Alhamisi, 24 Julai 2014
Home »
» Ban Ki Moon asema Iraq inapaswa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa
Ban Ki Moon asema Iraq inapaswa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa
Watu waliokuwa na silaha wameushambulia msafara uliokuwa umewabeba wafungwa kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, na kusababisha makabiliano makali na majeshi. Wafungwa zaidi ya 50 na wanajeshi kumi wameuawa katika shambulizi hilo lililodhihirisha hali ya kutokuwa na amani nchini Iraq. Hii ni hata baada ya wabunge kumchagua leo mwanasiasa kigogo wa Kikurdi Fouad Massoum kuwa rais mpya. Massoum mwenye umri wa miaka 76, alipata kura 211 kati ya 228 na sasa anachukua nafasi ya Jalal Talaban ambaye mihula yake miwili ya uongozi wa miaka kumi imekamilika. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon aliwasili nchini humo mapema leo akiwaomba wabunge "kutafuta msimamo wa pamoja" ili waweze kuutatua uasi unaofanywa na kundi la itikadi kali za kiislamu linalojiita Dola la Kiislamu, pamoja na wanamgambo wa Kisunni ambao wameiteka miji kadhaa ya kaskazini na magharibi mwa Iraq. Akizungumza pamoja na Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki, Ban amesema Iraq inakabiliwa na "kitisho kikubwa, lakini kinachoweza kutatuliwa kama itaunda serikali inayowahusisha viongozi wa matabaka mengi.
0 comments:
Chapisha Maoni