Jumamosi, 4 Oktoba 2014

Je Amisi Tambwe atacheza leo! Simba watoa majibu hapa

IMG_7718.JPG
MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Amisi
Tambwe juzi alizua hofu kwa kocha
Patrick Phiri na rais wa klabu hiyo,
Evans Aveva baada ya kuumia
mazoezi Uwanja wa Boko ,
Dar es Salaam.

Tambwe aliumia goti baada ya
kugongana na beki Abdi Banda na
kushindwa kuendelea na mazoezi hadi
akafungwa barafu baada ya kutibiwa
kwa muda na Dk Yassin Gembe.
Kocha Phiri alionekana mwenye
wasiwasi na kufuatilia kwa karibu hali
ya mchezaji huyo wakati akitoka nje. “Hakikisha anakuwa vizuri, ni
mchezaji wangu ninayemtegemea,”alisema Phiri
kumuambia Dk Gembe wakati anatoka
nje na mchezaji huyo.

Lakini sasa yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Stand United, mshambuliaji huyo aliyekuwa mfungaji bora msimu uliopita amethibitishwa kuwa fiti kuivaa timu hiyo ya Stand ambayo imepanda daraja msimu huu.
Tambwe anaweza kuanza leo kwenye safu ya ushambuliaji kwa pamoja na Emannuel Okwi.
Wakati huo huo kiungo Jonas Mkude amerejea kwenye timu baada ya kuandamwa na majeruhi kwa muda kiasi.

Related Posts:

  • WAATHIRIWA WA MABOMU MBAGALA WALALAMIKA Nyumba iliyoharibiwa na bomu kama inavyoonekana. Mkutano kati ya waandishi habari na Waathirika wa Mabomu Mbagala, ambao umefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mbagala Kuu ,jijini Dar-Es-Salaam mapema leo . Waathi… Read More
  • MFUNGWA AKUTWA NA SIMU MWILINI  Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ya Kenya imekuwa kero kubwa kwa maafisa wa magereza. Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza … Read More
  • Alichokiandika Steve Nyerere kuhusu kujiuzulu uongozi Bongo Movie.   Kupitia mtandao wa picha yaani Instagram aliyekuwa Rais wa Bongo Movie Unity,Steve Nyerere  leo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwenye klabu hiyo ya Bongo Movie huku akishindwa kuweka sababu iliyomfanya kujiu… Read More
  • WANACHAMA 100 WA BOKO HARAM WAUAWA   jeshi la Nigeria Jeshi la Nigeria linasema kuwa limewaua zaidi ya wanamgambo 100 wa kundi la Boko Haram kufuatia shambulizi la wapiganaji hao siku ya ijumaa kazkazini mashariki mwa jimbo la Borno. Vikosi vya ser… Read More
  • Shearer asema Welbeck atang'ara Arsenal  Mshambuliaji wa Arsenal Danny Wellbeck kushoto  Mshambuliaji mpya wa kilabu ya Arsenal Danny Welbeck anaweza kufunga mabao 25 kwa msimu mmoja ,hayo ni matamshi ya aliyekuwa … Read More

0 comments:

Chapisha Maoni