WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemchagua Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza kuwa Katibu wao.
Rweikiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, ambaye safari hii hakuwania nafasi hiyo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Msekwa uliopo ndani ya viwanja vya Bunge, Katibu huyo mpya wa Wabunge wa CCM alikuwa akipambana na Mary Chatanda, Mariam Kisangi na Abdalah Ulega.
Wabunge wote wa CCM pia walipiga kura kuwachagua wabunge 10 kati ya 21 walioomba ujumbe wa NEC.
Waliochaguliwa ni Livingstone Lusinde, Dk Hamis Kigwangalla, Stanslaus Nyongo, Steven Ngonyani, Peter Serukamba, Faida Bakari, Agness Marwa, Munde Tambwe, Angella Kairuki na Jamal Kassim Ali.
Wabunge ambao kura hazikutosha ni Mbaraka Dau, Alex Gashaza, Hawa Ghasia, Ibrahim Raza, Profesa Norman Sigalla ‘King’, Almas Maige, Angelina Malembeka, Yahya Massare, Mattar Ali Salum na Hafidh Ali Tahir
Jumamosi, 7 Mei 2016
Home »
» Jason Rweikiza Achaguliwa Kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM
Jason Rweikiza Achaguliwa Kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM
Related Posts:
Nguvu ya Mapenzi itamrudisha Chris Brown kwa Karrueche? Soma alichokiandika @Instagram Weekend iliyopita imeisha kwa habari za kuisha kwa penzi la Chris Brown na Karrueche, halafu story kuibwa ya pili ikawa yale madongo ambayo kila mmoja akimtuhumu mwenzake kwamba ndiye sababu ya mapenzi yao kuisha.… Read More
Umeipata hii ya Daktari feki aliyekamatwa Taasisi ya MOI? Moja kati ya matukio yaliyochukua headline ni hili tukio la kukamatwa Daktari feki, Dismas Macha katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) akiwa amevaa sare za kazi kama Daktari ambapo hii inakuwa mara ya pili kukamatw… Read More
TAKWIMU MBAYA KWA ARSENAL. Hali ndani ya klabu ya Arsenal imezidi kuwa mbaya baada ya mashabikiw a klabu hiyo kuendelea kushinikiza kuondoka kwa kocha wao Arsene Wenger . Shinikizo hilo liliongezeka mwishoni wa wiki iliyopita wakati Arsenal ilipof… Read More
Kiongozi wa Al-Qaeda auawa Pakistan Kiongozi wa Oparesheni wa kundi la Al Qaeda auawa nchini Pakistan katika uvamizi. Kiongozi mwandamizi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda anayeshukiwa kupanga kulipuwa treni mijini New York na London ameuawa … Read More
DADA WA KAZI ALIYEMTESA MTOTO UGANDA AOMBA MSAMAHAJolly Tumuhirwe Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo. Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokif… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni