Ni mwaka mmoja tangu Mzee Nelson Mandela alipofariki
dunia, wananchi wameedhimisha mwaka mmoja toka waondokewe na kiongozi
huyo ambaye aliiongoza nchi hiyo kutoka mikononi mwa Makaburu baada ya
kufungwa miaka 27 jela.
Maadhimisho hayo yametanguliwa na ibada
ya maombi ambapo wamekaa kimya kwa dakika tatu, na kisha kuweka mashada
za maua wakiongozwa na wazee waliopigana na makaburu wakati wa utawala
wa ubaguzi wa rangi, kumekuwa na upulizaji wa vuvuzela nchini kote,
kugonga kengele, ngoma, na kutakuwa na mechi ya mchezo wa kirafiki wa
kriketi.
Mandela alikuwa Rais wa kwanza mzalendo
kuiongoza Afrika Kusini kwa kipindi cha muhula mmoja wa miaka mitano
kuanzia mwaka 1994 hadi 1999 alipoachia madaraka kwa hiari yake
mwenyewe.
Maduka mengi ya kuchora Tatoo Nchini humo yameripoti ongezeko la watu wanaochora Tatoo za picha ya Mandela.
“… Kimwili hatuko nae lakini kiroho
Mandela tuko nae siku zote mpaka mwisho haijawahi kubadilika, Madiba
kiroho tuko nae kila siku, najua Madiba anatabasam, Madiba anafurahi kwa
sababu yeye ni miongoni mwa familia aliyochagua kuijenga”, alisema Mjane wa Mandela, Grace Machel.
Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, Desmond Tutu katika maadhimisho hayo ametoa wito kwa wananchi Afrika Kusini kuiga mfano wa Mandela.
0 comments:
Chapisha Maoni