Alhamisi, 18 Septemba 2014

MAN CITY YAANZA VIBAYA UEFA

 
Man City ilipata kichapo cha goli moja bila jibu
Mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia leo za Klabu Bingwa barani ulaya ambapo Manchester City walianza vibaya michuano hiyo baada ya kupata kichapo cha goli moja bila majibu kutoka kwa wenyeji wao Bayern Munich ya Ujerumani.
Goli la Bayern Munich lilifungwa na Jerome Boateng katika dakika 90
Wakati Man City wakiadhibiwa ugenini na Bayern Munich, wenzao Chelsea wakiwa nyumbani Stamfode Bridge walitoka sare ya goli moja kwa moja na Schalke.
AC Roma ya Italia wao waliadhibu CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 5 -1 huku Ajax na Paris St. Gamaine ya Ufaransa zikitoka sare ya moja kwa moja.
Bacelona wao waliamua kuushikisha adabu Apoel ya Syprus kwa kuifunga goli moja bila majibu wakati FC Porto ya Ureno wakifungulia mvua ya magoli iliyoambatana radi pale ilipowanyeshea wapinzani wao Bate Borisov ya Belarus kwa jumla ya magoli 6 bila majibu.
Matokeo mengine NK Maribor ya Slovenia ilitoka sare ya 1 - 1 na Sporting Lisbon ya Ureno huku Athletic Bilbao ya Hispania zikitoka uwanjani bila kufungana na Shaktar Donetsk ya Ukraine.

Related Posts:

  • Listi ya mastaa wa Real Madrid watakao tembelea bongoVODACOMA Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara ya magwiji waliocheza kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Real Madrid. Kikosi cha magwiji hao maarufu kama `Real Madrid Legends` kitafanya ziar… Read More
  • Ajali ya Ndege:Miili imewasili Uholanzi Miili ya abiria wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Eindhoven Ndege mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mash… Read More
  • MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO MUWE MAKINI Gari aina ya Toyota Hilux limetumbukia kwenye mtaro uliopo Sinza-Makaburini jijini Dar es Salaam baada ya dereva aliyekuwa akiliendesha gari hiyo kushin… Read More
  • LOWASSA AKAGUA SHULE ILIYOUNGUA HUKO MONDULI Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo (Jumatano) asubuhi. Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake… Read More
  • AJALI YA NDEGE YAUA 51 TAIWAN Taswira kutoka eneo la ajali. Vikosi vya uokoaji vikiwa eneo la tukio. TAKRIBANI watu 51 wamepoteza maisha huku saba wakijeruhiwa baada ya ndege waliyokuwemo kuanguka iliposhindwa kutua kwa dharura huko Taiwan, nchini… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni