Jumamosi, 11 Machi 2017

DODOMA: Bashe, Malima na Musukuma Mbaroni Wakidaiwa Kupanga Kuhujumu Vikao Vinavyoendelea

Wabunge wawili Bashe na Musukuma wamekamatwa leo asubuhi kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza kutokana na kudaiwa kubeba ajenda ya "kwenda kumpinga Mwenyekiti".

Kundi hili la wabunge lililokuwa na mjumbe mwingine, Adam Malima lilipanga Peter Serukamba ndiye awe kinara wa kuanzisha hoja ya kumpinga mwenyekiti.

Hata hivyo, kabla ya kutimiza azma yao walijikuta mikononi mwa Polisi huku Serukamba akidhibitiwa na kukosa kuwasilisha hoja ya kumpinga mwenyekiti, Magufuli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibisha na kuwataja waliokamatwa kuwa ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Geita vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma na Malima.

“Hao ndio waliokamatwa na bado tunaendelea na mahojiano na wengine bado tunaendelea kuwatafuta,”amesema Mambosasa.

Chanzo chetu kimedokeza kwamba huenda wakaendelea kushikiliwa hadi pale mkutano mkuu utakapomalizika!

Chanzo:Jamii Forums

Related Posts:

  • NI ZAIDI YA VIPODOZI,NI ASILI VISIVYO NA KEMIKALI;ORIFLAME. Ni aina mbali mbali za vipodozi kwa wanaume na wanawake,vimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu visivyo na kemikali.Ni vipodozi asili kabisa kulingana na ngozi yako jaribu aina hizi uone maajabu ya vitu asilia. Bidhaa hi… Read More
  • MAN CITY YAANZA VIBAYA UEFA  Man City ilipata kichapo cha goli moja bila jibu Mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia leo za Klabu Bingwa barani ulaya ambapo Manchester City walianza vibaya michuano hiyo baada ya kupata kichapo cha goli moja bila m… Read More
  • OMBI LA WAFUNGWA HUKO KENYA  Mkuu wa magereza anasema hakuna nafasi za kuweka vyumba vya faragha kwa wafungwa kushiriki tendo la ndoa. Kamishna-Generali wa Magereza nchini Kenya Isaiah Osugo amekataa ombi la wafungwa kuruhusiwa kufanya tendo la… Read More
  • Polisi wadaiwa kutesa raia Nigeria Polisi nchini Nigeria wamedaiwa kuwatesa wanaume na wanawake pamoja na watoto. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International. Shirika hilo limechapisha ripoti yake ambayo inada… Read More
  • Vyombo vya habari,usalama vyakutana TZ Uhasama wa kiutendaji kati ya vyombo vya habari na vya ulinzi na usalama nchini Tanzania huenda ukapungua kwa kiasi kubwa baada ya pande hizo kuanza kukaa pamoja na kujadili mambo yanayokwamisha utekelezaji wa majukumu … Read More

0 comments:

Chapisha Maoni