Jumatatu, 22 Septemba 2014

MANUEL"CHELSEA NI TIMU NDOGO"

Pellegrini ameikejeli Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo 
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ameikejeli Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo timu hizo zilipoambulia sare ya Moja kwa moja uwanjani Etihad.
Andre Schurrle ndiye aliyeiweka Chelsea mbele kabla ya mchezaji wa akiba Frank Lampard kuisawazishia man City ambayo ilikuwa na wachezaji . Pellegrini, 61,alisema "nafikiri tulicheza dhidi ya timu ndogo iliyokuwa inalinda ngome yake wala haitaki kucheza mbele.
Sio jambo la kufurahisha kamwe .
Wachezaji wangu 10 walilinda ngome yao na kupata bao la kusawazisha hadi tamati ya mechi.''
Pellegrini alifananisha mchezo wa Chelsea na ule wa Stoke ambayo iliilaza City 1-0 mwezi uliopita nyumbani kwao.
''Nafkiri tulicheza dhidi ya timu sawa na ile ya Stoke .Ilikuwa vigumu sana kwetu kufunga bao kwa sababu walikuwa wanalinga ngome yao badala ya kucheza mchezo wa hadhi inayostahili''
Sina haja ya kuwatathmini hata kidogo hilo nawachia timu zingine ''
City ilitoka nyuma na kusawazisha hata baada ya mlinzi wa kutegemewa Pablo Zabaleta kuoneshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea visivyo mshambulizi mpya wa Chelsea Diego Costa.
Kwa upande wake kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikataa kata kata kujibu madai hayo ya Pellegrini akisema ''mbona yeye husema kuwa hazungumzi kuhusi mimi na timu yangu ilihali anaendelea kupiga domo ?
Usiniulize chochote kumhusu Manuel"

Related Posts:

  • Je Amisi Tambwe atacheza leo! Simba watoa majibu hapa MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Amisi Tambwe juzi alizua hofu kwa kocha Patrick Phiri na rais wa klabu hiyo, Evans Aveva baada ya kuumia mazoezi Uwanja wa Boko , Dar es Salaam. Tambwe aliumia goti baada ya kugongana na beki Abdi… Read More
  • HATMA YA AFCON 2015 ? Shirikisho la soka barani afrika CAF limewaondoa mashindanoni waliokuwa wenyeji wa michuano ya AFCON Morocco baada ya taifa hilo kushikilia msimamo wake wa kutokuwa tayari kuandaa michuano ya AFCON mwaka 2015 kutokana na… Read More
  • Mtoto wa kizazi cha 'msaada' azaliwa  Womb Transplant baby  Mwanamke mmoja nchini Sweden amejifungua mtoto kutokana na kizazi alichowekewa kupitia upasuaji. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 alizaliwa bila kizazi kabla ya kuwekewa kizazi cha m… Read More
  • Tanzania vs Uganda katika Kickboxing. Mtanzania anayefanya vizuri kwenye mchezo wa kickboxing Emmanuel Shija hivi karibuni ataipeperusha bendera ya Tanzania nchini Uganda wakati atakapopanda ulingoni kupambana na  Mganda Moses Golola katika pambano la … Read More
  • Wanajeshi 9 wa Umoja wa Mataifa wauawa  Mwanajeshi wa Umoja wa Matifa mali  Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Mali unasema kuwa watu waliokuwa na silaha ambao walikuwa wakitumia pikipiki wamewaua walinda amani tisa wa Umoja wa Mataifa kaskazini ma… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni