Home »
» Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika Serikalini
Serikali imewataka wabunge wanaotaka utaratibu wa kulipwa pensheni mara baada ya kumaliza kipindi cha ubunge urejeshwe, walipeleka jambo hilo kwanza kwenye Tume ya Utumishi ya Bunge kabla ya kulifikisha serikalini.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amesema leo Jumanne bungeni kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo (NCCR_Mageuzi), James Mbatia.Mbatia amesema sheria ya mwaka 1981 ilikuwa inatambua pensheni kwa wabunge wanaomaliza muda wao na kuihoji Serikali inatamka nini kuhusu kulifufua suala hilo.Akijibu swali hilo, Mavunde amesema kwa sababu swali la mbunge huyo ni kufufua sheria ya pensheni ni vyema lianzie kwao ( Tume ya Utumishi ya Bunge) ndio lifike serikalini.Katika swali la msingi, Mbatia ametaka kufahamu Serikali haioni busara kuifanyia marekebisho Sheria ya Maslahi na Mafao ya Majaji namba 3 ya mwaka 2007 au vinginevyo ili majaji waweze kupatiwa huduma muhimu za matibabu wakati wanapostaafu.Akijibu Mavunde amesema masharti ya kazi na stahili za majaji ya mwaka 2013 kwa maana majaji wa Mahakama Kuu yamefafanua kuwa majaji hao wamejumuishwa katika utaratibu wa matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHF)wawapo kazini.Amesema gharama hizo hulipwa na Serikali na hata wanapostaafu wanaendelea kupata huduma hizo kupitia mfuko huo."Kwa wale waliostaafu kabla ya masharti hayo kuanza kutumika hawanufaiki na mfuko huo," amesema.Kuhusu kuangalia kulifanya suala hilo la kiutawala, Mavunde amesema kwa sababu ni suala la kisheria na sera wanalichukua na kulifanyia kazi.
Related Posts:
Ishara Za Kujua Iwapo Umemkuna Mwanamke Wako Vizuri Kunako 6 X 6..!!!
Leo acha niwape dondoo
kadhaa kuhusu namna ya kujua kama umemkuna ipasavyo mwanamke wakati wa tendo la ndoa.
1.Kufinya shuka kwa nguvu au kitanda kwa nguvu wakati unampa mambo
ni ishara mojawapo ya
kuonye… Read More
Ukweli Mchungu..Uwepo wa WCB; Bongo Fleva Inachungulia Kaburi...!!!
Hayo yote nayasema kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Adul Juma au
maarufu zaidi kwa jina la Diamond. Siku za hivi karibuni, Diamond
ameanzisha zoezi la kuwachukua wanamuziki na kuwaingiza kwenye kundi
lake maarufu s… Read More
Exclusive..Baada ya Kutemwa Yanga,Pluijm Kutua Taifa Stars,Mpango Mzima Uko Hivi..!!!
UNAAMBIWA ukiona cha nini mwenzako anasema nitakipata lini, kwani baada
ya Yanga kuamua kumtema kocha wao za zamani, Hans van der Pluijm, nyota
ya Mholanzi huyo imezidi kung’aa na sasa ana ofa mbalimbali kutoka ndani
… Read More
Kama Umeteseka kwa Muda Mrefu,Hizi Hapa Mbinu za Kuamsha Nguvu za Kiume Kwa Muda Mrefu..!!!!
Suala la nguvu za kiume kwa sasa limeshakuwa ishu kubwa kwa vijana wengi
wa sasa,kwa utafiti uliofanywa mwaka 2013 na shirika la Afya duniani
unaonesha kuwa zaidi ya asilimia themanini ya wanawake hawatoshelezwi
kimap… Read More
Jamani Nitoke Nnje ya Ndoa..?Nahitaji Ushauri Wenu...!!!
Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa!
Hakuna kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi
sana lakini huwa anadai haku… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni