Ijumaa, 29 Mei 2015

Watoto elfu 250 huenda wakafa kwa njaa Sudan

Watoto elfu 250 huenda wakafa kwa njaa Sudan

Mshirikishi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, Toby Lanzer, amesema kuwa takriban watoto laki mbili u nusu wamo katika hatari ya kufa katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo iwapo mashirika ya utoaji misaada, hayatafikisha misaada kwa watu walio na mahitaji.
Wafuasi wa Rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar wanaendelea kupigana 

Bwana Lanzer ameiambia BBC kuwa, watu wanateseka kwa sababu ya umaskini.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini imesambaratisha uchumi wa taifa hilo.
Watoto zaidi ya laki mbili u nusu wamo katika hatari ya kufa kwa njaa

Amesema kwamba mashirika ya utoaji misaada yatafanya yawezavyo kuwasaidia wahitaji, lakini amani itapatikana tu nchini Sudan Kusini iwapo viongozi watakubaliana kukomesha mapigano.
Bwana Lanzer amewasihi viongozi wa pande hasimu kusameheana ilikukomesha maafa.

0 comments:

Chapisha Maoni