Kesi ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa kalenda kwa mara nyingine tena kwa sababu Hakimu anayeendesha kesi hiyo kupata shughuli nyingine nje ya ofisi.
Mbasha alipanda kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya
Ilala kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo ambapo mwendesha
mashtaka Kiyoja Catherine aliahirisha kesi hiyo kutokana na Hakimu
Williberforce Luwhego kupata dharura.Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena 17 October mwaka huu
ambapo Mahakama itaanza kusikiliza ushahidi ambapo upande wa mashtaka
utakuwa na mashahidi wanne kwenye kesi hii inayomkabili mume wa Flora
Mbasha anaekabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mara ya mwisho kabla ya hii kuahirishwa Flora Mbasha
alikwenda Mahakamani kwa mara ya kwanza akiwa na watu wake na hakukutana
wala kuongea na mume wake ambapo muda mfupi kesi hiyo ikaahirishwa.
0 comments:
Chapisha Maoni