Kifo
 cha Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa 
CCM kapteni John Komba ambaye amefariki dunia akiwa hospital ya TMJ 
February 28 kilitanguliwa na kitu ambacho kinadhaniwa kama kilikua ni 
ishara ya siku yake ya mwisho.
Claudia John Komba ambaye ni mtoto wa 9 kati ya watoto 11 wa marehemu John Komba ameongea na youngluvega.blogspot.com
 na kuelezea baadhi ya vitu ambavyo kwao imekua kama kauli ya mwisho 
kutoka kwa Baba yao ambayo aliitoa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.
Claudia amesema >>>‘Taarifa
 ilinifikia mida ya saa 9 akasema anajisikia vibaya ambapo wakati yupo 
njiani akawa anaweweseka sana, tulipofika TMJ hospital walipofanya 
vipimo walisema ameshafariki’
youngluvega.blogspot.com Kabla ya hapo kulikua na ripoti ya mzee kuugua?
Claudia John Komba:
 ‘Zilikuwepo baba alikua amekaa ilikua mida ya asubuhi akawa analalamika
 anajisikia vibaya tukampeleka hospitali, tukagundua sukari imepanda 
sana na presha imepanda sana, akatolewa akawa anaendelea vizuri’
‘Juzi tarehe 26 february ilikua siku yangu 
ya kuzaliwa, akaita watoto wote akasema nataka kufanya birthday sababu 
birthday nyingi huwa zinanipita nakua nipo nje, akatukusanya watoto 
wote, aliongea maneno ya mwisho akatusihi watoto tupendane tusiweke  
matabaka kwamba huyu mdogo huyu mkubwa alisema yeye hana mkataba na 
Mungu’.






0 comments:
Chapisha Maoni