Jumatatu, 22 Septemba 2014

WATU 115 WAFARIKI KANISANI NIGERIA

 
Muhubiri T.B Joshua amewashangaza wengi kwa kusema aliona ndege ikizunguka jengo hilo kabla ya kuporomoka

Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa watu miamoja na kumi na tano wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki baada ya kanisa kuporomoka nchini Nigeria.
Idadi kamili ya raia wa Afrika Kusini waliofariki ilikuwa 84.
Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo la 'All Nations' mjini Lagos, ambalo linaongozwa na mhubiri T.B. Joshua.
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe kuporomoka.

Related Posts:

  • Aliyewakosoa Sasha na Malia ajiuzuluSasha na Malia walikosolewa kwa kuvalia sketi fupi mbele ya umati katika White House Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obam… Read More
  • BARNES:GERRAD BADO MZURI KWA LIVERPOOLSteven Gerrard bado ana kiwango cha juu kuendelea kuitumikia Liverpool Winga wa zamani wa Klabu ya Liverpool John Barnes anaamini kiungo na nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard, bado ni mzuri vya kutosha kuendelea kuitumik… Read More
  • MKE WA KIONGOZI IS AKAMATWA                      Kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdadi Vikosi vya usalama nchini Lebanon vimemkamata mkewe kiongo… Read More
  • Al Shabaab waua 36 Mandera,Kenya                                   Wapiganaji wa Al Shabab&n… Read More
  • Man city wazidi kupanda                Wachezaji wa Klabu ya Man city  Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema ushindi wa timu yake dhidi ya Southampton unadhi… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni