Home »
» Visa vya mapenzi haviishi…. huyu wa Dodoma kamuua mke kwa rungu, chanzo?
Siku
hizi mapenzi yamekua kama karata hivyo kila mmoja anacheza ajuavyo au
awezavyo kwenye huu uwanja mpana ambao kwa kiasi kikubwa miaka
inavyosogea ndio vifo vingi hutokea kutokana tu na visa vya mapenzi.
Taarifa kutoka Dodoma na kuthibitishwa na Polisi, zinahusu Wananchi
kupatwa na hasira na kumuua Mwanaume aliyemuua mke wake kwa kumpiga na
rungu tumboni kwenye kijiji cha Mzogole.
Mwanamke aliyeuwawa ana umri wa miaka 48 Mwajuma Chomola na mume wake
ambae ndio mtuhumiwa ana umri wa miaka 55 anaitwa Richard Kodi ambapo
kwa mujibu wa gazeti la HabariLEO, Mwanaume huyu alifariki dunia wakati akihudumiwa hospitali ya wilaya ya Mpwapwa.
Wakati uchunguzi ukiendelea, matokeo ya awali yanaonyesha chanzo cha
yeye kumuua mke wake waliekua wakiishi pamoja ni wivu wa kimapenzi na
kwamba ishu ilianzia pale Mwanamke alipochelewa kurudi nyumbani akitokea
kwenye sherehe iliyofanyika kwenye kijiji hichohicho wanachoishi lakini
mume alidhani mke kaenda kwengine.
Yaani sio kwamba alimfumania bali alihisi tu mke wake kaenda kwengine
ndio sababu iliyomfanya akachukua haya maamuzi, mara nyingi kwenye
mapenzi kumekua na kesi nyingi zinazosababisha Wanawake kupigwa au
kuuwawa kwa sababu tu Mwanaume anahisi vitu kama hivi bila kuwa na
ushahidi.
Related Posts:
Nyumba ya Mchungaji Lakatware Yasababisha January Makamba Kuchukua Hatua Kali Kwa Maafisa Hawa
SAKATA la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao
ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
w… Read More
Le Mutuz Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Amvaa Benard Membe..Adai Membe Ametukosea Sana Watanzania....
Lemutuz
Kufuatia kauli za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
kimataifa katika awamu ya nne Bernald Membe, kuonekana kupinga juhudi za
Rais John Pombe Magufuli kwenye masuala mbalimbali ikiwemo suala … Read More
Maswali 9 ‘Msukule’ Kukutwa Nyumba ya Tajiri Chini ya Shimo la Choo
Hofu
imeendelea kutanda maeneo ya Kibamba jijini Dar na kuacha maswali tisa
kwa wananchi kuhusiana na mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la urefu wa
futi kumi, nyumbani kwa mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja l… Read More
Kampuni ya UDA Yakanusha Kufilisika..Yadai ni Njama..Ripoti Kamili ipo Hapa
Mabasi ya UDA
Kumekuwepo na taarifa za uwongo kwenye vyombo vya habari, hasa kijarida
cha Dira ya Mtanzania, na mitandao ya kijamii kuhusu uongo kuwa
kufilisika kwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA) Limited.
M… Read More
Diamond Platnumz: Baada Ya Nape Nnauye Mimi Ndo Waziri wa Habari Na Michezo Mtarajiwa
Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa
zaidi kwa vijana.
Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alis… Read More
Hii sasa ni hatari
JibuFuta