii pamoja na wakina akinamama wajawazito
watanufaika na kampeni hiyo, ikiwemo ile ya ugawaji wa vyandarua kwa
wanafunzi shuleni ambayo imeanza kutekelezwa tangu mwaka 2013 kwa mikoa
ya Lindi,Ruvuma na Mtwara.
“kampeni
hii ni muhimu na ni mojawapo ya njia mbadala ya kuendelea kuwasaidia
akinamama wajawazito na watoto wachanga kujikinga na ugonjwa wa malaria
ikiwa ni mkakati wa kupunguza vifo vya akinamama na watoto”alisema
Mhe.Dkt. Kebwe
Aidha,
jumla ya vyandarua milioni 13 vimesambazwa kupitia mpango huo, ambapo
imechangia katika kuongeza matumizi ya vyandarua kwa akinamama
wajawazito kutoka 16% mwaka 2004 hadi 75% mwaka 2012 na kutoka 16%
hadi 76% kwa upande wa watoto.
Pia
alifafanua kuwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua itaendelea
kutolewa Kwa watumiaji wa vyandarua hivyo, kwani baadhi ya watu wamekuwa
wakitumia tofauti kwa kufugia kuku na hata wengine kuweka katika
bustani ili kukinga ndege waharibifu badala ya kujikinga na mbu.
0 comments:
Chapisha Maoni